Home » » Ujerumani:Wahamiaji ni Muhimu

Ujerumani:Wahamiaji ni Muhimu

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Saturday, June 13, 2015 | 6:06 AM

Maafisa nchini Ujerumani wanasema kuwa idadi inayozidi kuongezeka ya wakimbizi wanaowasili kutoka nchini kama syria watasaidia kujaza pengo la ukosefu wa wataalamu.

Mwenyekiti shirika la ajira nchini Ujerumani aliliambia gazeti moja kuwa watu wanaokimbia syria, wengine wameelimika na hivyo wanakaribishwa nchini Ujerumani.

Wakimbizi 350,000 watarajiwa kutafuta ajira nchini ujerumani mwaka huu.

Ujerumani hupokea maombi mengi ya hifadhi kuliko nchi yoyote katika muungano wa ulaya na idadi hiyo inazidi kuongezeka.
Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA