Home » » SPANEST WABUNI MBINU MPYA YA KUPUNGUZA VITENDO VYA UJANGILI ,WAANZISHA MICHUANO KOMBE LA KUPIGA VITA UJANGILI

SPANEST WABUNI MBINU MPYA YA KUPUNGUZA VITENDO VYA UJANGILI ,WAANZISHA MICHUANO KOMBE LA KUPIGA VITA UJANGILI

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Wednesday, July 9, 2014 | 1:37 AM

Na wao walibeba mabango yenye ujumbe huo
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dk Christine Ishengoma na Mratibu wa SPANEST, Godwell Olle Meing'ataki wakikagua timu ya Idodi FC
Hapa wakikagua Kitisi FC
Wakati timu hizo zikiingia uwanjani
Kitisi FC wakionesha mabango yenye ujumbe Piga Vita Ujangili, Piga Mpira, Okoa Tembo
Idodi FC wakiwa na mabango hayo
Wasanii wakiimba wimbo unaohamasisha upigaji vita ujangili

Nyomi ya watu
Mkuu wa Mkoa akamaliza kwa kuzipa neno timu zinazoshiriki ligi hiyo kuxzingatia sheria za mpira
Mbele ya kikombe kinachogombaniwa
Vumbi uwanjani, hivi ndivyo ilivyokuwa
Na waliofukuza kuku na kujinyakulia zawadi ya sh 30,000 walifanya hivi kwa upande wa wanawake
Na kwa upande wa wanaume hali ilikuwa hivi

Add caption

Hapa wakiwa katika mchezo wa kuvuta kamba
Kitisi waliibuka washindi
NGUVU  za  jitihada  za SPANEST katika kulinda wanyama wa hifadhi ya Ruaha Iringa na kupiga  vita  vitendo vya ujangili zimeanza kuonekana baada ya kuja na mbinu mpya ya kuanzisha  michuano ya soka kwa vijana wanaozunguka hifadhi ya Taifa ya Ruaha .

Mratibu wa  SPANEST, Godwell Olle Meing’ataki alisema lengo la ligi hiyo yenye kauli mbiu “Piga Vita Ujangili Piga Mpira Okoa Tembo” ni kuwaunganisha vijana katika vita dhidi ya ujangili wa wanyamapori wakiwemo Tembo.
Alisema wazo la kuunganisha vijana katika vita ya ujangili linaonekana kuwa njia muafaka ya kutokomeza ujangili kutokana na ukweli kwamba vijana ndiyo walengwa wakubwa katika kushawishika kuingia kwenye maeneo yaliyohifadhiwa na kufanya ujangili.

“Takwimu za ujangili katika maeneo yaliyohifadhiwa zinaonesha kuwa vijana wengi hukamatwa katika matukio hayo. Vijana hao hurubuniwa na watu wenye fedha ili wafanye ujangili,” alisema.
Akizindua michuano  hiyo mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dk Christine Ishengoma katika mchezo uliozikutanisha timu ya Idodi FC  na Kitisi FC katika uwanja wa Shule ya Msingi Idodi.

Katika mashindano  hayo wenyeji Idodi FC waliutumia vyema uwanja wao wa nyumbani na kufanikiwa kuibuka vinara kwa kuichabanga Kitisi FC kwa mabao 2-0.

Bao la kwanza la Idodi FC lilipatikana Dk 23 ya mchezo kupitia kiungo wake mkabaji Same Gembe aliyopokea pasi safi kutoka kwa mshambuliaji wao  Maneno Fumbe na kufanikiwa kupiga shuti kali lililomshinda golikipa wa Kitisi FC, Maneno Ng’ingo.

Kipindi cha kwanza kilimalizika kwa Idodi FC kuwa mbele kwa 1-0 bila dhidi ya Kitisi FC walioonekana wachovu muda wote wa mchezo.

Katika kipindi cha pili cha mchezo, Idodi FC waliongeza kasi na katika Dk 55 ya mchezo walifanikiwa kuongeza bao la pili lililofungwa kupitia kiungo mshambuliaji, Amad Kambangwa.

Kuzamishwa kwa bao la pili kuliwafanya wapinzani wao wapoteane zaidi na mpaka kipenga cha mwisho cha mchezo huo kinapulizwa, Kitisi FC walikuwa wamelala kwa bao 2-0.

Mechi hiyo ilitanguliwa na mashindano mengine ya kufukuza kuku na kuvuta kamba kwa wawakilishi wa vijiji vya Idodi na Kitisi.

Akizindua mashindano hayo yatakayozikutanisha timu 21 kutoka vijiji 21 vinavyozunguka hifadhi ya Taifa ya Ruaha,

Kwa mujibu wa Mratibu wa SPANEST, mshindi wa kwanza atapata kikombe, medali ya dhahabu, seti moja ya jezi, cheti, Sh 300,000, kutembelea Hifadhi ya Ruaha.Mshindi wa pili atapata medali ya fedha, mipira 2, cheti na Sh 200,000 taslim huku mshindi wa Tatu akipata medali ya shaba, cheti na Sh 100,00 huku mshindi wa nne akipta Sh 50,000 katika ligi hiyo itakayomalizika Agosti 8, mwaka huu.
Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA