Home » » Airtel Divas yatembelea kikundi cha Sauti ya walemavu kwenye Maonyesho ya Biashara ya Sabasaba

Airtel Divas yatembelea kikundi cha Sauti ya walemavu kwenye Maonyesho ya Biashara ya Sabasaba

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Saturday, July 5, 2014 | 12:52 AM

Wanachama wa Kikundi cha Wanawake wafanyakazi wa Airtel Tanzania ‘Airtel Divas’, Meneja wa Huduma kwa Jamii, Hawa Bayumi (kushoto), Afisa Uhusiano, Jane Matinde (wa pili kushoto), na Afisa mauzo, Rachael Mboya (kulia), wakichagua bidhaa zilizotengenezwa na Kikundi cha Sauti ya Wanawake wenye Ulemavu Tanzania (SWAUTA) cha Kinondoni, walipotembelea Banda la Swauta, lililopo katika Uwanja wa Maonyesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba), barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam jana. Airtel Divas ilikiwezesha kikundi hicho, kupata pesa kwa ajili kulipia banda hilo.Umoja wa kikundi cha wanawake cha Airtel Divas leo kimetembelea kikundi cha sauti ya wanawake walemavu Tanzania (SWAUTA) katika banda lao lililopo katika maonyesho ya Sabasaba jijini Dar es Saalam

Airtel Divas wamefanya hivyo hivyo ikiwa ni muda mfupi tu tangu walipofanya harambee ya kukiwezesha kikundi hicho kupata fedha za kulipia banda katika viwanja vya maonyesho ya 38 ya kimataifa maarufu kama Sabasaba ili nao kuonyesha bidhaa zao kwa watanzania

Akiongea wakati wa ziara hiyo, mwanachama wa Umoja wa wanawake wa Airtel na Meneja Huduma kwa jamii  Hawa Bayumi alisema” Airtel Divas tunayofuraha kuona tumeweza kuwasaidia kina mama wenzetu kutimizia lengo lao na kuwapa nafasi yakuweza kuonyesha ubunifu wao  uwezo wao na kazi zao za mikono kwa washiriki na wateja wa ndani na wanje wanaotembelea maonyesho haya ya Sabasaba
Ni matumaini yetu kuwa fulsa hii ya kuonesha na kujitangaza hapa saba saba itawawezesha kufikia malengo yao ya kutanua wigo wa biashara zao na kupata masoko na kuuza bidhaa zao kwa wingi zaidi.
Tunatoa wito kwa watanzania kujitokeza na kuwaunga mkono kina mama hawa katika banda lao lililoko Benjamini Mkapa
Kwa upande wake Mwanachama wa Umoja wa sauti ya walemavu Tanzania Bi Adelina Mluge Alisema 
“Tunawashukuru sana Airtel kwa kutuwezesha kuwepo katika mazingira mazuri ukilinganisha na ilivyokuwa na miaka iliyopita. mpaka sasa tumeweza kupata wateja wengi wakipita hapa kuona na kununua bidhaa zetu  kwa wingi. Tunategemea kufanya vyema katika maonyesho ya mwaka huu kutokana na maboresho haya na hivyo basi tunaishukuru sana kampuni ya Airtel kwa kujitolea kutusaidia  

Airtel kupitia huduma zake za jamiii imeweza kuwafikia jamii na kuwawezesha kupata huduma muhimu hususani katika elimu,  Airtel kwa kupitia Divas Airtel inaendelea kusaidia jamii katika maeneo mbalimbali ikiwemo kina mama hawa wa umoja wa sauti ya walemavu Tanzania.
Mwisho
Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA