Home » » YAW BERKO ASAINI MWAKA MMOJA LIBERTY PROF

YAW BERKO ASAINI MWAKA MMOJA LIBERTY PROF

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Tuesday, August 12, 2014 | 8:25 AM

Berko ameiambia BIN ZUBEIRY kwa simu jana kwamba amesaini Mkataba wa mwaka mmoja na Liberty baada ya kumaliza Mkataba wake wa miezi sita Simba SC.
Berko alisajiliwa Desemba mwaka jana Simba SC kama mchezaji huru baada ya kutemwa na Yanga SC msimu wa 2012/2013, hata hivyo akadaka mechi tano tu na kufungwa mabao sita kutokana na kuzidiwa kete na Ivo Mapunda, aliyekuwa kipa namba moja.
Yaw Berko amerejea Liberty Proffessionals ya Ghana

Alidaka Simba SC ikishinda 3-1 dhidi ya KMKM mchezo wa kirafiki, Dar es Salaam akafungwa bao moja, akadaka Simba SC ikishinda 1-0 na KMKM tena, akadaka Simba SC ikifungwa 1-0 na Mtibwa Sugar mchezo wa kirafiki, akafungwa moja, akadaka Simba SC ikitoka sare ya 1-1 na Mbeya City mchezo wa Ligi Kuu mjini Mbeya akafungwa moja kabla ya kudaka Simba SC ikifungwa 3-2 na JKT Ruvu Ligi Kuu akafungwa zote tatu.

Simba SC haikumuongezea mkataba mwishoni mwa msimu na sasa amerejea timu iliyomlea kisoka, Liberty.

Berko alianzia soka Liberty Professionals FC na mwaka 2005 alikwenda kucheza kwa mkopo Pisico Binh Dịnh FC ya Vietnam kabla ya kurejea Ghana baada ya mwaka mmoja. Alijiunga na Yanga SC Desemba mwaka 2009 na kucheza hadi 2013
Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA