Home » » WANANCHI MANYARA WAASWA KUEPUKA UHARIBIFU WA MAZINGIRA ILI KULINDA HIFADHI YA ZIWA MANYARA

WANANCHI MANYARA WAASWA KUEPUKA UHARIBIFU WA MAZINGIRA ILI KULINDA HIFADHI YA ZIWA MANYARA

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Tuesday, December 10, 2013 | 12:05 AM


Kaimu mkurugenzi wa TANAPA Dr Ezekiel Dembe akijibu maswali ya  wanahabari Iringa ambao wapo ziara ya mafunzo katika hifadhi za kaskazin kwa ajili ya kutangaza pia hifadhi za kusini ikiwemo Ruaha ambayo ni hifadhi  ya kwanza nchini kwa Ukubwa
haya ni madhara  yaliyojitokeza  hifadhi ya  ziwa Manyara  kutokana na wananchi  kulima katika vyanzo  vya maji

Ofisi  mbali  mbali katika  hifadhi ya  Taifa ya Manyara mkoani Arusha  zikiwa  zimekumbwa na mafuliko baada ya mvua kubwa  kunyesha mwezi April mwaka jana.

Wananchi wa wanaozunguka   hifadhi   ya  Taifa ya Ziwa Manyara  mkoani Arusha  wametakiwa  kusaidia  kulinda   hifadhi   hiyo kwa  kuachana na kilimo kisichozingatia  uhifadhi kwa  kulima katika vyanzo  vya maji na milima inayozunguka  hifadhi hiyo.

wito  huo  umetolewa na kaimu mkurugenzi wa TANAPA Dr Ezekiel Dembe leo  wakati akizungumza na  wanahabari mkoa wa Iringa ambao  wapo katika ziara ya mafunzo  ya utalii katika  hifadhi za  kaskazini.

Dr Dembe  alisema  kuwa kuna hatari kubwa ya  ziwa Manyara  kuendelea  kukauka  zaidi kutokana na wananchi wa eneo  hilo kulima katika milima na kupelekea mvua kujaza tope katika ziwa  hilo.

Pia  alisema kutokana na kilimo kisichozingatia uhifadhi wa hifadhi  hiyo hivi  sasa baadhi ya ofisi za hifadhi  hiyo zimeharibika vibaya kutokana na mafuliko na kuna mpango wa Tanapa kutafuta  eneo  jingine ili kujenga ofisi  hizo.

Kuhusu ubovu  wa  miundo  mbinu katika hifadhi za Taifa alisema kuwa  TANAPA  wapo katika mkakati wa  kuendelea  kuboresha miundo mbinu  hiyo ili kuvutia  zaidi watalii wanaofika katika  hifadhi  hizo ambao baadhi yao  wamekuwa  wakitoa maoni kuhusu ubovu huo wa miundo mbinu.

"Lile eneo linalozunguka  hifadhi  ya Manyara  limeendelea  kuharibika  kutokana na kilimo kinachoendelea katika eneo hilo na pia kingine ziwa Manyara hivi  sasa limejaa tope kutokana na kilimo hicho"
 
Akielezea kuhusu hifadhi ya Ruaha Iringa kutangazwa alisema kuwa hivi  sasa mkakati umewekwa wa kuelekeza nguvu ya kuitangaza hifadhi hiyo  ili kuvutia watalii  zaidi  japo alisema  changamoto  kubwa ni upatikanaji wa mafuta  ya Ndege ambazo zinaleta  watalii ambao  hulazimika kujaza mafuta Dodoma .

 Hata  hivyotumeanza mkakati wa kuhakikisha hifadhi ya Katavi na Ruaha katika viwanja wa ndege  vilivyopo  huko kunakuwa na mafuta ya ndege 

Pia   kutafuta  wawekezaji wa kujenga  Hotel za kisasa katika hifadhi ya Ruaha ili kuvutia  watalii wengi zaidi.

Kuhusu  usalama wa watalii alisema kuwa  TANAPA wamejipanga  kuweka usalama mzuri wa watalii ili ni pamoja na kuanzisha ulinzi wa askari  watakaofanya kazi ya kulinda  watalii pekee.

Japo alisema suala la usalama bado ni jukumu  la  watanzania  wote  hivyo ni lazima  kila mmoja  kufanya kazi hiyo.
Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA