Home » » Waziri Mkuu wa kwanza Mwislamu

Waziri Mkuu wa kwanza Mwislamu

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Sunday, August 10, 2014 | 11:57 PM


Rais Catherine Samba – Panza amemteua Mahamat Kamoun kuwa Waziri Mkuu mpya wa serikali ya mpito ya Jamhuri ya Afrika ya Kati. Msemaji wa Rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati amesema kuwa, kabla ya kuteuliwa kuwa Waziri Mkuu, Mahamat Kamoun alikuwa mshauri maalumu wa Rais Catherine Samba – Panza.
Mahamat Kamoun pia aliwahi kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Hazina kuanzia mwaka 2003 hadi 2013 wakati wa uongozi wa Rais Francois Bozize aliyeondolewa madarakani mwezi Machi mwaka jana.

Rais Samba –Panza amemteua Kamoun kuwa Waziri Mkuu mpya wa serikali ya mpito, zikliwa zimepita wiki mbili tokea yafikiwe makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya wanamgambo wa Muungano wa Seleka na kundi la Kikisto la Anti Balaka huko Brazzaville, Jamhuri ya Kongo.

 Imeelezwa kuwa, miongoni mwa changamoto kubwa itakayoikabili serikali ya Bangui ni jinsi ya kuyashirikisha makundi ya wanamgambo wanaobeba silaha kwenye serikali mpya nchini humo.

Mahamat Kamoun anakuwa Muislamu wa kwanza kuhudumu wadhifa wa uwaziri mkuu katika Jamhuri ya Afrika ya Kati, tokea nchi hiyo ilipojipatia uhuru kutoka kwa mkoloni Mfaransa mwaka 1960.   
Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA