Home » » MBUNGE GODFREY MGIMWA AKABIDHI MSAADA WA BATI KIJIJI CHA USENGERENDETI NA MAHANZI

MBUNGE GODFREY MGIMWA AKABIDHI MSAADA WA BATI KIJIJI CHA USENGERENDETI NA MAHANZI

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Monday, July 14, 2014 | 11:06 PMKatibu  wa mbunge  wa jimbo la Kalenga  Bw  Martine Simangwa  kushoto akikabidhi msaada wa bati  100 kwa  uongozi wa kijiji cha Usengerendeti  kwa  ajili ya ujenzi wa nyumba ya wauguzi wa Zanahati ya  kijiji  
Wananchi  wakishiriki kushusha  bati  hizo
Katibu  wa mbunge Mgimwa Bw Martine Simangwa akieleza kazi mbali mbali  zilizofanywa na mbunge Godfrey Mgimwa toka alipochaguliwa 
Katibu wa mbunge Mgimwa Bw Martine  Simangwa kushoto akikabidhi bati 80  kwa uongozi wa  serikali ya  kijiji  cha Mahanzi  kwa ajili ya ujenzi  wa vyumba vya madarasa katika  kijiji hicho kipya 
 Wananchi  wakimpongeza  katibu wa Mgimwa kwa niaba ya mbunge wao Godfrey Mgimwa 
......................................................................................................................................................
MBUNGE  wa  jimbo la  Kalenga  Godfrey  Mgimwa ametoa  msaada wa  bati 180 zenye tahamani ya  zaidi ya Tsh milioni 1 kwa  kata ya  Wasa kwa  kama  sehemu ya  utekelezaji wa ahadi zake  katika kata  hiyo.

Akikabidhi msaada  huo   kwa niaba ya mbunge Mgimwa katibu  wake Martine Simangwa alisema  kuwa  bati  hizo  ni   sehemu ya jitihada za mbunge  huyo kuunga  mkono  harakati za wananchi  katika  kuibua miradi ya kimaendeleo katika maeneo yao.

Hata  hivyo  alisema kuwa bati hizo 100 ni kwa ajili ya  kijiji  cha Usengerendeti ambao  wapo katika  ujenzi wa nyumba  ya  waganga katika  Zahanati ya  kijiji na bati  80 kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa  shule katika  kijiji kipya   cha Mahanzi .


Alisema kuwa moja kati  ya mambo ambayo mbunge  Mgimwa ameyawekea  kipaumbele zaidi ni pamoja na elimu pamoja na afya  na kuwa  jitihada za kuhakikisha  mambo  hayo yanashughulikiwa  zinafanyika .

Pia  alisema katika  kuhakikisha maendeleo ya  jimbo  hilo la Kalenga  yanaendelea  kusonga  mbele zaidi ni  vema  wananchi  wa  jimbo  hilo kuelekeza  nguvu zao katika maendeleo na kuachana na  baadhi ya  watu wanaopita katika  jimbo  hilo kwa ajili ya kuutaka ubunge mwaka 2015.

Kwani  kufanya hivyo ni kuendelea  kurudisha  nyuma maendeleo ya  jimbo  hilo na kuwataka  wanaofanya hivyo  kwa sasa  kusubiri  muda  ukifika ndipo  wananze  kujipitisha  na kuwa kimsingi katika nafasi ya  ubunge hakuna mbunge kivuli hivyo  kitendo cha  watu hao wanaojipitisha  kufanya hivyo kwa  sasa ni kuvuruga kasi ya maendeleo ya  jimbo  hilo.

Akizungumzia  kuhusu  suala la afya  katika  jimbo hilo alisema kuwa hali ya huduma ya afya  bado si mbaya  sana  japo kuna  changamoto mbali mbali ambazo  zinapaswa kushughulikiwa  ikiwemo ya dawa pamoja ,ukosefu wa  nyumba za  watumishi wa afya na baadhi ya maeneo  zahanati na  vituo hivyo vya afya  kukosa umeme.

Awali  wananchi  wa kata  hiyo ya   Wasa  walimpongeza  mbunge  huyo kwa  kuonyesha  uaminifu kwao na hata  kuanza  kutimiza ahadi  zake kwa wakati mfupi  zaidi  ukilinganisha na  wabunge  wengine  waliopata  kuongoza  jimbo  hilo ambao hadi  wameondoka madarakani  baadhi ya ahadi  hawajatekeleza kwa  wananchi.

Alisema Yohana Sanga  kuwa  jimbo la Kalenga kwa  muda  mrefu  limekuwa ni  jimbo linaloongoza kwa kubadili  wabunge kwa  kila kipindi  kimoja na ndi  sababu ya  jimbo  hilo  kuendelea  kuwa nyuma katika maendeleo  ukilinganisha na majimbo ambayo  wabunge wake wameongoza kwa  zaidi ya kipindi  kimoja na kuwa kwa  sasa wao  hawana haja ya  kubadili mbunge mwingine  zaidi ya Mgimwa .
Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA