Home » » AIRTEL YATOA FUTARI KWA WATOTO YATIMA MKOANI MWANZA.

AIRTEL YATOA FUTARI KWA WATOTO YATIMA MKOANI MWANZA.

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Monday, July 14, 2014 | 11:07 PMMeneja  Biashara Kanda ya Ziwa Raphael Daudi (wa tatu kutoka kulia) akiwa na Meneja wa Masoko Kanda Emanuel Raphael (wa kwanza kulia) pamoja na  Meneja wa Airtel mkoa wa Mwanza David Wankulu wakikabidhi msaada wa chakula cha kufuturisha katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani  kwa Katibu mkuu wa Jumuiya ya Kuendeleza Quran na Suna Tanzania (JUQUSUTA)  Twaha bin Bakari Utari (wa tano kutoka kulia) akiwa katika picha na wadau wengine wa Kituo cha watoto yatima cha Sharif Said Al-Bith kilichopo eneo la Nyegezi Majengo Mapya jijini Mwanza.
Vijana wa Kituo cha watoto yatima cha Sharif Said Al-Bith kilichopo eneo la Nyegezi Majengo Mapya jijini Mwanza wakishusha vyakula toka katika gari la wadau wa Airtel ambao wamedhuru katika kituo hicho kwaajili ya kusababisha tabasamu kwa watoto hao kwa kipindi hiki cha mfungo wa Mwezi mtukufu wa Ramadhani..
Upakuaji ukiendelea.
Ni sukari, chumvi, majani ya chai, mchele, sabuni, mafuta, unga wa sembe, unga wa ngano, juice za matunda na vinginevyo kama sehemu ya msaada wa chakula toka Airtel Tanzania kwa Kituo cha watoto yatima cha Sharif Said Al-Bith kilichopo eneo la Nyegezi Majengo Mapya jijini Mwanza.
Meneja wa Airtel mkoa wa Mwanza David Wankulu (kushoto) akiwa na Meneja wa Masoko Kanda Emanuel Raphael wakisaidizana kufanikisha shughuli hiyo ya makabidhiano. 
Mafuta kwa  Kituo.
Vijana wa Kituo cha watoto yatima cha Sharif Said Al-Bith kilichopo eneo la Nyegezi Majengo Mapya jijini Mwanza katika picha ya makabidhiano na wadau wa Airtel. 
"Hawa ni watoto wetu, hivyo tunapaswa kuwalinda" Kauli ya pamoja ya wadau wa Airtel kwa wale wote wenye mapenzi mema.
Share this article :

+ comments + 1 comments

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA