Home » » CCM yapania ushindi uchaguzi wa serikali za mitaa

CCM yapania ushindi uchaguzi wa serikali za mitaa

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Tuesday, October 14, 2014 | 3:01 AMJoyce Kasiki, Dodoma

KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (NEC) Oganaizesheni, Mohamedi Seif Khatibu amesema ushindi wa CCM katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa ni kishiaria cha ushindi wa kura za maoni kwa Katiba inayopendekezwa.

Akizungumza  leo katika ufunguzi wa semina ya Makatibu wa Mikoa na Wilaya wa CCM  katika ukumbi wa White House mjini hapa  ,katibu huyo amesema ili Katiba inayopendekezwa iweze kupigiwa kura za ndiyo ,ushindo wa kishindo unahitajika katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaitarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu.

"Katika uchaguzi  wa sasa wa Serikali za Mitaa ushindi ni muhimu, kwanza tunajiandaa uchaguzi mkuu wa mwakani, pili tuna kura ya maoni ambayo itafanyika kabla ya uchaguzi mkuu,.

Amesema kushinda katika uchaguzi wa Serikali za mitaa itakuwa ni kiashiria kizuri kwa katiba inayopendekezwa kupigiwa kura  ya ndiyo lakini pia kujihakikishia ushindi katika uchaguzi Mkuu ujao wa Madiwani,wabunge na Rais.

"Tunaamini hakuna vita ambayo haviandaliwi, tumekutana kwa ajili ya vita vikubwa vya uchaguzi ulio mbele yetu," alisema

Amesema  Semina hiyo imeandaliwa kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa Desemba na kwamba kwa mujibu wa Katiba ya CCM inataka kila uchaguzi ambao chama chama hicho kitashiriki lazima kishinde

Khatib amesema pamoja na kuwepo kwa viongozi wengi wa chama hicho lakini makatibu wa CCM wa wilaya na mikoa ndio makamanda wakubwa katika kufanikisha chaguzi hizo.

Amesema matokeo ya matukio hayo matatu ndio maeneo ambayo makatibu hao watapimwa utendaji wao wa kazi  na kuwataka kila mmoja aanze kujipima mwenyewe.

"Kila mmoja  ajipime, kama umepoteza nafasi katika eneo lako maana yake hufai, tutapima uwezo wa  utendaji  wenu kutokana ushindi huu,tunajua CCM inao uzoeufu wa kushinda katika chaguzi ndogo kwa kuwa hushinda chaguzi hizo.

Akifungua semina hiyo, Naibu Katibu Mkuu wa CCM ZAnzibar,Vuai Ali Vuai aliwataka wana CCM wasiwe na hofu kwa upande wa Zanzibar wakati uchaguzi kwa kuwa chama hicho kipo imara visiwani humo.

Alisema CCM imeandaa semina hiyo kwa kuwa inaamini ushindi ni mipango siyo ubabe wala kuvunja sheria.


Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA