Home » » WAZIRI WA FEDHA DR MGIMWA HAJAFARIKI DUNIA -FAMILIA

WAZIRI WA FEDHA DR MGIMWA HAJAFARIKI DUNIA -FAMILIA

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Monday, December 23, 2013 | 6:29 AM                                                     Waziri wa fedha  Dr Wiliam Mgimwa
 Mdogo  wa waziri  Dr  Mgimwa   Bw Joachim Mgimwa
 .........................................................................................................
WAKATI  kukiwa na uvumi  mbali  mbali  juu  ya afya ya  waziri  wa  fedha Dr Wiliam Mgimwa(pichani) ambaye  amelazwa  nchini Afrika  kusini kwa matibabu  kwa  zaidi ya  wiki  mbili  sasa,familia ya waziri  huyo imekanusha   taarifa  kifo  cha  waziri  huyo na  kuwa ni mzima  wa afya na anaendelea  kupatiwa matibabu.

Mdogo  wa waziri  Dr  Mgimwa   Bw Joachim Mgimwa ambae  yupo  nchini Afrika ya Kusini  akimuuguza  kaka  yake  ,alisema  kuwa  amekuwa  akipokea simu  kutoka kwa  watanzania kutoa  maeneo mbali mbali  wakitaka  kujua  juu ya taarifa  ambazo  zimesambazwa na mitandao  ya kijamii  kuwa waziri  huyo amefariki  dunia.

Bw Mgimwa  alisema  kaka  yake ni mzima  wa afya  na kwa mujibu  wa madaktari  wanaomtibu anaendelea  vizuri na  kuwa  si kweli hata  kidogo kama amefariki  dunia.

" Ni  kweli  mheshimiwa  waziri wa fedha na mbunge wa jimbo la Kalenga anaumwa  na anaendelea na matibabu hapa  Afrika  ya kusini ....ukweli kwa  sasa anaendelea  vizuri na ninawaomba  watanzania na  wananchi wa  jimbo la Kalenga  kuondoa  hofu ...mbunge  wenu ni mzima kama  kutakuwa na habari  tofauti  tutawaambia pia  tunashukuru  vyombo  vya habari kwa  kufuatilia  suala  hili"

Taarifa  za  kifo  cha waziri Dr Mgimwa  zilivuma  pande mbali mbali za Tanzania  jana
 
jumapili  kiasi cha  kuzua  hali ya  taharuki kwa  wakazi  wa mkoa wa Iringa na  jimbo la Kalenga .

Miongoni mwa  viongozi  walioonyesha kuguswa kwa  uvumi  huo ni pamoja na katibu msaidizi  wa CCM mkoa  wa Iringa Bw  Jimson Mhagama  ambae  hadi  majira ya saa 3 usiku wa kuamkia  jana  alikuwa akifuatilia maeneo mbali mbali ili  kupata  ukweli wa uvumi  huo .

" Hata  mimi  nimesikia kuwa  waziri Dr Mgimwa amefariki  dunia  ila toka majira ya saa 12  jioni jumapili  nilikuwa  nikipiga  simu  huku na kule  ili  kujua ukweli lakini  hadi  sasa saa 3  hii usiku  nimebaini  si kweli   kwani waziri  na mbunge  wetu  ni mzima  wa afya  njema"

Mwandishi  wa habari  hizi  pia  alipata  kuwasiliana na   naibu  waziri  wa maji Dr  Binilith Mahenge ambae  alikuwa njiani   kuelekea  jimboni kwake Makete  pia  alidai  hana taarifa  yoyote  juu ya kifo  cha  waziri mwenzake   huyo.

Dr Mahenge  alisema anatambua  kuwa  waziri  huyo anaumwa  ila hana  taarifa  yoyote  ya  kifo  chake zaidi  ya taarifa  ya  kuumwa  kwake  na kuwa   kama angekuwa amekufa  basi ingefahamika .

Waziri  wa  nchi  ofisi ya  waziri mkuu  sera  na uratibu wa  bunge Bw Wiliam Lukuvi ambae ni mbunge wa  jimbo la Ismani alisema kuwa amepata  kuwasiliana na familia yake kupata  ukweli   juu ya uvumi  huo ila hakuha ukweli  wowote na  kuwa  waziri Dr Mgimwa ni mzima na anaendelea na matibabu.

Mtandao  huu  wa  www.matukiodaima.com na www.francisgodwin.blogspot.com  unawaonya  wale  wote wanaoeneza uvumi wa  kifo cha mpendwa  wetu  kuacha  mara moja kwani  ni  kinyume na mipango ya  Mungu  pia  tunawaomba  watanzania kwa wakati  huu ambao waziri wetu  yupo katika matibabu  kuendelea na jitihada za kumwombea  afya njema  ili arejee salama nchini kwa  kuendelea na jitihada  zake za  kulitumikia  Taifa na  wana kalenga .

Mungu wetu  wa upendo  wanao tunakuomba  umpe  afya  njema  waziri  wetu  mpendwa
MWISHO
Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA