Home » » WAANDISHI wa habari mkoani Dodoma wametakiwa kuzipigia debe ibara za 30na 31 ili zipite kwa sababu zina walenga wao moja kwa moja

WAANDISHI wa habari mkoani Dodoma wametakiwa kuzipigia debe ibara za 30na 31 ili zipite kwa sababu zina walenga wao moja kwa moja

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Monday, August 11, 2014 | 5:58 AM

Akizungumza katika mdahari ya wadau wa habari na waandishi wa habari mkoani humo, Jemas Marenga kutoka taasisi inatoa huduma za kisheria kwa wananchi Nola alisema kuwa waandishi wa habari wanatakiwa kuimba kuhusiana na ibara hizo ili zipete.
 Alisema kuwa waandishi wamekuwa wakilia kutetea watu wengine na kupigania haki za wengine wakati wao wakiwa na midomo mizito kutetea masuala yanayo wahusu wao.

"Waandishi inatakiwa tulie kwa sautu kupigania kuwa hizi ibara mbili zinakuwemo katika katiba, kwani hizi ndizo zitatupa Uhuru wa kweli katika utendaji wa kazi zetu," alisema Marenga.

Alisema kuwa ibara hizi zikiwemo katika Katiba ya nchi waandishi watakuwa huru na kufanya kazi bila kuzuiliwa kwani zinaweza uhuru kwa kujieleza na kutoa maoni pasipo kuwa na kukwazo.

 Aliongeza kuwa ibara hizo zikiwepo zitaweka utaratibu wa waandishi wa habari kutambulika kisheria na kusajiliwa kama ilivyo kwa wanataaruma ya Sheria kwa mawakili na kupewa uhuru wa kufanya kazi bila ya kuvunja sheria. "Ibara hii itatamua fani hii ya uandishi wa habari na waandishi kufanya kazi kwa kibali atakaye kiuka atakuwa anafutiwa kibari cha kufanya kazi zake kwa mujibu wa sheria kwani kutakuwa na chombo kinacho simania wanataaluma na bodi ndiyo itakuwa ikijua mwandishi fulani anapatikana wapi," Alisema Marenga.

 Alisema kuwa waandishi wakiwa wamesajiliwa na kuwa na kubali itakuw araishi kumjua mtu anapatikana wapi na anafanya kazi kwa uadilifu ama la na itakuwa rahisi kumbana mtu anapo enda kinyume na maadili ya uandishi wa habari. Alisema kuwa pia ndani ya ibara hii vyombo vya habari vitakuwa vikibanwa kuhusiana na maandili na maudhui ya picha zinazo tumika katika vyombo hivyo.

 Mwisho.
Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA