Home » » MAUREEN GODFREY KUTOKA NJOMBE AWA REDDS MISS KANDA YA NYANDA ZA JUU KUSINI 2014 , IRINGA ,NJOMBE NA RUVUMA KWENDA TAIFA

MAUREEN GODFREY KUTOKA NJOMBE AWA REDDS MISS KANDA YA NYANDA ZA JUU KUSINI 2014 , IRINGA ,NJOMBE NA RUVUMA KWENDA TAIFA

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Saturday, June 28, 2014 | 4:07 AM

Mshindi  wa  taji la Redds Miss Kanda ya nyanda za juu kusini mwaka 2014 Maureen Godfrey akiwapungia mkono  wadau wa  urembo katika ukumbi wa Highlands usiku wa kuamkia leo  baada ya  kutangazwa mshindi
kaimu mkuu wa mkoa wa Iringa Gerald Guninita kulia akimpongeza mshindi wa taji la Redds Miss kanda ya nyanda za juu kusini mwaka 2014 Maureen Godfrey baada ya kutawazwa mshindi  usiku wa kuamkia leo
 Mrembo  Maureen Godfrey katikati akiwa na washindi  wa nafasi ya  pili Martha John na mshindi wa tatu Naba Magambo katika  picha ya pamoja 
........................................................................................................
ZOEZI la  kumsaka Redds Miss kanda ya  nyanda za juu  kusini limekamilika kwa Redds Miss Njombe 2014   Mrembo Mauren Godfrey kutoka mkoa wa Njombe kufanikiwa  kushika nafasi ya kwanza katika kinyang'anyiro  hicho .

Huku  mkoa  wa Iringa  ukiwakilishwa na Martha John aliyekuwa Redds Miss Iringa 2014 na mkoa wa Ruvuma ukiwakilishwa na mrembo  wake  Naba Magambo ambae  ni Redds Miss Ruvuma 2014  kwa  ushindi  huo  warembo hao wa tatu  ndio  watakaopeperusha bendera ya urembo ya mikoa ya nyanda za  juu kusini katika kinyang'anyiro  cha kumsaka Redds Miss Tanzania 2014

Katika shindano  hilo lililofanyika usiku wa kuamkia leo  katika  ukumbi wa Highlands mjini Iringa na kushuhudiwa na kaimu mkuu wa mkoa wa Iringa Gelard Guninita mrembo Maureen aliweza  kumpokea  taji  hilo aliyekuwa Redds Miss Kanda ya nyanda za juu kusini mwaka 2013 Lina Allan  ambae alipokea  taji  hilo mwaka 2011 kutoka kwa Christine Wiliam .

Katika  kinyang'anyiro  hicho warembo Salome George ,Magreth Tarimo,Naba Magambo,Elizabeth Mussa,Maureen Godfrey,Martha John,Juliana Gilbert,Flaviana Msalila,Faina Salum na Atukuzwe Fabian ndio  ambao  walifanikiwa  kuingia hatua ya  kumi bora na kupelekea  kuingia katika wakati mgumu  zaidi wa kuenguliwa kwa maswali.

Katika  hatua  hiyo ya kumi  bora majaji  walilazimika  kufanya mchujo na kuwapata  watano  bora ambao ni 
Maureen Godfrey,Naba Magambo,Faina  Salum,Atukuzwe  Fabian  na Martha John kabla ya  kumpata mshindi wa kwanza hadi tatu kwa njia ya maswali .

Maureen na wenzake  wawili  waweza  kung'ara  zaidi katika kinyang'anyiro  hicho baada ya  kuonyesha uwezo mkubwa wa  kujibu maswali na kujieleza  zaidi na kupewa  baraka za kuiwakilisha kanda ya nyanda za juu kusini katika kinyang'anyiro kama  hicho ngazi ya taifa .

Awali mratibu wa mashindano hayo Doss Magambo  alisema kuwa mshindi wa kwanza katika kinyang'anyiro  hicho atazawadiwa kiasi  cha Tsh milioni 1  wakati mshindi wa pili atazawadiwa  kiasi cha Tsh 500,000 na mshindi wa tatu atazawadiwa kiasi cha Tsh 300,000 huku  kila mshiriki atapewa  kiasi cha Tsh 80,000 kama  kifuta jasho zoezi ambalo litafanyika siku  moja baada ya shindano
Share this article :

+ comments + 2 comments

May 22, 2015 at 11:02 PM

very nice kwa kuiinua njombe

May 22, 2015 at 11:03 PM

very nice kwa kuiinua njombe

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA