Home » » Profesa Mpangala apinga sifa ya Mbunge kuwa ni kujua kusoma na kuandika

Profesa Mpangala apinga sifa ya Mbunge kuwa ni kujua kusoma na kuandika

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Friday, December 12, 2014 | 5:53 AM

THE Deputy Vice Chancellor Academics (DVCA) of Ruaha Catholics University (RUCU) Prof. G. Mpangala presenting his paper on the constitution and building democracy in 53 years of independence of Tanzania.

Na Friday Simbaya, Iringa

MAKAMU Mkuu wa Chuo Kikuu cha kikatoliki cha Ruaha (RUCU) ProfesaGaundence Mpangala amepinga hatua ya lililokuwa Bunge maalamu la katiba kuweke kipingele kinachotaja moja ya sifa ya Mbunge kuwa ni kujua kusoma na kuandika.Mpangala alitoa kauli hiyo juzi wakati alipokuwa akizungumza kwenye kongamano la siku ya uhuru iliyoandaliwa na serikali ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Katoliki cha Ruaha (RUCU) mkoani hapa.

Hivi karibuni lililokuwa bunge la katiba lilimaliza mchakato wake wa kuandika katiba inayopendekezwa mjini Dodoma na kuweka kipengele kinachotaja mmoja ya sifa za Mgombea Ubunge kuwa ni kujua kusoma na kuandika.

Alisema miongoni mwa mambo yanayopaswa kuondolewa katika katiba inayopendekezwa ni kipengele cha sifa ya Mbunge ya kujua na kusoma pekee na kuongeza kuwa inahitajika elimu ya kutosha kutokana na jukumu walilonalo wabunge.

"Katika suala la mchakato wa katiba hadi ulipofikia nampongeza Rais Jakaya kikwete kwa kuanzisha mchakato wa katiba mpya inayoendana na vyama vingi vya siasa vilivyopo kwa sasa,hapaamezingatia Demokrasia kwani lengo la kudai uhuru ni kupata Demokrasia"alisema Mpangala

"Hata hivyo mmoja ya vipengele vinavyotakiwa kuondolewa katika katiba ile ni hiki kinachosema sifa ya Mbunge inapaswa kujua kusoma na kuandika, Mbunge ni mtu muhimu,anatunga sheria na inapotokea Mbunge anakuwa na elimu ndogo anakuwa hana uwezo wa kupambanua mambo"aliongeza.

Katika kongamano hilo Mpangala alielezea kuvutiwa na kazi iliyofanywa na Tume ya Mabadiliko ya katiba iliyokuwa ikiongozwa na Jaji Mstaafu Joseph Warioba akidai rasimu waliyotoa ilizingatia hatamu,ushiriki,ukombozi wa wananchi na kuzingatia misingi ya kidemokrasia ikiwamo ushirikishwaji wa wananchi.

"Mimi ninaunga mkono rasimu ya katiba iliyopendekezwa na iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya katiba ya Jaji Warioba,rasimu ile ilizingatia vigezo vyote vya utawala bora ambapo inawataka wananchi kuiwajibisha serikali pamoja na viongozi pindi wanapokiuka maadili"alisema Mpangala.

Akichangia kwenye mdahalo huo Kaspal Mtotomwema aliiomba serikali kuchapisha katiba inayopendekezwa na kuisambaza kwa wananchi ili waweze kuisoma kwa madai kuwa hadi sasa wananchi wengi hawajaipata.


"Ingawa serikali inatushawishi tuipigie kura katiba
inayopendekezwa,hadi leo badohata ukienda katika maduka ya serikali
huwezi kuikuta,mimi ninashauri serikali izichape na kuzitawanya kw
awananchi ili tuweze kuisoma na kuielewa kabla ya mchakato w akuipigia
kura"alisema Mtotomwema.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa kongamano hilo mkuu wa wilaya ya
kilolo GERARD GUNINITA kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa iringa AMINA
MASEZA amesema kuwa ili kupiga hatua watanzania wanapaswa kuwa
wazalendo na kuthamini uhuru uliopo kwa kuzingatia maadili.

Amesema kuwa nchi ya china ilikuwa ikilingana hali ya kiuchumi na nchi
ya Tanzania lakini imepiga hatua kutokana na kuwa ilithamini Uhuru wa
nchi kwa kujali lugha ya taifa na masilahi kwa kuzingatia maadili
ambayo yaliendana na uzalendo.
Wakati huohuo, imeelezwa kuwa tatizo la ajira hapa nchini ni kubwa
kulinganisha na nchi nyingine zilizopo katika ukanda wa Afrika
Mashariki.
Kauli hiyo ilitolewa juzi na Mhadhiri Mwandamizi wa Sheria wa Chuo
Kikuu cha Katoliki cha Ruaha (RUCU)  Ross Kinemo.
Ross alilikuwa akizungumza kwenye kongamano lililoandaliwa na serikali
ya wanafunzi ya Chuo Kikuu cha Katoliki cha Raaha (RUCU Cha Mkoani
Iringa.
Mdahalo huo ulikuwa maalumu kwaajiliya maadhimisho ya miaka 53 ya
uhuru wa Tanzania bara.
Akitoa mada iliyohusu tatuzo la ajira nchini kwa vijana Ross alisema
kila mwaka vijana zaidi ya 700,000 wamekuwa wakiingia katika soko la
ajira na kuongeza kuwa kati yao ni 40,000 ndio huoata ajira.
Alisema idadi ya vijana waliokosa ajira kwa sasa hapa ni zaidi ya
asimia 11.8 taofuati na ile ya vijana wanaokosa ajira nchini ya Uganda
ambao ni asilimia 4.6.
Katika madahalohuo Ross alitaja sababu zinazochangia  tatizo la ajira
kuwa ni pamoja na wahitimu kutoka vyuo mbalimbali kukosa taarifa za fursa za ajira kwa wakati,baadhi ya vijana kutokuwa na uwezo wa kufanya kazi wanazoziomba..


Alitaja tatizo changamoto nyingine inayochangia tatizo hilo kuwa
utauzi wake kufwanyw akwa msingi wa kiasia na kuongeza kuwa serikali inawajibu wa kuwawesha vijana kiuchumi.

Kwa uapnde wake mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa Jesca Msambatavangu aliwataka vijana wanaohitimu elimu ya juu kutumia fursa zilizopo za ajira na kuondokana na ajira kutoka serikalini.

"Mimi ninawasihi vijanawetu wasominaomba muache kulalamikana
badalayake tumieni elimu mliyoipata kutumia fursa za ajiria ikiwamo kujiajiri ,hii ndiyo njia pekee ya kukabiliana na changamoto ya ajira"alisema Jesca.

Alisema kuwa wasomi wanapomalizavyuo wasi subiri kuajiriwa lakini watafute fursa ya ajira na wawe watu wenye uwezo wakuona mwanya wa biashara.

Kwa upande wake Athony Mongongwela ambaye ni mwanafunzi wa chuo hicho wa mwaka watatu alisema  serikali imekosa ubunifu wakutengenezea nafasi za ajira vijana.

Mongomwela alisema pamja na kuwa Tanzania inamiliki madini ya Tanzania inauza madini ya Tanzania katika soko la dunia kwa bei ya kutupwa huku jirani zetu kutoka Kenya wakinufaikana madini hayo kw akuuza kwa bei kubwa katika soko la dunia.

Aliitaka serikali kutengeneza mazingira yatakayoiwezesha Tanzania kuuza madini kwa bei kubw ana kunufaika na madini hayo ambayo ndiyo rasimali kubwa ya uchumi kwa anchi masikini.
.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM  mkoa wa Iringa, Jesca
Msambatavangu, ambaye amebobea katika masuala ya ujasiliamali aliwaasawasomi kuacha kulalamika na kutafuta  fursa za ajira.

Alisema kuwa wasomi wanapomalizavyuo wasi subiri kuajiriwa lakini watafute fursa ya ajira na wawe watu wenye uwezo wakuona mwanya wa biashara.habari ya picha

THE Deputy Vice Chancellor Academics (DVCA) of Ruaha Catholic
University (RUCU) Prof. G. Mpangala presenting his paper on the
constitution and building democracy during the symposium organized by
the student government of (RUCUSO) at the 53 years of independence of
Tanzania celebrations held at Benjamin William Mkapa Learning Resource
Centre on Tuesday in Iringa Region. (PHOTO: FRIDAY SIMBAYA)
Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA