Home » » Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Naima Mrisho, alisema kuwa elimu hiyo imetolewa kwa wenyeviti wa kamati hiyo ambao ni wakuu wa mikoa wamepatiwa elimu hiyo ili kuwafikishia wananchi.

Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Naima Mrisho, alisema kuwa elimu hiyo imetolewa kwa wenyeviti wa kamati hiyo ambao ni wakuu wa mikoa wamepatiwa elimu hiyo ili kuwafikishia wananchi.

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Monday, August 11, 2014 | 5:55 AM
MIKOA 17 ya Tanzania imepatiwa elimu juu ya kupambana na maafa ikiwa ni mikakati ya tume ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu kwa lengo la kuelimisha jamii kujihami na maafa ya nguvu za asili kwa kupunguza madhara. Elimu hiyo imekuwa ikitolewa kwa kamati za maafa za mikoa hiyo kwa lengo la kuwafikishia elimu hiyo wananchi kwa ngazi ya Mkoa, wilaya, kata, hadi kijiji na kupunguza madhara yatokanayo mafuriko na ukame na majanga mengine ya asili.


 Akizungumza NIPASHE Mjini hapa hivi karibuni, Mratibu wa Mafunzo na  Alisema kuwa wananchi wanatakiwa kufahamu mambo ya kufanya wakati yanapotokea maafa ili kupunguza ukali wa madhara kwao.


Alisema kuwa wananchi katika ngazi ya kijiji wanatakiwa kupatiwa elimu juu ya kujikinga na maafa ili yanapo tokea wajikinge na kujiokoa dhidi ya madhara hayo. Naima alisema kuwa wananchi wanatakiwa kuizingatia elimu hiyo na matangazo yanapotolewa juu ya kutokea kwa jaga lolote ama kama kutanokea ukame, wananchi wanatakiwa kujikinga kwa kutouza chakula alicho nacho na kupanda mazao yanayo kubali mvua chache.


 Aidha kumekuwa na sheria inayosimamia maafa ambayo ni ya mwaka 1990 sheria namba 9 sasa inafanyiwa marekebisho ili kuongeza vifungu vitakavyo wabana watu ambao wapo katika maeneo ambayo wanaweza kupata mafuriko na kuwaondoa kwa mujibu wa sheria hiyo itakavyo rekebishwa.


 Aliongeza kuwa wakuu wa mikoa ambao ndio wenyeviti wa kamati hizo wanatakiwa kuzifikisha elimu kwa wananchi vijijini ili kila mwananchi waelewe kuhusiana na kujikinga na maafa yanapotokea. Alisema kuwa Idara hiyo inashirikiana na sekta zingine ambazo hufanya kazi kwa pamoja pindi yanapo tokea maafa, ambazo ni Afya na Zimamoto ambao hufanya kazi kwa pamoja mara yanapotokea maafa.


 Naima alisema kuwa Tume hiyo imekuwa ikijihusisha na kupima madhara ya maafa na kutoa tathimini ya madhara ya maafa hayo na kuchukua hatua za kufanya uokozi na kutoa dawa kwa waathirika wa maafa pamoja na chakula kutoga ghara la taifa la chakula.

                                   Mwisho
Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA