Home » » MIROSLAV KLOSE ASTAAFU UJERUMANI BAADA YA REKODI YA KUTISHA YA MABAO HADI KOMBE LA DUNIA

MIROSLAV KLOSE ASTAAFU UJERUMANI BAADA YA REKODI YA KUTISHA YA MABAO HADI KOMBE LA DUNIA

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Monday, August 11, 2014 | 6:11 AMMFUNGAJI bora wa kihistoria wa Ujerumani, Miroslav Klose, ametangaza kustaafu soka ya kimataifa.
Kiasi kama cha mwezi mmoja tangu ashjinde Kombe la Dunia na nchi yake nchini Brazil, mkongwe huyo mwenye umri wa miaka 36 ameamua kupumzika timu ya taifa.
Amefikisha jumla ya mabao 16 aliyofunga katika Kombe la Dunia na jumla ameifungia mabao 71 timu yake ya taifa. Huyo ndiye pia mfungaji wa mabao mengi zaidi katika Fainali za Kombe la Dunia, akifuatiwa na Mbrazil Ronaldo Lima mwenye mabao 15. 
Mchezo umekwisha: Miroslav Klose ametangaza kustaafu soka ya kimataifa baada ya kuifungia Ujerumani mabao 71

REKODI YA MABAO YA KLOSE KOMBE LA DUNIA

1, 2, 3: Ujerumani 8-0 Saudi Arabia, makundi, 2002
4: Ujerumani 1-1 Jamhuri ya Ireland, makundi, 2002
5: Cameroon 0-2 Ujerumani, makundi, 2002
6, 7: Ujerumani 4-2 Costa Rica, makundi, 2006
8, 9: Ecuador 0-3 Ujerumani, makundi, 2006
10: Ujerumani 1-1 Argentina (baada ya dakika 120, penalti 4-2), Robo Fainali, 2002
11: Ujerumani 4-0 Australia, makundi, 2010
12: Ujerumani 4-1 England, 16 Bora, 2010
13, 14: Argentina 0-4 Ujerumani, Robo Fainali, 2010
15: Ujerumani 2-2 Ghana, makundi, 2014
16: Brazil 1-7 Ujerumani, Nusu Fainali, 2014
Perfect ending: Klose scored twice as 
Germany lifted the World Cup in Brazil this summer
Klose alifunga mabao mawili Ujerumani ikitwaa Kombe la Dunia nchini Brazil mwaka huu
Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA