Home » » ZAIDI YA MIRADI 50 YENYE THAMANI YA SH. 10.3 BIL. KUPITIWA NA MWENGE WA UHURU MKOANI MOROGORO.

ZAIDI YA MIRADI 50 YENYE THAMANI YA SH. 10.3 BIL. KUPITIWA NA MWENGE WA UHURU MKOANI MOROGORO.

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Saturday, June 13, 2015 | 5:46 AM 
Na. Andrew Chimesela – Morogoro
 MKOA  wa Morogoro unatarijia kupokea Mwenge wa Uhuru kutoka Mkoa wa Tanga  Juni 15, 2015 ambao utakaopitia miradi ya Maendeleo 51 yenye thamani ya Shilingi 10,367,768,943 za kitanzania.

Ukiwa Mkoani Morogoro, Mwenge wa Uhuru utakimbizwa katika Halmashauri zote saba za Mkoa huo ambazo ni Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero itakayopokea Mwenge kutoka Wilaya ya Kilindi, Halmashauri ya Wilaya ya Gairo na Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro.

Halmashauri nyingine ni pamoja na Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro, Ulanga, Kilombero na Halmashauri Kongwe ya Wilaya ya Kilosa ambayo baada ya kukamilisha kukimbiza Mwenge huo itakabidhi Mkoa wa Iringa.

Ukiwa Mkoani Morogoro, Mwenge huo unatarajia kupitia miradi ya Maendeleo 51 yenye thamani ya shilingi 10,367,768,943/=ambayo itahusisha  kuzinduliwa kwa baadhi ya miradi, kuwekewa mawe ya msingi, kufunguliwa na miradi mingine kuonwa.

Kati ya miradi itakayopitiwa na Mwenge wa Uhuru, miradi tisa ni ya Sekta ya Elimu, inafuatiwa na miradi mingine tisa ya Sekta ya Afya, Miradi Saba Sekta ya Kilimo, miradi Sita ni ya sekta ya Maji na miradi sita mingine ya kuhifadhi Mazingira.

Miradi iliyobaki ambayo itapitiwa na mwenge huo ni ujenzi wa Ofisi za Watedaji wa Serikali kama Ofisi za kata/Vijiji, ujenzi wa vituo vya Polisi na Hoteli zilizojengwa na wananchi wenyewe kwa njia ya ujasiliamali. 

Miradi mingine ni nyumba za Kulala wageni, nyumba bora zilizojengwa na wananchi, uimarishaji wa Vikoba, vikundi hai vya waendesha pikipiki, maarufu kama Bodaboda, na shughuli nyingine za kijamii ambazo pia zitapitiwa na mwenge huo. 

Mwenge wa uhuru utamaliza mbio zake Mkoani Morogoro Juni 22, 2015 na kukabidhiwa Mkoa wa Iringa, Wilaya ya Kilolo, eneo la Ruaha Mbuyuni.
Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA