Home » » KISWAGA AKIWEZESHA KIKUNDI CHA VIKOBA CHA TWIYENDAGE KALENGA

KISWAGA AKIWEZESHA KIKUNDI CHA VIKOBA CHA TWIYENDAGE KALENGA

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Monday, March 31, 2014 | 5:27 AM


Wanachama  wa  kikundi  cha Vicoba cha Twiyendage  Kalenga  wakimpokea Jackson Kiswaga  leo
Mtendaji  wa kijiji cha Kalenga  akimkaribisha Kiswaga  kuzindua  kikundi hicho
Wanachama wa  Twiyendage Vicoba  wakisoma Risala yao kwa  Kiswaga
Kiswaga  akifuatilia risala kwa makini
wanachama  wa  Twiyendage Vicoba  wakifurahia hotuba ya Kiswaga
Kiswaga  akizindua kikundi  cha Vicoba  cha Twiyendage Kalenga
Kiswaga akiwa na  wanachama wa kikundi  cha Vicoba Twiyendage Kalenga mara  baada ya kuzindua  kikundi hicho
Aliyekuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa kikundi   cha Twiyendage   Vicoba Kalenga ,mkurugenzi  wa kampuni ya Tigo nyanda za  juu  kusini Bw Jackson Kiswaga  akimkabidhi mwenyekiti  wa kikundi hicho Bi Mwahija Witala msaada  wa fedha kiasi cha Tsh 500,000 kati ya shilingi 700,000 alizoahidi kwa kikundi hicho
MKURUGENZi  wa  kampuni ya  simu ya Tigo kanda  ya nyanda za  juu  kusini  Jackson  Kiswaga  amechangia  kiasi cha Tsh 700,000 kwa  ajili ya  kukiwezesha  kiuchumi kikundi cha Vicoba cha Twiyendage kata  ya Kalenga  wilaya ya Iringa .

Kiswaga  alikabidhi msaada  huo leo wakati wa   uzinduzi  wa kikundi  hicho  chenye  wanachama 30 kama  njia ya  kuunga  mkono  jitihada za  wanawake  hao katika  kujiletea maendeleo.

Akizungumza  wakati  wa   uzinduzi  wa  kikundi  hicho  Kiswaga  aliwataka  wanachama wa  kikundi hicho kuzidi  kuwahamasisha  wenzao  kujiunga na  vikundi  kama  hivyo kama  njia ya  kujikwamua  kiuchumia na  kuwataka  wanachama  kujenga utamaduni  wa  kurejesha  mikopo  pindi wanapokopeshana .

Kwani  alisema  iwapo  wanachama  wengi  zaidi  watahamasishwa  kujiunga na vikundi hivyo  vya  kiuchumia upo uwezekano mkubwa  wa  serikali na  taasisi  mbali mbali za kifedha kuunga mkono  jitihada za  vikundi  hivyo.

"Awali  ya  yote ninapenda  kuwashukuru wanachama kwa  kunialika  kuwa mgeni rasmi hapa  leo ila bado napenda  kuwatia nguvu kwa  kuwachangia  kiasi  cha Tsh 700,000 ili  kuongeza mtaji  wenu zaidi ... ili  kuweza kujikomboa  kimaisha  ni lazima  kuanzisha  vikundi kama  hivi vya kiuchumia"

Awali  mwenyekiti  wa  kikundi hicho Mwahija Witala alisema  kuwa  kikundi  hicho kina  wanachama  30  kutoka makundi  mbali mbali ya  kijamii  wakiwemo   walimu, wakulima wafanyabiashara  na wa wale  wasio  kuwa na ajira .

Witala  alisema  hadi  sasa  kikundi  hicho  kina mtaji wa Tsh milioni 3 na lengo ni  kuendelea  kusaidiana  zaidi ikiwa ni pamoja na  kusaidia makundi mbali mbali ya jamii yaayowanzunguka  wakiwemo  watoto  yatima.
Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA