Home » » MAJI MACHAFU YAWA KERO KUBWA KWA WAFANYABIASHARA WA MASHINE TATU

MAJI MACHAFU YAWA KERO KUBWA KWA WAFANYABIASHARA WA MASHINE TATU

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Wednesday, August 13, 2014 | 3:45 AM


Wafabiashara wanaofanya biashara eneo la mashine tatu lililopo mkoani Iringa wameiomba Serikali iwatafutie wafabiashara wa samaki wabichi eneo ambalo watakuwa wanafanyia biashara zao. Hayo yalisemwa na baadhi ya wafanyabiashara wa eneo hilo walipokuwa wakizungumza na mtandao huu wa www.matukiodaima.com kuhusiana na maji machafu yanayomwagwa na watu wanaofanya biashara za samaki wabichi eneo hilo na kusababisha harufu kuwa mbaya pamoja na eneo hilo kuonekana kutokuwa katika hali ya usafi.
 “hali ya maeneo hapa ni machafu sana, asubuhi kuna watu wanauza samaki na wanamwaga maji machafu hapo kwahiyo yanakaa sana mpaka yanatoa harufu kama hiyo mnayoisikia, tushamuita kiongozi wetu wa daladala na tushamueleza na akasema atalishughulikia, hivyo tunaiomba Serikali iwatafutie eneo hawa wauza samaki ili wakafanyie biashara zao mbali na hapa maana hapa wanatuhalibia mazingira” alisema Bwana Emmanuel Stephano Dereva wa daladala maeneo ya mashine tatu. Hata hivyo wafanyabiashara hao walisema walishatoa taarifa mara kibao kwa watu wanaohusika na afya lakini cha kushangaza wakija pale kuangalia maeneo hayo hawachukui hatua yeyote ile kwa watu hao wanaochafua mazingira maeneo hayo.
 “Taarifa tulishapeleka kwa mabwana afya na wamekuja kama wanne ila wanapewa vitoweo vya samaki na wanaondoka bila kuwafanya chochote, kwa hiyo unakuta hili zoezi haliezi kukomeshwa kwa sasa pili kuna baadhi ya watu wanakojoa kwenye mitaro ikifika mida ya usiku sasa ukichanganya na hayo maji ya samaki basi harufu ndo inazidi kabisa, sababu za watu kukojoa hakuna vyoo kwa hapa stendi ya mabasi ya mashine tatu mda mwingine tunakuta hadi haja kubwa”.
 Alisema Bwana Chagu Chaly mfanyabiashara wa maeneo hayo ya mashine tatu. Pia bwana Chaaly alisema inaonyesha Mkurugenzi wa Manispaa anawatuma mabwana afya waje waangalie tatizo linalowakabili wafanyabiashara hao ila wakifika wanatulizwa na vitoweo vya samaki na kisha wanaondoka bila kutekeleza walichoagizwa na Mkurugenzi. 
NA DIANA BISANGAO WA MATUKIO DAIMA.COM, IRINGA
Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA