Home » » ZIMEBAKI SIKU MBILI KUFANYIKA KUMBUKUMBU YA KIFO CHA ALIYEKUWA WAZIRI WA FEDHA DR WILIAM A. MGIMWA .....

ZIMEBAKI SIKU MBILI KUFANYIKA KUMBUKUMBU YA KIFO CHA ALIYEKUWA WAZIRI WA FEDHA DR WILIAM A. MGIMWA .....

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Tuesday, August 12, 2014 | 4:03 AMRais Jakaya Mrisho Kikwete akimfariji Godfrey Mgimwa, mmoja wa watoto wa Marehemu wakati wa mazishi ya aliyekuwa Waziri wa Fedha na Mbunge wa Kalenga 
Dr Mgimwa  akikagua  maendeleo ya  shule ya Msingi kibaoni kata ya Ifunda  enzi  za uhai  wake


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na mkewe Mama Zakia Bilal, wakiifariji familia ya marehemu Dkt. William Mgimwa 
Rais  Dr  Jakaya  Kikwete kulia  akisalimiana na waziri  Dr Mgimwa  enzi  za uhai wake  katika  uwanja  wa ndege Nduli  Iringa 
Rais  Kikwete na mkewe  wakitoa heshima za mwisho katika kaburi ya Dr Mgimwa 
MBUNGE wa  jimbo la Kalenga Dr  Wiliam Mgimwa akiandika hundi ya Tsh  milioni 2 kwa ajili ya kuchangia   ujenzi  wa shule ya  sekondari Lyandembela mwaka  juzi 
...................................................................
Familia ya  mheshimiwa Godfrey  Mgimwa  mbunge wa jimbo la Kalenga  inapenda  kuwashukuru  wakazi  wa  jimbo la Kalenga  mkoani Iringa na watanzania  wote  waliopo nchini na  wale waliopo nje ya nchi kwa ushiriki  wao  mkubwa katika kuuguza na hadi mazishi ya  marehemu  babake  mpendwa  aliyekuwa waziri wa fedha Dr Wiliam A. Mgimwa  ambae pia alikuwa  mbunge wa jimbo la kalenga na  waziri wa  fedha .

Familia inapenda  kutoa shukrani nyingi kwa  wote  na ilipendeza kutoa mkono wa  shukrani kwa  kila mmoja ila tunaomba  kwa  salam hizi  pia iwe  sehemu ya  kushikana mkono .

Hata  hivyo familia inapenda kuwaalika  wote kwa  umoja  wetu nyumbani kwa marehemu  kijiji  cha Magunga kwa ajili ya misa ya  kumaliza msiba  ,misa  itakayofanyika Agosti 14 mwaka huu hivyo  tunawaomba  wananchi  wa Kalenga na wale  waliopo nje ya Kalenga  kufika  kuungana katika kuhitimisha 40 ya mpendwa  wetu .

Ifahamike  wazi kuwa  familia na  watanzania kwa ujumla tulimpenda  sana baba yetu na  kiongozi wetu ila Mungu alimpenda  zaidi  yetu 
Hivyo hatuna budi  kusema  jina lake Bwana na  lihimidiwe milele yote
Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA