Home » » ZITTO KABWE AOMBWA POMERINI SEKONDARI

ZITTO KABWE AOMBWA POMERINI SEKONDARI

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Friday, August 29, 2014 | 3:48 AM

Mkuu  wa  shule ya  Sekondari Pomerin Bw  Shadrack Nyaulingo
Wanafunzi wa  kidato  cha nne  Pomerini wakijisomea
Mwalim  wa  taalum shuleni hapo
Mwanafunzi  wa  Pomerin wakijis
omea
Baadhi ya mabweni  ya  shule hiyo
wanafunzi  wakijiandaa kwenda katika  michezo
Na  Matukiodaima.co.tz
MWENYEKITI  wa kamati ya  bunge  hesabu  za serikali (PAC) Zitto Kabwe ameombwa kuwa  mgeni  rasmi  katika  jubilie  ya  miaka 25  ya  shule ya sekondari  Pomerin wilaya ya Kilolo mkoani  Iringa.

Akizungumza   leo   na  wanahabari mjini  Iringa mkuu  wa  shule  hiyo Shadrack Nyaulingo  alisema  kuwa wamemwandikia  barua  ya  kumwomba Kabwe  kuja kuwa mgeni rasmi katika  sherehe  hizo  za   shule  kutimiza miaka 25 toka  ilipoanzishwa na  kuwa  mbali ya  kuazimisha miaka  hiyo 25  pia  wataendesha  harambee  kwa  ajili ya  uboreshaji  wa  majengo ya  shule   hiyo ambayo  kwa  sehemu kubwa  yapo katika hali mbaya  zaidi.

" Tumemwandikia barua  ya  kumwomba  mheshimiwa  Zitto  kuja  kuwa mgeni rasmi kutoka na kingozi  huyo kuwa  ni mmoja kati ya wadau  wa maendeleo  katika mkoa  wa Iringa hasa  ukizingatia  kuwa alisoma katika  shule ya  sekondari ya  Tosamaganga iliyopo mkoani  Iringa..... hivyo  tumeona  tumwombe kuja  kusaidia  kuendesha harambee kama sehemu ya kutambua  mchango  wake  katika  Taifa "

Nyaulingo  alisema  kuwa  jumla ya  kiasi cha  Tsh milioni 61 zinahitajika  kwa  ajili ya ukarabati  wa majengo  hayo na  kuwa  mbali ya  kumwandikia  barua  Kabwe  ambae  ni mbunge  wa  jimbo la Kigoma Kaskazin  bado  wamesambaza  barua kwa  watu  mbali mbali  wakiwemo  wabunge wa CCM kama mbunge wa  jimbo la Ludewa  Deo Filikunjombe, mbunge wa  jimbo la Kilolo Prof Peter Msolla, mbunge wa  viti maalum  mkoa  wa Iringa Ritta Kabati pamoja na  makada na  watu mbali mbali kama Salim Asas, Frederick Mwakalebela  na wengine

Alisema  kuwa pia   wanafunzi  mbali mbali ambao  wamesoma katika  shule  hiyo  wamealikwa na kuombwa  kuchangia ukarabati  wa  shule  hiyo huku  akiwataka  wale  wote watakaohitaji  kusaidia  ukarabati  wa  shule  hiyo  kutuma  mchango  wao  kupitia akaunti ya  NBC 028103002306  na  CRDB ni  01J2070000100 ama M-pesa kwa namba 0768911120

Mkuu  huyo alisema shule  hiyo ambayo ilijengwa  miaka  50  iliyopita  na  wajerumani ilikuwa  ikitumika kama  shule ya  msingi kabla ya kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya  Iringa kuichukua na kuifanya sekondari  miaka  kwa miaka 25  sasa .

Hata  hivyo  alisema kuwa  mbali ya  kanisa  kufanya ukarabati  mkubwa  ila bado baadhi ya majengo   yana hali mbaya  kiasi  cha  kuhitaji  kufanyiwa  ukarabati  zaidi  hasa na  paa kutokana na sehemu  kubwa ya  majengo  paa zake  kuwa katika hali ya uchakavu mkubwa .

Akielezea  kuhusu ubora wa  elimu  shuleni  hapo  alisema  kuwa  kati ya  shule  bora katika mkoa wa Iringa na Tanzania  ni pamoja na Pamoreni  kutokana na rekodi  nzuri iliyopo kwa  kuendelea  kushika nafasi ya shule  20 bora  katika matokeo ya kidato cha  sita na  shule ya pili kimkoa kwa  kufanya  vema katika matokeo  hayo ya kidato  cha  sita .

Alisema  kuwa jubilei  hiyo  ya  miaka 25 ya  shule  hiyo itafanyika  Octoba 25  mwaka  huu na hivyo  kuwaomba  wanafunzi wote  waliosoma katika  shule  hiyo na  wafanyakazi  waliopata  kufanya kazi kushiriki  katika sherehe  hizo  ili  kujumuika na mgeni rasmi na wadau  wa maendeleo  mkoani hapa katika harambee  hiyo.
Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA