Home » » REDDS MISS IRINGA 2015 KUPATIKANA KESHO , RC IRINGA KUSHUHUDIA

REDDS MISS IRINGA 2015 KUPATIKANA KESHO , RC IRINGA KUSHUHUDIA

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Thursday, June 19, 2014 | 5:16 AM


Baadhi ya  washiriki wa shindano la Redds Miss Iringa 2014 ambao kesho watapanda  ulingoni kuwania taji hilo 

 mratibu  wa Redds Miss Iringa 2014 Victor Chakudika akizungumza na mtandao  huu wa matukiodaima ofisini kwake leo 
.................................................................................................................................................
MKUU  wa  mkoa  wa Iringa Dr Christine Ishengoma kuungana na wakazi wa  mkoa  wa Iringa kumshuhudia mrembo atakayevishwa  taji la Redds Miss Iringa 2014.

Katika kinyang'anyiro hicho kinacho kutanisha warembo 11 kutoka chuo kikuu  cha Iringa ,Ruco na vyuo vingine vya mkoa  wa Iringa na warembo wakali  kutoka nje ya vyuo ,mkuu huyo wa mkoa anatarajiwa  kuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo itakayofanyika usiku wa  kesho ijumaa katika ukumbi wa St Dominic .

Awali  shindano hilo  lilipangwa kufanyika Juni 6 mwaka huu  lilikwama  kufanyika baada ya mratibu wake aliyepewa kibali na  kamati ya Redds Miss Tanzania  kuingia mitini bila ya  kufanyika kwa onyesho .

 Kutokana na hali  hiyo ili  kunusuru  mkoa wa Iringa  kukosa mwakilishi katika shindano la Redds Miss Tanzania kamati ya  Redds Miss Tanzania chini ya mratibu  wake  Hashim Lundenga walilazimika kumpa mratibu mpya kutoka kampuni ya Chakudika Intertainment chini ya mkurugenzi wake Victor Chakudika ambaye ni Meneja wa kituo cha radio ya Nuru Fm  ya mkoani Iringa .


Hata  hivyo kampuni  hiyo  imeweza kufanya kazi  hiyo ya kuhakikisha inafanya maandalizi makubwa ya  kusaka warembo na  wadhamini ambao  wangewezesha shindano hilo kufanyika .

Akizungumzia maandalizi ya shindano hilo mratibu wa kampuni hiyo Chakudika alisema maamuzi ya kuandaa shindano la Redds Miss Iringa kwa lengo a kutopoteza vipaji vya mabinti waliokuwa tayari kushiriki shindano hilo na kuondoa aibu ya mkoa wa Iringa kutopelekwa mwakilishi katika shindano la Redds Nyanda za Juu ambako wamekuwa wakishiriki kila mwaka.
Alisema kuwa shindano la Redds Miss Iringa limekuwa chachu ya ajira kwa mabinti wengi mkoani hapa kwa kuweza kutangaza vipaji vya washiriki wanaojitokeza kushiriki kila mwaka.
Chakudika alisema shindano hilo linatarajia kuwa la kisasa kutokana na maandalizi yake kuendelea vyema na kuwataka wadau wa tasnia ya urembo ujitokeza kwa wingi katika ukumbi wa St. Dominic likalofanyika shindano hilo.
Aliongeza kuwa hadi sasa warembo 11 wamejitokeza kushiriki shindano hilo na wanaendelea na mazoezi katika ukumbi wa Hotel ya Gentle hill ya mjini hapa.
Aidha msanii Mo Music anayetamba na wimbo wake wa ‘Basi Nenda’ anatarajia kutoa burudani kali katika shindano hilo ,wasanii wengine chupukizi wa mjini Iringa, vikundi vya sanaa, Wakali wa Kudance wa mjini Iringa.

Aliwataja wadhamini wa shindano hilo licha ya TBL kupitia kinywaji chake cha Redds, wengine ni Nuru Fm, kampuni mpya ya mabasi ya Sutco High Class, Gentle Hills na kuwataka wadau zaidi kujitokeza kudhamini shindano hilo.

Chakudika alisema  kuwa kiingilio  ni kati ya Tsh 10000 na 20,000 kwa V.I.P na mshindi wa taji  hilo ataondoka na fedha   kiasi cha Tsh 500,000 ,mshindi wa  pili atapewa Tsh 300,000 na mshindi wa tatu atazawadiwa  kiasi cha Tsh 200,000 wakati  washiriki  wengine  wote watapata  kifuta jasho  cha Tsh 100,000 kila mmoja .

Usikose kushuhudia Redds Miss Iringa 2014 mtandao huu utarusha  moja kwa moja hapa kesho 
Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA