Home » » CCM IRINGA MJINI WAZINDUA KAMPENI KWA KISHINDO MWIGULU ASEMA MSIGWA HATOSHI UBUNGE

CCM IRINGA MJINI WAZINDUA KAMPENI KWA KISHINDO MWIGULU ASEMA MSIGWA HATOSHI UBUNGE

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Monday, September 7, 2015 | 8:18 AMKamanda wa UVCCM Mkoa Salim Asas akiwa na aliyekuwa Mgombea Ubunge jimbo la Iringa Mjini Balozi Augustino Mahiga  leo ofisi za CCm Wilaya
Makada wa CCM
Balozi Mahiga akipokelewa
MWAKALEBELA Mgombea Ubunge akipokelewa
Aliyekuwa mbunge wa jimbo la Iringa Monica Mbega akipokelewa
Balozi Mahiga
Aliyekuwa Naibu Katibu mkuu ambae leo mgeni RASMI Bw Nchemna akiwasili
Mwakalebela katikati akiwa na mwigulu Kushoto kuelekea uwanja wa MwembetogwaBaadhi ya  wasanini wa  Bongo  Muvi wakiwa  jukwaani


Mwakalebela  akiomba kura
Mwigulu akiomba kura za CCM wakati wa uzinduzi wa kampeni za Ubunge jimbo la Iringa Mjini leo
Wananchi wakiwa juu ya miti baada ya uwanja kujaa

BENDI ya yamoto wakiwa kazini 

Kada maarufu wa CCM Bw Fahad Abri ambae ni Mdau wa wanahabari Mkoa wa Iringa na kiongozi wa mtandao wa matukiodaima akiwa katika mkutano
Mumbe wa mkutano mkuu wa CCM Taifa ARIF Abri mwenye kanzu katikati ,Katibu wa CCM Mkoa Bw Mtenga , Kamanda wa Uv CCM Salim Asas wakifuatilia mkutano wa uzinduzi wa kampeni za CCM 

 Na MatukiodaimaBlog  ,Iringa 

CHAMA cha mapinduzi ( CCM ) jimbo la Iringa Mjini wazindua mkutano wa kampeni za Ubunge kwa kushindo huku Naibu  Katibu mkuu mstaafu CCM Mwigulu Nchemba azindua kampeni za Ubunge jimbo la Iringa Mjini kwa kumnadi Frederick Mwakalebela huku akiwataka  wananchi kuchagua mtu wa kwenda kufanya Kazi ikulu ya kuwatumikia wananchi na sio wa kwenda kujaza nafasi inayoachwa wazi na Rais Dr Jakaya Kikwete

 Mwigulu ambae alikuwa mmoja Kati ya Makada wa CCM waliojitokwza kuwania Urais pamoja na Dr John Magufuli na Naibu Waziri wa fedha aliyasema hayo jana wakati akizundua kampeni hizo za CCM jimbo la Iringa Mjini katika uwanja wa Mwembetogwa.

Alisema kuwa Kati ya wagombea wa Urais wa Vyama vyote vya siasa hapa nchini na wale waliojitokeza kuwania nafasi hiyo ndani ya CCM hakuna hata mmoja anaye mfikia Dr Magufuli kwa uadilifu na uchapakazi pamoja na ufuatiliaji wa mambo na kuchukua hatua kwa wakati.

Bw Mwigulu alisema kuwa Dr Magufuli hajazungukwa na watu wa dili wala mtandao wa wakwepa kodi na kuwa mmoja Kati ya wagombea Urais toka Enzi za baba wa Taifa alikuwa hana sifa ya kuwa kiongozi kutokana na kuwa ni mtu wa kupiga dili kila sekta anayopewa.

" Mgombea wa upande wa pili toka Enzi za Mwalimu alikuwa amezungukwa na kuifanya Kazi ya kupiga dili kwenda mbele na sasa anataka kwenda mwenyewe Ikulu kuendeleza kupiga dili ..... Leo tunataka kupeleka genge la wapiga dili Ikulu .....tunasema hatuwezi kupeleka mpiga dili Ikulu "

Alisema kuwa mwaka huu watanzania wameanza kudanganywa  na genge la wapiga dili ili kuwapeleka Ikulu jambo ambalo ni hatari .

Bw Mwigulu akiwahutubia maelefu ya wakazi wa jimbo la Iringa ambao toka kuanza kwa mfumo wa vyama vingi chama hicho hakijapata kupata idadi hiyo ya watu ,alisema kuwa iwapo leo CCM wangemchukua mgombea wake Edward Lowasa hali ingekuwaje ndani ya CCM.

Alisema kuwa wapo ambao walikuwa wakipinga kwa nguvu zote Lowasa kuwa Rais akiwemo mwenyekiti wa Chadema Taifa Bw Freeman Mbowe na aliyekuwa mbunge wa jimbo la Iringa Mjini Mchungaji Peter Msigwa ambao leo wamegeuka kumtakasa waliyemwita fisadi ili awe Rais .

Aidha alisema kuwa umefika wakati wa watanzania kuchukiwa watu wanaolazimisha kupeleka Ikulu Rais wa kwenda kupumzika na kumuacha mtu wa Kazi Dr Magufuli.

" Ikulu wakati mwingine Baraza la mawaziri tunakesha hadi saa 9 usiku kupanga mambo ya kitaifa na Rais Dr Kikwete anaongoza .... Ila sasa hivi tunataka kupeleka Rais tia maji tia maji wa kupeleka Rais anayeweza kukesha na kuongea dakika tatu... tuache kulifanyia mdhaha Taifa"

Akimnadi Mwakalebela alisema kuwa wakati wana Iringa wanafurahia kutatuliwa Kero Yao ya kuuza mawazi baada ya kampeni ya Asas Dairies Ltd kuwekeza katika kiwanda Cha maziwa ila Mchungaji msigwa anasimama jukwaani kutaka watanzania kususia bidhaa zake kwa kuwa yupo Ccm .

Alisema wakati Mchungaji Msigwa na genge linalimpeleka Rais mpiga dili dawa Yao ni kutoswa Mwezi wa 10 kwa kumchagua Mbunge Mwakalebela ,Rais Dr Magufuli na madiwani wa CCM Kuchana na wale wanaotaka kutekelezwa matakwa Yao binafsi .

"Mimi nataka kuwaambia genge la wapiga dili kuwa hatuwezi kuiachia nchi hii kwa wapiga dili hadi sasa kwa mwonekano wa CCM kushinda unaonekana kuwapa kura Ukawa ni kujeruhi nafsi zao bure baada ya matokeo ya wazee waliohama CCM ndipo watatambua kuwa CCM ni ile ile .... DR Magufuli na Mwakalebela pamoja na madiwani watashinda tu"

Hivyo alisema kuwa wakimchagua Mwakalebela kwa kila jambo la Iringa atahakikisha anashirikiana kulipigania kwa nguvu zote .

Kwa upande wake Katibu wa CCM Mkoa wa Iringa Hassan Mtenga alisema chama kimejipanga kuzunguka kata zote kusoma bajeti ya mfuko wa jimbo ambayo wananchi wametapeliwa na aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo .

Bw Mtenga alisema kuwa hadi sasa ana faili la kila kata na kiasi cha Pesa za mfuko wa jimbo ambazo zingepaswa kupelekwa ila hakuna jipya hadi sasa na kumtaka mbunge huyo kuonyesha alikopeleka Pesa za wananchi.

Hata hivyo alimtaka Mchungaji Msigwa kusimama jukwaani kuwaeleza wananchi wake kwa miaka mitano kazi gani ya kimaendeleo ameifanya jimbo la Iringa Mjini zaidi ya kufanya maandamano na kupelekea vijana kufungwa.


Akiomba kura kwa wananchi hao Mgombea Ubunge jimbo la Iringa mjini Bw Mwakalebela alisema atahakikisha anafanya Kazi na makundi yote bila kuwabagua na vyama vyote atafanyanao Kazi.

Alisema kila kata atazunguka na kueleza kipaumbele chake na jinsi gani atakavyowatumikia wananchi hao wa jimbo la Iringa ambao wamepata machungu makubwa kwa miaka mitano hivyo kuwataka kuondokana na machungu hayo kwa kuchagua CCM

Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA