Home » » RADIO COUNTRY FM NA WATUMA SALAM IRINGA WAWAKUMBUKA WAJONGWA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA IRINGA LEO

RADIO COUNTRY FM NA WATUMA SALAM IRINGA WAWAKUMBUKA WAJONGWA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA IRINGA LEO

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Tuesday, July 29, 2014 | 9:39 AM

Mwakilishi wa CFM Abbas Upete  akisoma  risala huku DJ Yeyo kulia  akirusha  hewani  Live
Watuma  salam mkoa  wa Iringa na  wafanyakazi wa Radio  Country Fm Iringa  wakielekea katika Hospitali ya  Rufaa ya  mkoa wa Iringa  kutoa msaada kwa  wagonjwa
Wadau  wa  radio  Country Fm wakiwa katika  Hospitali ya  mkoa wa Iringa ,mwenye kanzu  ni mwakilishi wa Radio  Ebony Fm Dj Kwasa
Meza  kuu
Mratibu  wa CFM Huruma Mgaya  kulia akikabidhi mfano wa mashuka  24  yaliyotolewa na kituo hicho cha radio
Bw Mgaya na msemaji mkuu wa   watumasalam mkoa  wa Iringa Ismail Mlenga baba  Mwadhani  wakikabidhi misaada  yao
Mganga mfawidhi  wa Hospitali ya  Rufaa ya  mkoa wa Iringa Bw D Manyama  kulia akipokea  mashuka  hayo kutoka kwa katibu tawala  wilaya ya Iringa
Picha ya  pamoja
ter" cellpadding="0" cellspacing="0" class="tr-caption-container" style="margin-left: auto; margin-right: auto; text-align: center;">

Mratibu wa Radio  Country Fm Bw  Huruma Mgaya  akieleza  lengo la kufika Hospitali ya  Rufaa ya mkoa wa Iringa

Mmoja kati ya  watuma  salam akimpa  zawadi  mtoto
KITUO cha  Radio  Country  Fm Iringa  kimeungana na umoja  wa watumasalam mkoa  wa Iringa kukabidhi  misaada  mbali mbali  yakiwemo mashuka kwa uongozi  wa Hospitali ya  rufaa ya  mkoa wa Iringa kwa ajili ya matumizi ya    wagonjwa  waliolazwa hospitalini  hapo.

Akizungumza  katika  hafla   hiyo mratibu  mkuu wa shughuli  hiyo Bw  Huruma Mgaya  alisema  kuwa  kituo hicho cha radio Counrty  Fm mbali ya  shughuli nyingine za  kuwajibika kwa jamii kama chomba  cha habari  ila  bado  kimeendelea  kuwa karibu na  wadau  mbali mbali  wakiwemo  watumiaji wa vyombo  vya habari  ikiwemo  radio hiyo kama  watumasalam na  wengine .

Hivyo  alisema  kwa  ushirikiano mkubwa uliopo kati ya  kituo hicho  cha  radio na  wadau wake  wakiwemo  watumasalam mkoa  wa Iringa  walilazimika  kuandaa siku hii ya  leo  kuwatembelea  wagonjwa katika  Hospitali  hiyo ya  Rufaa mkoa  wa Iringa kama  njia ya kuwafariji  ila pia  kuunga mkono  wa  serikali katika  kuiboresha  hospitali  hiyo na kuipandisha hadhi kuwa  Hospitali ya  rufaa ya  mkoa.

Mgaya  alisema  kuwa  mkoa  wa  Iringa ni  moja kati ya  mikoa ambayo  inaendelea  kukua kwa  kasi kutokana  na fursa  zilizopo  za utalii katika  hifadhi  kubwa  ya  Ruaha  vikiwemo  vivutio  vingine  vingi  ambavyo  vimekuwa  vikiwavutia  watalii kufika mkoani  Iringa .

Kwani  alisema katika  kuwawezesha  watalii  zaidi  kupanda  mkoa wa Iringa na mikoa ya nyanda za  juu kusini ni pamoja na kuwepo kwa  huduma  nzuri  za afya kama ilivyo  Hospitali  hiyo ya  rufaa na  wao kama  wadau  wa maendeleo  mkoani Iringa  wasingependa  kuwa nyuma kuunga mkono  jitihada za serikali katika  maendeleo  mbali mbali.

Alisema kuwa  kituo hicho  cha radio Country  Fm kama kituo  kikongwe  zaidi mkoani  Iringa na mikoa ya  nyanda za  juu  kusini kwa kushirikiana na  wadau mbali mbali  wakiwemo  watuma  salam wamekuwa  wakiweka mikakati mbali mbali ya  kuyafikia makundi  yenye mahitaji  wakiwemo  wagonjwa na watoto  yatima na ndio  sababu ya kufika katika Hospitali hiyo  kutoa  misaada mbali mbali kwa  wagonjwa .

Mratibu  huyo alisema kuwa miongoni mwa misaada  iliyotolewa ni pamoja na mashuka ,sabuni ,vikombe na  vitu  vingine  vingi

Pia  aliikumbusha  serikali ya  mkoa  wa  Iringa  kuendelea  kujenga mahusiano  mazuri na vyombo  vya habari na pele  yanapojitokeza  matukio ya kitaifa basi  kuangalia  uwezekano  wa  kuvipa kipaumbele zaidi  vyombo  vya ndani ya mkoa wa Iringa na wanahabari  wake  badala ya  kutoa  wanahabari na vyombo kutoka nje ya mkoa.

Kwa  upande  wake mganga mfawidhi  wa  Hospitali ya rufaa ya mkoa wa Iringa Deogratius Manyama mbali  ya  kuipongeza  radio  Country Fm na  watumasalam na  wadau  wengine  waliounga mkono  zoezi hilo bado  aliwataka  wadau  wengine  kuiga mfano  huo wa kituo hicho  cha radio na  watuma   salam katika  kuisaidia  Hospitali hiyo.
Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA