Home » » HAKUNA DINI YA KWELI INAYOCHOCHEA MAUAJI

HAKUNA DINI YA KWELI INAYOCHOCHEA MAUAJI

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Monday, August 11, 2014 | 6:02 AM


MJUMBE wa Baraza la Uendeshaji la UNESCO linalosimamia ukuzaji wa utamaduni, Dk. Mary Mbiro Khimulu amesema machafuko na mauaji hayana uhusiano wowote na dini ambayo ni ya kweli.

 Ametoa kauli hiyo leo mchana (Jumatatu, Agosti 11, 2014) wakati akishiriki mjadala wa jinsi ambavyo bara la Afrika linakabiliana na migogoro inayotokea barani humo kwenye mkutano wa Dunia unaojadili masuala ya Amani, Usalama na Maendeleo jijini Seoul, Korea Kusini.
 

Dk. Khimulu ambaye ni raia wa Kenya, alisema: "Dini ya kweli haiwezi kuruhusu umwagaji wa damu, hakuna dini ya kweli inayochochea mauaji wala kuruhusu mapigano. Ninawasihi wote mliopo hapa, msiruhusu dini zenu zitumike kufanya mambo mabaya.


" Dk. Khimulu alisema ili kuepuka migogoro ya dini, anashauri diplomasia ya utamaduni (cultural diplomacy) itumike kuleta amani, usalama na maendeleo barani Afrika. "Kwa kuitumia diplomasia ya utamaduni, tuangalie ni kwa njia gani mijumuiko ya pamoja ya kidini (inter-faith communities) inaweza kutumika kuleta amani, upendo na mshikamano kwenye jamii tunazoishi," alisema. Vilevile, Dk. Khimulu alisema kwa kutumia diplomasia ya utamaduni tunaweza kuvunja chuki na kuleta mshikamano na umoja miongoni mwa watu wetu, watu wakatembeleana kupitia michezo, nyimbo au matamasha, na wakajenga mahusiano ya kuheshimiana kidugu.


Alisema kwa kuwa vita huanzia akilini mwa mwanadamu, ni humo humo ambamo mawazo ya kuacha mapigano ama machafuko yanapaswa kuingizwa. "Kwa hiyo tuitumie diplomasia ya utamaduni kama njia pekee ya kujenga mahusiano ya karibu kwenye jamii zetu na itusaidie kufikia malengo yetu ya kupata amani na usalama kwa watu wetu,"aliongeza. 


Mapema, Balozi wa Kudumu wa AU kwenye Umoja wa Mataifa, Balozi Antonio Tete alisema wakati Umoja wa Afrika unaanzishwa mwaka 1963, baadhi ya wakuu wa nchi walikuwa na ndoto ya kuwa na jeshi moja barani Afrika ambalo lingekuwa na kazi ya kukabili migogoro yote barani humo. "Kutokana na mabadiliko ya wakati na kadri muda ulivyosonga mbele, matarajio yao hayakutumia. Viliundwa vikosi vya muda navyo havikudumu.
Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA