Home » » LEO NI KUMBUKUMBU YA KIFO CHA MWANAHABARI DAUDI MWANGOSI

LEO NI KUMBUKUMBU YA KIFO CHA MWANAHABARI DAUDI MWANGOSI

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Monday, September 1, 2014 | 9:38 PM


ILIKUWA ni majira  ya  saa 10 jioni ktk kijiji  cha Nyololo wilaya  ya Mufindi  tarehe  kama  ya leo tarehe  2/9/2012 alipopoteza  maisha  mwanahabari  wa  kituo  cha  Chanel Teni na  aliyekuwa  mwenyekiti  wa  chama  cha  waandishi  wa  habari  mkoa  wa  Iringa ( IPC) Daudi Mwangosi.

Wakati  tunakumbuka  siku  hii wanahabari Iringa tutaungana  kuadhimisha  siku  hii kwa  kufanya  sara  fupi ktk uwanja  wa IDYDC Mtwivila na  baada ya  hapo utafanyika  mchezo  wa  kirafiki  kama  kutambua mchango  wa  vyombo  vya habari mkoa  wa  Iringa  ila pia  kuenzi na kutambua  mchango  wake  katika michezo kama  njia ya  kudumisha mshikamano wetu  wanahabari  mkoa wa  Iringa .

Pia  kutakuwa na mazungumzo  mafupi  ya  kukumbushana tulikotoka na tunanakokwenda  katika utendaji kazi  yake  yatakayofanywa na mwenyekiti wa IPC Frank Leonard 
Pia  tutazindua  kikombe  cha upendo kwa  ajili  ya mshikamano  kwa  wanahabari mkoa  wa  Iringa  

Mungu  ailaze  roho  yake mahali pema peponi 
Amina
Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA