Home » » DIWANI MCHILO AJISIFU KUMZIDI KUCHANGIA WAZIRI PINDI CHANA ,AMPA ONYO KALI KUWA AKITUMIA VIBAYA UWAZIRI WAKE KUTISHA WATENDAJI ATAONGOZA MAANDAMANO IKULU

DIWANI MCHILO AJISIFU KUMZIDI KUCHANGIA WAZIRI PINDI CHANA ,AMPA ONYO KALI KUWA AKITUMIA VIBAYA UWAZIRI WAKE KUTISHA WATENDAJI ATAONGOZA MAANDAMANO IKULU

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Friday, December 12, 2014 | 4:32 AMMh. Pindi  Chana
Diwani Monica Mchilo akiwa na viongozi wa  dini
Na matukiodaimablog
MCHANGO  wa  Tsh 15,000 uliotolewa na   naibu  waziri  wa maendeleo ya jamii jinsia na  watoto Pindi Chana (mb) kwa  ajili ya kuchangia shule ya msingi Ludewa  mjini iliyokumbwa na maafa  ya  vyumba  vyake  vitatu   kuezuliwa na  kimbunga Februari 28  mwaka  huu umezidi kuvuta hisia za  wengi   nje na ndani ya  wilaya ya  Ludewa kiasi  cha  kupelekea baada ya madiwani  wa CCM Ludewa kumuonya waziri  huyo kuacha kutafuta mchawi kwa mchango  aliochangia mwenyewe kwa  moyo mkunjufu.

Diwani  wa kata ya  Ludewa mjini Monica Mchilo akizungumza na  mwandishi  wa habari hizi mjini Ludewa jana  alisema  kuwa amesikitishwa na  hatua ya naibu  waziri  kuanza kuwatuhumu baadhi ya  viongozi  kuwa wanamchafua wakati suala   hilo ni  kweli  na  mbaya  zaidi  kuanza  kutoa vitisho kwa baadhi ya  walimu na watendaji wa serikali jambo  ambalo kama diwani  wa kata   hiyo iliyokumbwa na maafa  hayo hatakubali kunyamaza.

"Anachotaka  kukifanya   naibu  waziri Chana  ni kuwafanya  viongozi  mbali mbali  wa ngazi za chini  kufuta utamaduni wa  kuishukuru  serikali ,CCM na  viongozi mbali mbali wanachangia maendeleo .....hivi kuna  ubaya gani  kwa waziri  kupongezwa kwa  kuchangia maendeleo " alihoji  diwani   huyo.

Kuwa uongozi  wa  shule   hiyo na viongozi wa tarafa na kata walitoa  pongezi hizo  kwa nia  nzuri ya  kutambua  mchango  wake na  pia kama  sehemu ya kushawishi wadau  wengine  kuzidi  kuchangia maendeleo hivyo waziri  huyo kama mbunge wa  viti maalum mkoa wa Njombe na mkazi wa kata   hiyo ambayo shule  imepatwa na maafa alipaswa  kutambua na  kuzipokea  pongezi zake badala ya kugeuza pongezi kuwa ni uadui.

"Shule   hiyo ili majengo  yake  yaweze kujengwa  zaidi ya Tsh milioni 13  zilikuwa zikihitajika na yeye kama mbunge wa  viti maalum na  waziri ambae  pia  yupo pua na mdomo na  shule   hiyo kutokana na nyumba  yake  kuwa kama mita  100  hivi alionyesha  kuguswa  na taizo  hilo na kuchangia kiasi alichokuwa nacho na mimi kama diwani pia  nilichangia Tsh 20,000 huku  wananchi  wa kawaida  ilikuwa ni Tsh 3000 kila  mmoja na watumishi Tsh 5000 sasa katika mchango  huo ni  wazi alivuka lengo la kuchangia Tsh 5000 kwa  watumishi na Tsh 3000 kwa  watu wa kawaida japo  mimi kama  diwani kweli lazima nijivune  nilimfunika mbali kwa  kujikamua Tsh 20,000 huku mbunge  Filikunjombe alichangia  mifuko 50 ya  saruji kwa awamu ya kwanza na awamu  hii ya pili amejitolea  kujenga  majengo hayo kwa zaidi ya Tsh milioni 13 na leo  ujenzi unakaribia kwisha"

Diwani  huyo alisema  kuwa  kila mtu anatoa kulingana na uwezo   wake  hivyo si  wakati wa  waziri  huyo kuanza kutoa vitisho kwa mkuu  wa  shule   hiyo na viongozi  wengine kwa madai ya kuanikwa mchango  wake   huku akitambua  kuwa suala  hilo la mchango halikuwa ni  siri lilikuwa  wazi kwa  kila mmoja kuchangia na ndio  sababu kila fedha  iliyopatikana  ilitangazwa katika vyombo  vya habari.

Hata   hivyo alisema  kuwa  iwapo naibu  waziri  huyo atatumia nafasi yake ya  uwaziri kutisha walimu ama kuhamisha walimu na watumishi katika kata na wilaya   hiyo yeye kama  diwani  wa kata  ya  Ludewa mjini ataungana na wananchi wake kufanya maandamano hadi Ikulu kwa Rais Dr Jakaya Kikwete kufikisha malalamiko ya wananchi dhidi ya matumizi mabaya  ya uongozi kwa  waziri  wake.

"Nimepata  tetesi  kuwa ameanza kupiga  simu kwa mkuu  wa shule na  kwa afisa  elimu kutaka mwalimu mkuu wa shule ya msingi Ludewa mjini Agnes Mageza kushushwa cheo ama  kuhamishwa pia kumtisha mtendaji wa kata  anayehusika na  kukusanya  michango hiyo .....sasa nafuatilia kama  kweli anafanya  hivyo majibu  yake atayapata"

Mchango  wa waziri Chana  umeendelea  kuvuta hisisa za  wengi  huku  mwenyewe akionyesha  kukana  kuwa hakuchangia japo  ushahidi  wa kila mchangiaji upo  wazi .

Mbali ya  kukana  kuchangia ila pia waziri  huyo amekuwa akinukuliwa katika  vyombo  mbali mbali vya habari ikiwemo Radio Clouds Fm  kuwa anachafuliwa kisiasa na mbunge wa   jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe jambo  ambalo linahojiwa na  wengi  kuwa mbunge  wa jimbo kujitolea  kuchangia zaidi ya Tsh milioni 13  kujenga vyumba   hivyo  vya madarasa  ili  watoto  wasome  na  waziri kuchangia kulingana na uwezo  wake ni kumchafua kwani alitamani  kuona  watoto  hao wakikosa sehemu ya  kusomea.

Tayari  mbunge  wa Ludewa Bw Filikunjombe ametoa kauli  yake ya  kumtaka waziri Pindi kuacha kuingiza siasa katika shida  za  wananchi na  kuwa akiw kama mbunge ambae  amechaguliwa na wananchi  wa Ludewa kazi yake  kubwa ni  kuwatumikia katika raha  na  shida huku lengo lake  kuona wananchi wa Ludewa  wanafanana  na wale wa mijini kwa  kuwa na maendeleo bora.
Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA