Home » » Wanajeshi wa Kenya wauawa na Al Shabaab

Wanajeshi wa Kenya wauawa na Al Shabaab

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Monday, May 26, 2014 | 9:45 PMWapiganaji wa Al Shabaab

Serikali ya Kenya imethibitisha kuwa maafisa wake wawili wa jeshi wameuawa na wengine wawili kujeruhiwa, baada ya wapiganaji wa Kiislamu wa Al Shaabab kufanya shambulio la kuvizia, baada magari yao kukwama barabarani huko Somalia.

Ripoti zinasema msafara wa wanajeshi wa Kenya ulikuwa ukielekea eneo la Ras Kamboni wakati shambulio hilo lilipotokea.

Kamanda wa polisi mjini Mombasa Robert Kitur amethibitishia BBC kuwa shambulio hilo limetokea.
Kwa upande wao, msemaji wa Al shabaab, Abu Mus'ab amedai kuwa wapiganaji wake walifanikiwa 

kuteketeza magari kadhaa ya jeshi la Kenya, madai ambayo yamekanushwa vikali na utawala nchini kenya.
Aidha amesema wa wapiganaji kadhaa wa Al shabaab waliuawa na wengine kujeruhiwa wakati wa makabiliano hayo.
Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA