Home » » SYDS KUWANUFAISHA WANAWAKE NA VIJANA ZAIDI YA 300 KUPITIA KILIMO PAWAGA

SYDS KUWANUFAISHA WANAWAKE NA VIJANA ZAIDI YA 300 KUPITIA KILIMO PAWAGA

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Thursday, November 27, 2014 | 5:47 AM


Mwakilishi wa ubalozi wa marekani David Feldmann akihutubia mamia ya wakazi wa vijiji vya tarafa ya Pawaga wakati sherehe ya kufunga mafunzo ya mradi wa kuwawezesha akina katika kilimo kupitia asasi ya mpango salama wa maendeleo ya vijana (SYDS) kwa ufadhili ya watu wa marekani.
Wasanii   wakionyesha  igizo jinsi  watakavyonufaika na asasi hiyo


Mwakilishi wa balozi wa Marekani David Feldmann wa  pili  kulia akifuatilia  burudani mbali mbali
Baadhi ya  viongozi  wakimsikiliza mwakilishi wa balozi wa Marekani nchini
Wanakikundi  wakiwa katika mkutano  huo wakimsikiliza mwakilishi  wa balozi
Baadhi ya  wana  kikundi  watakaonufaika na taasisi  hiyo
Wananchi  Pawaga  wakifuatilia  mkutano huo
Wanahabari  Iringa  wakimhoji  mwakilishi wa balozi  wa Marekani Nchini Bw David Feldmann
Msanii kutoka mjini Iringa  akionyesha  ujuzi wa kucheza na nyoka aina ya  chatu kwa kujaribu  kumumeza
Na Friday Simbaya wa matukiodaima.co.tz Iringa
Jumla ya vikundi 43 vya wajasiliamali ambao ni sawa
sawa na wanawake na vijana zaidi ya 300  wa tarafa ya Pawaga wilayani Iringa, mkoa wa Iringa wamenufaika na mafunzo ya kuwezesha akina mama katika kilimo kutoka SYDS.

Mafunzo hayo yaliendeshwa na asasi isiyo ya kiserikali ya mpango salama wa maendeleo ya vijana (SYDS) kwa ufadhili wa serikali ya marekani kupitia ubalozi wake nchini Tanzania.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati sherehe ya kufunga mradi huo wa mrejesho kwa vikundi, meneja mahusiano wa SYDS, Arnold Pangani alisema SYDS imejitoa  kuendeleza mapambano dhidi ya changamoto zinazowakabili wengi wa akina mama katika sekta kilimo nchini.
“SDYS kwa udhamini wa serikali ya Marekani kupitia ubalozi wake nchini Tanzania tunaungana kwa pamoja na wananchi wa Pawaga zaidi tukitambua ushiriki wa wanawake katika kilimo,” alisema Panagani.

Aidhi, wanavikundi walitoa shukrani ya dhati kwa SDYS kwa kuwapatia mwongozo bora ambao umewawezesha kupata uelewa juu ya elimu ya mpango biashara na uendashaji vikundi.

Walisema kuwa kuja kwa asasi ya SDYS kumeweza kuhamasika na kuunda vikundi ambavyo vitasaidia katika shughulu za kilimo.
Walisema kwa mafunzo hayo kama vijana wametambua umuhimu wao kama vijana ni nguvu kazi na wanatakiwa kushiriki  shughuli za maendeleo na kujifunza zaidi juu ya mpango salama kwa maendeleo ya vijana.
Kwa upande wake mwakilishi wa ubalozi wa marekani nchini Tanzania, David S. Feldmann alisema Tanzania itajengwa na watazania wenyewe na marekani itajengwa na wamarekani.
Alisema kuwa matatizo ya watanzania hayawezi kumalizwa na marekani isipokuwa katika uwezekaji ndiyo suluhisho matatizo yote.

Alisema ni jukumu kwa kila mwananchi kuhakikisha anashiriki kikamilifu katika kuinua na kukuza uchumi.

Alisema watanzania lazima walipe kodi kwa serikali iliwaweze kupatiwa huduma stahiki kutoa kwa serikali kama ilivyo marekani.

Alisema kuwa asilimia 90 ya serikali ya marekani inaendeshwa kwa mapato ya ndani kwa vile wananchi wengi wanalipa kodi kwa serikali bila kutegemea misaada ya nje.
Share this article :

+ comments + 1 comments

December 1, 2014 at 12:36 AM

inahamasisha sana pale unapoona vijana wa kitanzania wanapokua na ile hali ya uthubutu na kuweza kufanya jambo fulani, big up Syds

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA