Home » » LORI LAACHA NJIA LAGONGA NYUMBA LAUA WATANO PAPO HAPO , LAJERUHI WATATU IRINGA

LORI LAACHA NJIA LAGONGA NYUMBA LAUA WATANO PAPO HAPO , LAJERUHI WATATU IRINGA

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Wednesday, July 16, 2014 | 4:47 PM

dereva  wa  lori  hilo Bw Kasimu Ahmed Mambo akipel;ekwa wodini katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Iringa usiku huu
Nyumba ambayo ilikuwa  klabu cha pombe iliyogongwa na lori hilo na kusababisha  vifo vya  watu  watano papo hapo usiku huu
Majeruhi Mussa Abdalah Kadege (34) utingo ambae ni makazi wa Kijiweni akipelekwa wodini
Hili ndilo  lori lililosababisha ajali  hiyo likiwa limelowa  damu
AJALI mbaya ya gari im,etokea usiku  wa leo  mkoani Iringa baada ya lori  la mizigo lenye namba za  usajili T 801 ACD lililokuwa  likielekea mkoani Mbeya  kuacha njia na kugonga  nyumba iliyokuwa ikitumiwa kama sehemu ya klabu cha kuuzia pombe za  kienyeji na kusababisha  vifo vya watu  watano papop hapo wakiwemo watatu wa familia moja.


Tukio  hilo limetokea majira ya saa 4 usiku wa  leo  katika eneo la njia panda ya makumbusho ya Isimila kata ya Mseke wilaya ya Iringa  katika barabara kuu ya Iringa - Mbeya .

Mashuhuda  wa  tukio  hilo  waliozungumza na mtandao  huu  wa www.matukiodaima.co.tz eneo la  tukio akiwemo John Kalinga alisema kuwa  wakati ajali hiyo ikitokea  watu  hao  walikuwa  wakiendelea kunywa  pombe katika  klabu  hicho  na ghafla walijikuta wakifuatwa na lori  hilo ambalo  lilikuwa  limeacha njia .

Alisema  kuwa wakati  tukio hilo  likitokea  baadhi  yao  walikuwa nje ya  klabu  hicho  hivyo kulazimika  kukimbia huku  wakipiga kelele  kuwataka wale  waliopo ndani kukimbia japo hawakufanikiwa kukimbia kutokana na lori hilo  kuwa tayari  limekwisha isambaratisah  nyumba  hiyo.

Hata  hivyo  alisema muuzaji wa klabu hicho kwa wakati huo alikuwa ametoka nje kwenda nyumba  ya  pili kuchimba  dawa na wakati akiwa  huko alisikia kelele  za  watu  kutoka klabuni kwake na wakati akisogea  ndipo  aliposhuhudia  watu hao  wakikutwa na mauti.

Kwa mujibu wa jeshi la polisi  waliopoteza maisha ni pamoja na Leonard Mkendela (35),Neema Mkendela na Kamsia Mkendela wote  wa familai moja wakati  wengine ni Ester  Mwalomo na Oscar Zosama (25) wote  wakazi wa eneo  hilo la Isimila .

Huku majeruhi wa ajali  hiyo ni pamoja na  Kasimu Ahmed Mambo(44) mkazi  wa Kijiweni ambae  ndie  dereva wa lori hilo  ,Mussa Abdalah Kadege (34) utingo ambae ni makazi wa Kijiweni na  Juma Abdalah Omary Ally (40) ambae  anadaiwa  kwa wakatyi  huo alikuwa akiendesha  lori hilo na kusababisha ajali hiyo

Majeruhi  wote  watartu  wamelazwa  katika  Hospitali ya Rufaa ya  mkoa wa Iringa huku  wawili wakiendelea vizuri na mmoja Bw Juma Omary Ally hali yake  ikiwa mbaya zaidi na amelazwa  wodi la  wagonjwa mahututi akipumua kwa mashine .
Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA