Home » » COASTAL UNION YAKANUSHA FIKIRINI SULEIMANI KUSAJILIWA NA AFRICAN SPORTS

COASTAL UNION YAKANUSHA FIKIRINI SULEIMANI KUSAJILIWA NA AFRICAN SPORTS

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Sunday, August 17, 2014 | 9:57 AM

UONGOZI wa Klabu ya Coastal Union “Wagosi Kaya “umekanusha vikali taarifa zilizizoenezwa kuwa mlinda mlando wa kikosi cha Vijana wenye umri chini ya miaka ishirikini U-20 Fikirini Suleimani “Mapara kuwa amesajiliwa na Klabu ya African Sports “Wanakimanumanu”
Taarrifa hizo hazina ukweli wowote bali Fikirini bado ni mchezaji halali wa Klabu ya Coastal Union ya Tanga na ni miongoni mwa wachezaji watakaoonekana kwenye kikosi hicho msimu ujao.

Taarifa iliyotolewa leo kwa nyombo vya Habari kupitia msemaji wa Klabu hiyo Oscar Assenga zimeelezwa kuwa fikirini bado ana ni mchezaji halali wa timu hiyo kwa kusajiliwa hivyo tarifa ya kuwa amejiunga na Africa Sports hazina ukweli wowote ule.
 Assenga amesema kuwa ili wadau wa soka waweze kuthibitisha kuwa mchezaji huyo bado yupo kwenye kikosi cha wagosi hao wa kaya wafike mazoezini Jumatatu kwani atakuwepo kwenye mazoezi hayo.
Amesema kuwa Fikirini ni miongoni mwa wachezaji waliosajiliwa kwa ajili ya kuitumikia timu hiyo msimu ujao wa Ligi kuu soka Tanzania bara.
Mwisho.
na fredy mgunda
Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA