Home » » WAZIRI MGIMWA ANOGESHA UZINDUZI WA ALBAMU KWAYA YA SESILIA

WAZIRI MGIMWA ANOGESHA UZINDUZI WA ALBAMU KWAYA YA SESILIA

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Tuesday, August 12, 2014 | 5:26 AM

IMG-20140812-WA0028_54e5e.png
IMG-20140812-WA0029_dbd20.png
Naibu waziri wa Maliasili na Utalii Mahamoud Mgimwa akizindua kanda hiyo
IMG-20140812-WA0035_1efcd.png
IMG-20140812-WA0033_19980.png
Paroko wa Parokia ya Mdabulo akihesabu fedha hizo baada ya kukabidhiwa.

Sherehe za Uzinduzi wa Albamu ya Kwaya ya Mtakatifu Sesilia Parokia ya mdabulo umefanyika katika kata ya Mdabulo, Tarafa ya Ifwagi, jimbo la Mufindi kaskazini.
Albamu hiyo inayojulikana kwa jina moja la Nauli ya Mbinguni ina jumla ya nyimbo 11 zenye ujumbe mbalimbali wa kuwajenga wananchi kimwili na kiroho.
Katika sherehe hizo mgeni rasmi aliyezindua kanda hiyo alikuwa ni Naibu waziri wa Maliasili na Utalii Mahamoud Mgimwa kwa kuwachangia jumla ya shilingi 2,000,000/=.
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Mufindi Evarista Kalalu amewatia moyo kwa kuchangia jumla ya shilingi 200,000, ambapo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi Paul Mtinika naye amechangia shilingi 200,000.
Naye Mwenyekiti wa Halmashuri ya Wilaya ya Mufindi Peter Pesanane Tweve amechangia shilingi 50,000 wakati Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Taifa ccm Maliselina Mkini amechangia 230,000, Katibu Uchumi wa CCM Wilaya ya Mufindi Practus Mgimwa amechangia shilingi 300,000 huku mdau Samwel Masasi akichangia shilingi 300,000 sambamba na Diwani wa Kata ya Mdabulo Elinei Nyeho aliyechangia shilingi 100,000.
Zoezi hilo lilimalizika kwa wajumbe mbalimbali kuichangia Kwaya ya Mtakatifu Sesilia kwa kuuza albamu hiyo ambapo fedha zilizopatikana ahadi ikiwa ni shilingi 850,000, Keshi ikiwa ni 4,374,000 ambapo jumla ya fedha zote zilizopatikana ni shilingi 5,224,000.
Mgimwa ambaye ndiye aliyeendesha harambee hiyo ya kuichangia kwaya hiyo amewataka wana kwaya hao kuendelea kutenda matendo yaliyo mema ili kujenga mahusiano mazuri baina ya waumini wa kanisa hilo na mungu.
Aliongeza kwa kuwashukuru wakazi wa Mdabulo kwa heshima kubwa waliyompatia ya kuwatumikia akiwa mbunge, kupitia uchaguzi mkuu uliofanyika mwaka 2010 kwa kumpa dhamana kubwa ya kuliongoza Jimbo la Mufindi Kaskazini kwani uaminifu huo ulichangia kuaminiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete kwa kumteua kuwa Naibu wa Maliasili na Utalii.
Alienda mbali zaidi kwa kuwapongeza wananchi waliojitokeza katika sherehe hizo jinsi ambavyo wamekuwa wakijitoa katika shughuli za maendeleo ili kuhakikisha Jimbo la Mufindi Kaskazini linasonga mbele katika kupambana na vita dhidi ya Umasikini.
Aidha alimshukuru Paroko wa Parokia ya Mdabulo pamoja na msaidizi wake Paroko Kihwelo kwa jinsi ambavyo wanajitoa kusaidia baadhi ya shughuli mbalimbali hususani katika sekta ya Afya, Elimu na Maji katika Kijiji hicho.
Mgimwa aliwaaahidi wananchi wa Mdabulo kuwa baada ya wiki mbili umeme utapatikana katika Kata ya Mdabulo hivyo wananchi wajiandae kwa ajili ya kutumia umeme huo kwa ajili ya kufanya shughuli mbalimbali za kuwaongezea kipato kwani fursa itakuwa imepatikana.
Naye Paroko wa Parokia ya Mdabulo Baptist Duma, amempongeza Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii kwa kuwa karibu na waananchi wa Jimbo hilo kwa kushauriana akiwa kwenye ziara zake kwa kufanya mikutano na hatimaye baada ya kumaliza mkutano kwenda kulala Parokiani hapo.
Sambamba na hayo Mgimwa ameichangia Kwaya ya Sesilia jumla ya shilingi 1,700,000 kwa ajili ya kusaidia mradi ya kunua mashine za kupasulia mbao.
Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA