Home » » StarTimes yazindua huduma zake mkoani Iringa

StarTimes yazindua huduma zake mkoani Iringa

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Friday, December 12, 2014 | 5:35 AM

Mkuu wa Wilaya ya Iringa Dkt. Leticia Warioba  (katikati) akipata maelezo namna ya kujiunga na vifurushi wa king'amuzi cha StarTimes kutoka kwa afisa habari na masoko, Erick Cyprian huku meneja wa tawi la StarTimes mkoa wa iringa Boki Shabani wakati uzinduzi  wa duka hilo
leo. 
Mwanafunzi wa darasa la nne wa shule ya msingi mlangali, manispaa ya Iringa, Grace Nyimbi akifurahia zawadi ya kalama kwa kujaribu kuandika wakati uzinduzi  wa duka hilo leo.


Mkaguzi msadizi wa wilaya, Ibrahim D.RC akipekea zawadi ya kisimbuzi kwa ya OCD Iringa kutoka meneja wa tawi la startimes mkoa wa iringa, Boki Shabani wakati uzinduzi  wa duka hilo leo.

Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Dkt. Leticia Warioba akipekea zawadi ya 
kisimbuzi huku meneja wa tawi la startimes mkoa wa iringa, Boki 
Shabani akishuhudia wakati uzinduzi  wa duka hilo leo. (PICHA ZOTE NA 
FRIDAYSIMBAYA)
Katika kuhakikisha watanzania wanafikiwa na matangazo ya uhakika ya digitali, kampuni ya startimes imezindua duka kwa ajili yakutolea huduma za  madishi (DTH) katika mkoa wa Iringa.


NA FRIDAY SIMBAYA
kwa huduma za kampuni hiyo mkoani iringa kunafanya idadi ya matawi nchi nzima kufikia 15 huku sehemu nyingine zikiwa mbioni kufunguliwa.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa duka hili jipya, Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Dkt. Leticia warioba alipongeza jitihada za dhati za kampunihiyokwa kuyaleta matangazoya digitali wilayani kwake kwani kilikuwa ni kilio kikubwa cha wananchi wake na ana imani kuwa fursa hiyo itatumika kuinua shughuli za kiuchumi.

“Hakuna asiyefahamu umuhumuwamatangazo ya televisheni nchini,kutazama televisheni sio kitu cha anasa kama ilivyokuwa ikitafasiriwa kipindi cha nyuma. Kupitia matangazo hayo wananchi wanaweza kutafuta taarifa mbalimbali za habari, maendeleo ya kiuchumi, kisayansi na kiteknolojia,”Dkt. Warioba alisema.

“Wakulima nawaombaa mtumie kutazama vipindi vinavyohusu kilimo,kupata taarifa za pembejeo na masoko. Wafanyabiashara tumieni fursa hii kuweza kujua maeneo sahihi ya kuwekeza, kuuza bidhaa zenu na pia kujua wafanyabiashara wenzenu sehumu nyingine. Hivyo hata wanafunzi nao watazamevipindi ambavyo vitawaongezea maarifa na ujuzi zaidi na kuweza kufaulu katika masomo yao,” aliongeza Dkt. Warioba.

Aidha mkuu wa wilaya ya Iringa huyo amewataka wananchi wake kuyapokea mabadiliko hayo mapya ya sayansi na tekinolojia kwa dunia nzima inabadilika na wao hawanabudi kufanya hivyo.

Alisemakuwa imekuwa kawaida kwa wananchi wengikulalamika linapokuja suala la kupokea mfumo mpya wa maisha, na kuongeza kuwa ‘information is power’ kwa lugha ya Kiswahili habari ni nguvu.

Aliwaasa wanairnga kutofanya hivyo bali wapokee kwa nguvu moja mabadiliko hayo wakiamini yatasogeza mbele zaidi maendeleo yao.

Kwa upande wake meneja wa duka hilo jipya mkoani Iringa, Boki Shabani alibainisha kuwa kuzinduliwa rasmi kwa huduma zao mkoani hapa ni jitihada za dhati kabisa za startimie kuhakikisha inwafikia watanzania popote pale walipo.

Alisema kuwa ni dhahiri kuwa dunia sas inakimbilia kufikia n2015 ambao ndio mwisho wa kutumia masafa ya analojia na kwa umakini wa serikali ya Tanzania imeamua kuanza mapema mchakato huu tangu 2010.

Ambapo mwaka 2012 mikoa mbalimbali ilizimwa kama Dar es Salaam, Dodoma, Arusha, Mbeya na Moshi na sasa mkoani Iringa.
Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA