Home » » MTENDAJI KATA YA MSHINDO AICHAFUA OFISI YA MKURUGENZI ADAIWA KUGEUZA OFISI YAKE MAHAKAMA YA RUFAA

MTENDAJI KATA YA MSHINDO AICHAFUA OFISI YA MKURUGENZI ADAIWA KUGEUZA OFISI YAKE MAHAKAMA YA RUFAA

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Tuesday, July 29, 2014 | 9:39 AM


                                                          Bw  Ayoub Mwenda
BAADHI ya  wanafamilia  wa  familia ya marehemu  Abdalah  Athuman Mwenda  wamepanga  kuandamana kwenda  ofisi ya  mkurugenzi  wa Halmashauri ya Manispaa ya  Iringa Teresia Mahongo  kumlalamikia  afisa  mtendaji  wa kata ya Mshindo mjini  Iringa John Tweve  kwa hatua yake ya  kugeuza ofisi ya kata  kuwa mahakama ya  rufaa kwa  kesi  zinazoshindikana mahakama  za  mwanzo.

Akizungumza mtandao  huu  wa www.matukiodaima.co.tz  mmoja kati ya  wanafamilia  hayo Bw  Ayoub Mwenda  alisema kuwa  mbali ya mahakama ya  mwanzo bomani kutengua  jina la Sadiki Mwenda  kama  msimamizi wa mirathi  hiyo  ila  bado  mtendaji  huyo wa kata  amekuwa akiendelea  kuitumia  ofisi  yake kuitisha  vikao vya  familia  ili  kulazimisha aliyetenguliwa na mahakama  kurejeshwa kama  msimamizi  wa mirathi hiyo kwao  wanaona ni  mwanzo wa  kuchochea mgogolo wa  kifamilia.

Hivyo  alisema  kuwa  walilazimika  kufikisha  jambo  hilo  kwa mstahiki meya wa Manispaa ya  Iringa na  sasa  baada ya mtendaji  huyo  kuendelea na mpango  wake  huo wa kuitisha  vikao kinyume na maagizo ya kimahakama wanakusudia  kesho  kumshtaki  mtendaji kwa mkurugenzi  wa Halmashauri kama mwajiri  wake .
           Hii ni nakala ya  barua  ambayo mtendaji  huyo aliandika kwa  wanafamilia hao
Hivyo  alisema  kutokana na mtendaji  huyo kuendelea  kuitumia ofisi  hiyo  kutafuta suluhu iliyoshindikana mahakamani kutokana na  mahakama ya mwanzo bomani  kutengea jina la aliyekuwa msimamizi  wa   miradhi Sadiki  Mwenda wao  kama  wanafamilia  wamekusudia  kumfikisha  mtendaji huyo kwa  mwajiri  wake.

Pia  Mwenda  alisema  kuwa baada ya  mahakama  hiyo kutengua  jina la Sadiki kutojihusisha na usimamizi wa mirathi hiyo wao  walikuwa  mbioni  kuitisha kikao  cha  wanafamilia ili  kupitia  kikao  hicho kuweza  kuteua mmoja kati yao  kuwa msimamizi  wa mirathi kabla ya  kwenda mahakamani  kuthibitisha  jina lake .

Alisema  kuwa hofu  yao  iwapo ofisi ya mkurugenzi  wa Halmashauri  ya Manispaa ya  Iringa  kupitia mtendaji  huyo wa kata ya mshindo  itaendelea  kutumika  kama  sehemu ya mahakama  ya  rufaa ama  ofisi ya  kuingilia mambo ya  kifamilia  kuna  uwezekano mkubwa wa  kusababisha machafuko  katika  familia.

" Hivi  kama  wanafamilia  tunajiuliza  iweje  mtendaji  huyo wa kata ya Mshindo  Bw  Tweve  kuingilia kati suala  hili ambalo halipo eneo lake  kwani mali  za marehemu kama mashamba yapo kata ya  Nduli  iweje  leo  suala  hilo  lishughulikiwe na kata ya mshindo na   kwa  nini kama mahakama  imetutaka  wana ndugu  kuchagua mmoja  wetu  atakayekuwa  msimamizi wa  mirathi  iweje  mtendaji na yule  aliyekataliwa na mahakama  ndio  wahusike  kutukutanisha ili  tumchague  tena asiyekubalika"

Mwenda  alisema  kuwa mali  zinazohitaji  msimamizi wa  mirathi   ni pamoja na mashamba yenye ukubwa wa zaidi ya hekari 10 na nyingine  japo kuna  tetesi kuwa yupo mmoja mtu nyuma yao anayetaka  eneo hilo.

Kwa  upande  wake  mtendaji  huyo  Bw  Tweve  akizungumza na  mwandishi wa habari hizi kwa njia ya  simu  alikiri kuandika barua ya  kuwakutanisha  wanafamilia  hao japo  alisema  kuwa alifanya hivyo kwa  kutokujua ila hatakubali  kupitisha barua  yao kwa ajili ya kumthibitisha msimamizi wa  mirathi atakayeteuliwa .
Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA