Home » » UTENDAJI KAZI WA MBUNGE MGIMWA WAWAKUNA VIONGOZI WA DINI ,WASEMA JIMBO LIMEPATA MBUNGE

UTENDAJI KAZI WA MBUNGE MGIMWA WAWAKUNA VIONGOZI WA DINI ,WASEMA JIMBO LIMEPATA MBUNGE

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Sunday, June 8, 2014 | 1:23 AM

Mchungaji Aikam Chavala akimpongeza mbunge wa jimbo la Kalenga Godfrey Mgimwa katika mkutano wa hadhara  leo Ihemi

Mbunge Mgimwa akipongezwa na mchungaji Aneth Fweni leo Ihemi 
......................................................
MBUNGE wa  jimbo la Kalenga Godfrey Mgimwa awakuna viongozi wa  dini kwa  utendaji kazi  wake wadai  kuwa  ni wakati  wake  kuliletea maendeleo  jimbo  hilo.
Wakizungumza na katika mkutano wa hadhara ulioandaliwa na mbunge Mgimwa kwa ajili ya kuwashukuru leo katika  kijiji cha Ihemi viongozi hao akiwemo mchungaji  wa kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) usharika  wa Ihemi Aikam Chavala na mchungaji Aneth Fweni walisema  kuwa huu ni  wakati wake mbunge  huyo  kuongoza  jimbo hilo .
Huku  wakidai  kuwa kazi  yao kama  viongozi wa  dini ni kuendelea  kumwombea kwa Mungu afya  njema kwani  hawajapata  kuwa na mbunge kama  huyo ukiacha mbunge Dr Wiliam Mgimwa aliyefariki ambae  pia utendaji kazi  wake  ulikuwa ni wa mfano.
Hivyo walisema  kuwa  wanajivunia kuwa na mbunge  kijana na mchapa kazi kama   huyo na  hivyo kumpongeza na kumwomba azidi  kuwatumikia vema wananchi.
Kwa  upande  wake  diwani wa kata ya Ihemi Denis Lupala alisema  kuwa wananchi  wa   kata ya Ihemi  hawapendi kuona mbolea ya minjingu katika kata  hiyo na kuitaka  serikali kuacha mara  moja kuwaletea mbolea  hiyo na kuwa kama Mbeya  wameikataa na Arusha inakotengenezwa hawaitumii iweje wao waletewe.
Hivyo alimtaka  waziri wa kilimo kusikia kilio cha wananchi  juu ya mbolea  hiyo na  kuwa iwapo hata fanya hivyo basi ni  vema serikali kuacha kabisa  kuwapa ruzuku ya mbolea kama hiyo.
Lupala alimwomba mbunge  Mgimwa  kusaidia  kutatua  suala  hilo la mbolea ya mijingu kwa  kuwasemea  bunge  na pia kuwasaidia kutatua kero ya mwekezaji katika kata  hiyo ambae amekuwa kero  kubwa na hata  kufunga barabara na kuwa iwapo mwekezaji  huyo ataendelea  hivyo  watafanya maandamano hadi kwa  waziri wa wizara  husika .
Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA