Home » » KMKM CHUPUCHUPU KWA ADAMMA KAGAME, YACHOMOA DAKIKA YA MWISHO

KMKM CHUPUCHUPU KWA ADAMMA KAGAME, YACHOMOA DAKIKA YA MWISHO

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Tuesday, August 12, 2014 | 8:23 AM

BAO la Juma Mbwana Fakhi dakika ya 90 na ushei, limeinusuru KMKM kuzama mbele ya Adamma, baada ya kulazimisha sare ya 1-1 katika mchezo wa Kundi A, Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame Uwanja wa Nyamirambo, Kigali, Rwanda.

KMKM baada ya kusawazisha bao leo Nyamirambo

Adamma ya Ethiopia ilitangulia kupata kipindi cha pili mfungaji Wonooson Milkesa kabla ya KMKM ya Zanzibar kukomboa dakika za majeruhi.

Hiyo ni sare ya pili kwa KMKM baada ya awali kutoka 1-1 pia Atlabara uya Sudan Kusini kabla ya kufungwa 4-0 na Azam FC, wakati Adamma katika mchezo wake wa kwanza ilifungwa 2-1 na Rayon.
Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA