Home » » Chadema wazidi kuumbuana hadharani kwa matendo yao mbaya na yasiyo faa kwa jamii.

Chadema wazidi kuumbuana hadharani kwa matendo yao mbaya na yasiyo faa kwa jamii.

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Friday, August 15, 2014 | 3:13 AMChama cha Demokrasia na Maendeleo kimezidi kuumbuana kwa yale matendo yao yasiyofaa kwa jamii ya Kitanzania.
Ni muda sasa tangia chama hicho kuhusishwa waziwazi na vitendo vya kigaidi wakijaribu kutengeneza huruma ya watu kwa kuwaumiza na kuwaua raia wasio na hatia.


Leo katika mkutano wake na waandishi wa habari Habibu Mchange asema yote kuhusu Chadema na ukatili wao wa kutisha.
TAARIFA YA NDUGU HABIBU MCHANGE KUHUSU KUHUSISHWA NA KUSHIRIKIANA NA VIONGOZI WENGINE ILI KULIPUA HELKOPTA YA SLAA NA MNYIKA ILIYOTOLEWA NA CHADEMA NA MASWALA MENGINE
TAREHE.14.08.2014.
 UTANGULIZI.
Ndugu wanaHabari,
Mtakumbuka kwamba Tarehe 9.08.2014, katika vyombo mbali mbali vya habari  na mitandao ya kijamii imeripotiwa Taarifa ya TUNDU LISSU na waliokuwa MADIWANI wa shinyanga mjini baadae wakahamia CCM, pamoja na Tuhuma nyingine  kwamba kuliwahi upangwa mpango wa KUILIPUA HELKOPTA iliyowabeba WILBROD  SLAA na JOHN MNYIKA ili wafe,
Na wanasema miongoni mwa waliohusika kufanya mkakati huo ni Ndugu HABIBU MCHANGE, ambaye ni Mimi.
Japo kuwa hii si habari ya kwanza ya kipuuzi inayotolewa na viongozi wa CHADEMA ikinihusisha mimi ama moja kwa moja au la, tangu baada ya mgogoro wangu wa kisiasa ndani ya CHADEMA may 2011.
Na habari nyingi kati ya hizo nimeamua kuzipuuzia, leo ninaomba kusema kidogo ili kuweka kumbukumbu sawa na sahihi.
KUHUSU KUILIPUA HELKOPTA.
Pamoja na kwamba hekaya hii ni ya kipuuzi,
Haingii akilini hata kidogo kwamba mimi Habibu Mchange Nimepanga na CCM na naibu waziri kuilipua helkopta ambayo ingewabeba Slaa na Mnyika.
Upuuzi huu ulioratibiwa na Tundu Lissu, ni uthibitisho wa kushindwa na kuporomoka kisiasa kwa kasi ya ajabu kunakoikabili CHADEMA kwa sasa, na kujiokoa kwenye hilo wanaanza sasa kutengeneza tuhuma za kitoto namna hii zisizokuwa na kichwa wala miguu ili kupata huruma ya wananchi.
Ninawezaje kupanga mikakati ya kulipua helkopta, ili iwe nini?
Kwangu mimi kwa sasa Slaa ni miongoni mwa wanansiasa dhaifu waliowahi kutokea kwenye ulimwengu wa siasa za Tanzania.
Slaa ameshajiishia, nimlipue ili iwe nini?
Mtu aliyeishiwa ushawishi kama yeye, kiasi cha kushindwa kumshawishi hata mke wake aliyemzalia watoto wawili, anawezaje kuwa Tishio na kupangiwa mikakati ya kulipuliwa?
Nasema siwezi kufanya ujinga wa namna hii na hata kama angekuwa tishio kisiasa, si hurka yangu kujihusisha na matukio ya KIGAIDI namna hii.
CHADEMA NA MAUAJI / UJANGILI
SLAA, LISSU, MBOWE, MNYIKA, LEMA na CHADEMA ndio mabingwa wa matukio ya KIGAIDI na utoaji roho za wenzao, hasa pale wanapokuwa wametofautiana misimamo na mitazamo ndani ama nje ya Chama. Tafadhali wasitafute mtu wa kushiriki naye dhambi za mauaji waliyoyatenda na wanayoendelea kutenda.
Dunia Nzima inajua kwamba watu hawa wameshiriki kikamilifu kumuondoa DUNIANI aliyekuwa makamu mwenyekiti wa chama CHACHA ZAKAYO WANGWE, Hii haina ubishi kwamba, MBOWE, SLAA na MNYIKA walijaribu mara kadhaa kutaka kumuua CHACHA WANGWE kwa kutumia sumu na kushindwa mpaka walipofanikiwa kumuua kwa ajali ya kutengeneza tarehe 28.7.2008 wakimtumia kijana ambaye Dunia nzima inamjua.
Na Mungu anawaumbua, sasa wanahaha, leo nitaongeza ushahidi kwenye mauaji ya haya.
Angalia Mfano huu.
Tarehe 28.05.2008, JOHN MNYIKA, akiwa mkurugenzi wa vijana CHADEMA taifa kipindi hicho, alitukutanisha mimi Habibu Mchange, Marehemu Regia Mtema, Deus Mallya na vijana wengine wawili, ofisini kwake ambapo kwa sasa ofisi hiyo inatumika kama ofisi ya Naibu katibu mkuu, pamoja na mambo mengine tukajadiliana namna ya kulieneza Baraza la Vijana na kuongeza wanachama wengi vijana, na tukapeana majukumu, kwamba mimi nishuhulike mashuleni na vyuo vikuu vishiriki kama DIT na CBE, kwa kuwa nilikuwa na mahusiano na watu wengi huko, DEUS MALLYA alipewa jukumu lingine sambamba na marehemu REGIA MTEMA, lakini kwa pamoja tukawa kwenye kamati ambayo mwenyekiti wetu ni JOHN MNYIKA mimi nikiwa mjumbe kutokea wilaya ya Temeke.
Tarehe 28.07.2008 usiku, CHACHA WANGWE aliuawa PANDAMBILI DODOMA, na mtu aliyekuwepo kwenye tukio hilo ni DEUS MALLYA, nini kilitokea?,
Tarehe  29.07.2008 saa tano asubuhi, JOHN MNYIKA alifanya mkutano na Waandishi wa HABARI, akimkana DEUSI MALLYA kwamba CHADEMA haimtambui, na kwamba SERIKALI iwajibike kuueleza UMMA kwamba DEUS MALLYA ni nani na amewezaje kuwa Dereva wa Chacha wangwe ambaye ni Mbunge huku chama kikiwa hakimtambui DEUS MALLYA wala hakijawahi kumuona mahala popote na kwamba akamatwe Haraka na hatua kali dhidi yake zichukuliwe Haraka.
Maana yake nini?. Ni kwamba MNYIKA na CHADEMA wamemkana DEUS MALLYAkimkakati ili kukiondoa chama kwenye ushahidi wa mauaji ya kiongozi wake mkuu msaidizi.
Jiulize maswali, kwanini MNYIKA alimkana DEUS MALLYA aliyekuwa sio tu rafiki yake lakini mshirika wake mkuu kwenye harakati za ujenzi wa chama?.
Kama hawahusiki Kumuua WANGWE kwanini waogope kiasi cha kumkana mwanachama mwandamizi wao?.
Na kwanini Mbowe alitumia nguvu kubwa sana kuhakikisha Deus Mallya anashinda Rufaa na anafutiwa Kesi?.
Na kwanini Mnyika na Mbowe walimuomba Msamaha Deus Mallya baada ya Kutoka Gerezani kwa kitendo chao cha Kumkana baada ya tukio la mauaji?.
Watanzania wanatambua  kwamba MBOWE, LISSU, SLAA na CHADEMA tumeshiriki kikamilifu kutengeneza matukio ya hatari yenye kuonyesha nchi haitawaliki na upinzani hasa CHADEMA inanyanyaswa na Dola na polisi ili chama kizidi kupata umaarufu wa kisiasa.
Hii ndio maana MBOWE na SLAA wamemtuma kijana mmoja mrefu, mweupe mwenye mazoea ya kufuga nywele nyingi aliyechanganya uraia wa Tanzania na German(ama nchi nyingine ya ulaya)(sitamtaja jina kwa sasa. Mbowe na CHADEMA wanamfahamu) ambaye kwa sasa ni kiongozi katika ngazi ya wilaya mkoa mmoja wa kaskazini kutekeleza mpango wa mauaji kwenye matukio makubwa ya mikutano ya kisiasa hasa inayohusisha vurugu kati ya chadema na polisi na kumuandaa mtu mmoja maalum kwa ajili ya kupiga picha matukio hayo na kusambaza haraka mitandaoni huku mwengine akichukua VIDEO.
Kijana huyu ambaye ni Swahiba wa MBOWE na LEMA, ameweza kutekeleza kazi yake hii Tarehe 05.2.2011 pale ARUSHA kwa kwaua watu kadhaa na kisha umma kuaminishwa kwamba mauaji yale yalifanywa na polisi walipokuwa wanawazuia waandamanaji. Mpaka sasa polisi inahangaika kujinasua kwenye matukio haya ya kutengeneza. Mimi, Mbowe,Slaa, Lissu na Mnyika tunafahamu kila kitu.
Kijana Huyu kwa maelekezo ya MBOWE kupitia kwa SLAA na MNYIKA ili kuwatisha wakazi wa IGUNGA, usiku wa tarehe 9.9.2011 Wakitumia gari namba T587 AZJTOYOTA  LANDCRUISER VX mali ya FREEMAN AIKAEL MBOWE, Mwenyekiti wa CHADEMA, Mbunge wa Hai na Kiongozi mkuu wa Upinzani Bungeni akiwa na HEMEDI SABULA, HENRI KILEWO na JOHN HECHE wakiwa na vijana kadhaa wenyeji wa IGUNGA walimteka na kumtesa sana kijana MUSSA TESHA na kisha kumpeleka Pori la MSITU WA HANI HANI na kummwagia  TINDIKALI Usoni, ili eti vijana wengine waogope kuiunga mkono CCM na vyama vingine.
Na haya yote yalifanywa kwa maelekezo ya SLAA na MBOWE na ndio maana baada tu ya Tukio, Slaa alimuagiza mkurugenzi wa kampeni na uchaguzi aidhinishe malipo ili mkurugenzi wa fedha alipe na vijana hawa wakapelekwa MWANZA na kuhifadhiwa kwenye Hotel ya MAGNUM kwa zaidi ya Mwaka mmoja. Wakiendeshwa na Dereva mmoja maarufu sana wa chadema, sitamtaja kwa leo kwa kuwa alikuwa anatii maelekezo ya viongozi wake.
Mauaji na Mateso yote ya Kijangili yaliyofanywa IGUNGA na ARUMERU yaliwekwa kwenye mpango mkakati wa CHAMA na kupitishwa na KAMATI KUU YA CHAMA.
Ni hatari sana kikao kikuu cha chama kuhalarisha mauaji. Nimeambatanisha na sehemu ya ripoti na mkakati huo wa mauaji.
U wapi sasa uzalendo wa viongozi hawa?, uko wapi uzalendo wa mbowe, uko wapi uzalendo wa Slaa, Lissu na wahuni wenzao wengine?. HAWA NI WAUAJI TU KAMA WAUAJI WENGINE. NA WALAANIWE
MBOWE, SLAA na LISSU, wanajua namna gani walivyomtuma muuaji wao huyu aliyesomea kwa kushiriki kumuua mtu asiye na hatia pale morogoro tarehe 27.08.2012ndugu ALLY ZONA aliyekuwa muuza magazeti pale msamvu, leo hii Dunia nzima inajua kwamba Ally aliuawa na polisi, ila MBOWE, SLAA na CHADEMA wanaujua ukweli halisi.
Wakati Dunia Nzima Leo inaamini kwamba polisi wa F.F.U walihusika kumuua David Mwangosi tarehe 2.9.2012 pale Nyororo Iringa, MBOWE, LISSU, MNYIKA na SLAAwanaujua ukweli, wanajua ni namna gani mchezo huu ulipangwa, namna gani mpiga picha aliandaliwa, namna gani taarifa za awali zilisambazwa na namna gani mlipuaji alifika eneo latukio na kutekeleza kazi yake maalum na baadae kuondoka kwa utaalamu wa hali ya juu, wanafahamu fika. Na kwenye hili pia mpaka sasa polisi wanahangaika kujinasua, lakini bado wamekwama.  
MBOWE, SLAA, LISSU na CHADEMA huku wakishangilia, waliwaagiza vijana wao wampige, na kumdharirisha Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA ndani ya kikao cha kamati kuu Ndugu SHAABAN MAMBO tarehe 3.1.2014 ukumbini MBEZI GARDEN
CHADEMA NI WATEKAJI.
Tarehe 6.1.2014SLAA aliwaagiza HEMEDI SABULA, MEDI, MWAKYEMBE naREDBRIGADE kwenda kufunga OFISI YA MWENYEKITI WA CHADEMA TEMEKE JOSEPH YONAH , na ilipofika SAA TANO USIKU wakamfuata mtaani kwake, wakamteka, wakampiga sana kisha wakaenda kumtupa UNUNIO baada ya kudhani kwamba wameshamuusa.
Na wakati wote wakimpiga na kumtesa walisema wapo Tayari kumsamehe na kumuachia ikiwa tu atakubali kukiri na kurekodiwa kwamba ametumwa na Zitto Kabwe, Mwigulu Nchemba, Usalama wa Taifa kukihujumu CHADEMA. Jambo ambalo si kweli na si sahihi.
Tulipomuokota UNUNIO alipofika Hospitali, SLAA aliwatuma vijana wake kwenda kuiba PF3- na kwa njia walizozijua mpaka sasa PF3 ya YONA ipo mikononi mwa SLAA ambaye kwa kweli ni Muuaji na wala hana huruma.
SLAA akishirikiana na watesi wenzake walimteka, kumtesa na kumjeruhi ndugu JOHN MARWA NYANCHABO, kwa muda wa siku nne kuanzia tarehe 6.02.2014 mpaka tarehe 9.02.2014 na kumfungia ndani ya chumba cha ofisi ya CHADEMA wilayani BAGAMOYO huku wakimlazimisha kusema maneno ya hovyo kwamba ametumwa na CCM na ZITTO kuihujumu CDM na mambo mengine.
Sasa kunihusisha mimi naulipuaji wa helkopta ya Slaa na Mnyika helkopta ambayo waliopanda wana utaalam wa ujangili ni kunikosea heshima. Na kwa kweli kwenye Hili Mwenyezi Mungu wa Rehema atawalaani.
KUHUSU MADIWANI KUHAMIA CCM.
Kuniambia kwamba mimi ndiye niliyewashawishi wahame CHADEMA na wahamie CCM ili kisha wahamie ACT ni utoto ulipitiliza.
Pamoja na kwamba nina mahusiano mazuri sana na Diwani SEBASTIAN PETER – OBAMA.
Ninafahamu kwamba OBAMA alibakisha wiki mbili afukuzwe uanachama wake wa chadema, kama mnyika alivyotangaza pale shinyanga,
Na ninafahamu kwamba OBAMA ni miongoni mwa vijana wanaochukizwa na UBAGUZI wa wazi unaoendelea ndani ya chama, na mimi nayeye uhusiano wetu umeimarishwa hasa na misimamo hiyo.
Hivyo ninakumbuka namna ambavyo alikuwa anapambana kuhakikisha haki yake ya kutokufukuzwa inapatikana, hii ni yeye na diwani wa kahama ndugu SHABAN BOBSON
Na hata alipojiunga na CCM sikushangaa sana nilimpongeza kwa uamuzi wake kwa kuwa alikuwa kwenye political frastruations nay eye ni muandishi wa hatma yake mwenyewe.
Kusema kwamba mimi nilimshawishi ahamie CCM anaongopa, na anaongopa pengine anataka kuwaaminisha kwamba viongozi wengi wa CHADEMA wana uwezo mdogo sana, kiasi kwamba wanaweza kushawishiwa na mtu ambaye siyo mwanaCCM ili wao wajiunge CCM nay eye akabaki kutokuwa mwanaCCM.
Lakini pia OBAMA anajaribu kuonyesha namna ambavyo viongozi wetu wa upinzania wasivyokuwa na misimamo, kama jana alijiunga na CCM na SLAA akatangaza hadharani kwamba huyo ni msaliti na kwamba angefukuzwa muda mchache, leo karudi CDM anaitwa kamanda na mzalendo. Viongozi wa namna hii ikitokea chama kikashinda dola wanaweza wakarubuniwa zaidi na zaidi na kujikuta wanauza nchi kwa ahadi na matarajio ya kitoto
Lakini pia nina fahamu kwamba OBAMA na mwenzake wapo kwenye UJIRA, wamelipwa ama kununuliwa wafanye wanachokifanya ili kunjusuru uhai wa CHADEMA,
Na hili ni azimio halali la kikao kati ya MBOWE, SLAA na viongozi wengine kilichoketi DODOMA wakati wa Bunge la Bajeti, ambapo pamoja na mambo mengine, CHADEMA imeadhimia kuwanunua viongozi na wanachama wote wanaowapinga. Tayari wamefanikiwa kwa OBAMA.
Leo hii Benson Kigaila ametumwa na SLAA kigoma kununua viongozi wengine watoe matamko kama ya OBAMA, na JOHN MREMA yupo TABORA anazunguka wilayani kugawa pesa ili waseme watakayoyasema, Henry Kileo na Kigaila kwa pamoja wamemuhakikishia Joseph Yonah wa Temeke kwamba iwapo atajitokeza hadharani kusema kuwa alikuwa anatumiwa na ZITTO ama na CCM kupitia Mimi basi MBOWE na SLAA watabadilisha maisha yake na kumuahidi donge nono. Tumefanikiwa kuwarekodi wakiongea ujinga huu.
Kwa hiyo sina shaka kwamba madiwani hawa wanalipa walichokula, kwa hiyo ni wakati wao kuendelea kubwabwaja, ukikubali kula cha mtu ukubali pia kuliwa.
Ila wawasaidie tu kuwaambia watanzania kama yale waliyokuwa wanayalalamikia kutendeka ndani ya chadema siku chache nyuma kama tayari yametatuliwa au bado?. Na kwamba Ufisadi wa mbowe waliousema Tayari umeisha ama bado?, kwamba ubadhirifu wa SLAA waliousema Tayari umekoma au Bado?, kwamba mauaji ya mbowe kumuua shelembi wa shinyanga kama walivyosema yamebadilishwa ama bado?.
KUHUSU LEKADUTIGITE NA NSSF
Kila mara Lissu amekuwa akijitahidi kupambana na zitto hata katika maeneo asiyoyaweza.
Mimi habibu Mchange, nimekuwa mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Lekadutigite, kampuni iliyoundwa na wasanii wa kigoma, na haijawahi kutokea hata siku moja zitto ama kampuni kuhongwa pesa kiasi chochote na NSSF na kwamba Lekadutigite walitengeneza wimbo ambao ni Tangazo linaloitangaza NSSF na kupewa milioni 21 kama gharama za Tanzazo hilo na hili ni kwamba wasanii hawa walijitolea walipaswa kulipwa hata milioni 900 kulinganisha na ukubwa wa kazi waliyofanya na ukubwa wa wasanii husika, na maelezo mengine kuhusu malipo ya Nssf na lekadutigite tayari Nssf wenyewe wameshayatolea ufafanuzi.
UNAFIKI WA LISSU.
·         Lissu anasema pesa za NSSF ndizo zilizotumika kulipa hao madiwani. NI UWONGO – LEKADUTIGITE na NSSF mkataba wao wa kazi ni January mpaka February 2013 na walikabidhi kazi kisha wakatumbuiza Arusha mbele wa Makamu wa Rais
·         Niliacha kazi LEKADUTIGITE April 2013 ili kuendelea na siasa hasa kuandaa jimbo langu la uchaguzi la kibaha mjini
·         Zitto na baadhi ya Viongozi wa CHADEMA waligombana mwishoni mwa 2013 na mahakamani ni mwanzoni mwa 2014
·         ACT imeanzishwa mwezi may 2014, wakati hao madiwani wameshaondoka kitambo CHADEMA
Kumuhusisha Zitto na mambo haya ni kuweweseka kwa kiwango cha juu kwa watu hawa. Wao walishamfukuza zitto, wakasema hana impact, sasa yanini wanahangaika naye?, kwanini hawalali wanaweweseka naye?, kwanini wanajihami?, Hawajiamini?, kwanini wanakiogopa kivuli chake?,
Waache kumfuata fuata na waendelee na mambo yao.
Wajifunze kwa Zitto kukaa kimya na kuendelea na Maisha.
Lissu namshauri aache ubinafsi na ubabaishaji.
Dunia nzima inafahamu kwamba alikula milioni 250 za wafadili kwenye shirika lao la kiraia na shirika likafia hapo hapo nay eye kwenda kujenga ghorofa pale tegeta.
Lissu hawezi kuwa kama zitto, zitto ni zitto na lissu ni lissu. Ninamshauri apunguze kukubali kuchukuliwa kama zezeta.
LISSU ni MBINAFSI ALIYEPITILIZA na UBINAFSI WAKE ndio umemfanya mpaka alipoombwa kushauri namna bora ya kupatikana kwa wabunge wa viti maalum kama mwanasheria wa chama, akaweka sharti na kuhakikisha kwanza Dada yakeCHRISTINA LISSU anakuwa Mbunge wa Viti maalum, na ndio maana dada yake alikuwa MBUNGE wa viti maalum wa chadema kwanza kabla ya kuwa MWANACHADEMA. Alipelekewa kadi ya CHADEMA bungenidodoma baada ya kula kiapo cha ubunge.
LISSU NI MROPOKAJI ALIYEKUBUHU, na wote mnafahamu namna alivyotumika kuropoka upuuzi kuhusu watu na taasisi mbali mbali na sasa CHADEMA wanajifanya kuungana nao
Ni lissu ndiye ndiye aliyemtukana na kumdhihaki Prof. BAREGU na kutaka ajitoe kwenye chama ama abaki tume ya katiba kwa kuwa Tume haina weledi
Ni lissu ndiye aliyemzihaki JOSEPH WARIOBA na kusema kwamba anaendesha tume ki CCM CCM na kwamba CHADEMA haiungi mkono kitakachotolewa na Tume. – leo LISSU na CHADEMA wamekuwa makwapani mwa TUME na WARIOBA
Aliwakashifu CUF akawaita WAKE WA CCM, akawakashifu NCCR na MBATIA wao, akawakashifu MAASKOFU na MASHEIKH akawakashifu wazanzibar. Leo aibu ya CHADEMA imefichwa na CUF na NCCR-MAGEUZI.
Aache kuwa mnafiki wa kisiasa.
CHADEMA INAKUFA KWA KASI
Mwisho,
Yanayoendelea kutokea kwenye chadema leo ni kielelezo cha chama Kufa kwa kasi ya ajabu.
Watanzania tumewaongopea vya kutosha sana, tumetengeneza matukio vya kutosha sana, na tumewalaghai watanzania vya kutosha sana.
Sasa hakuna uwongo mpya tunaoweza kuwapa, hakuna tukio jipya tunaloweza kulitengeneza, tumeamua kujitekenya wenyewe halafu tunacheka wenyewe. Hii ni ishara ya kudidimia kwa chama
Wazee wetu wanasema ukiwa mwongo uwe na kumbukumbu, na ukitaka kuruka uagane na nyonga.
Kwa kuwa tulikubali kujenga chama kwa kutegemea mtaji wa uwongo, na chama kimeamua kufa kwa kutumia uwongo huo huo, mwisho wa siku jamii itatucheka kwa kuwazoesha uwongo.
Nitaendelea kusimamia kweli na haki daima Dumu. Nitaendelea kulilinda na kulisimamia Taifa langu milele. Na nitaendelea kupiganian demokrasia ya kweli kila siku
Mungu ibariki Tanzania
‘’SIO MAKOSA YANGU, MAKOSA LABDA YA KAZI’’

Habibu Mchange
0762178678/0658178678
‘’The Freedom Is Not Free’’
Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA