Home » » ZITTO KABWE -NITAPAMBANA KUTETEA UANACHAMA WANGU

ZITTO KABWE -NITAPAMBANA KUTETEA UANACHAMA WANGU

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Monday, December 23, 2013 | 5:02 AM
Kwa upinzani ni lazima tufanye tofauti na CCM. Tuhuma za matumizi mabaya ya fedha za umma kwa upinzani ni mbaya zaidi kuliko.
 Hivyo uwajibikaji kwa wote bila kujali vyama. Uwajibikaji sio msamiati kwa watawala tu bali kwa viongozi wote.
 Namna tunavyotaka nchi iendeshwe ndivyo hivyo tuendeshe vyama vyetu. Tuhuma dhidi ya Kiongozi wa Upinzani kuhusu masuala ya uadilifu zinapaswa kuhukumiwa kwa namna ile ile wanayohukumiwa watawala.

Ninarudia kuwaambia ndugu zangu kwamba sitoki CHADEMA. Chama kina jasho langu na nitapambana mpaka dakika ya mwisho kutetea haki ya uanachama wangu. 

Mimi ni CHADEMA toka ujana. Niliingia CHADEMA kwa kuchagua na sio wengine walioingia kwa Mazingira Ya kupata fursa za kugombea. Wengine wangepitishwa na chama walichokuwa kuwa wagombea Leo wasingekuwa upinzani na inawezekana wangekuwa mawaziri mizigo au waendesha operesheni tokomeza!

Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA