Home » » WANAHABARI IRINGA WATUA ARUSHA KUTANGAZA UTALII ,WAJIPANGA KUPANDA MLIMA KILIMNJARO

WANAHABARI IRINGA WATUA ARUSHA KUTANGAZA UTALII ,WAJIPANGA KUPANDA MLIMA KILIMNJARO

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Tuesday, December 3, 2013 | 9:48 PM


Mwanahabari  Anita Boma  akijaza  mafuta katika  gari  lililokuwa likitumiwa na  wanahabari  kutoka Iringa  kwenda Arusha  kufanya  utalii wa ndani
Utigo  wa gari  hilo akisaidiana na mwanahabari Boma  kujaza mafuta
Ni  ziara ya kwenda  kutangaza utalii wa ndani mkoani Arusha
Wanahabari  wa vyombo mbali mbali kutoka  kulia Adoph Mbata  TBC 1,Clement  Sanga Chanel Ten,Mshana Qbra ten Fm na Hakim Mwafongo ,gazeti la Mwananchi kushoto  wa kwanza wakiwa na vijana  wawili wa pili na wa tatu  kushoto ambao  walikuwa  wakiomba msaada wa usafiri baada ya  kudai kunyanyaswa na boss wao
Wanahabari  Iringa ndani ya Arusha
Mwonekano  wa mji  wa Arusha  asubuhi ya  leo
Jiji la Arusha  leo ni jiji  zuri lenye mazingira  bora
JUMLA   ya  wanahabari 16  kutoka vyombo mbali mbali mkoa wa  Iringa  wamewasili  mkoani Arusha usiku  wa jana kwa ajili ya  ziara ya  siku 13  kwa lengo la  kutangaza  vivutio vya utalii hapa nchini.

Mbali ya  kuvitangaza vivutio  hivyo pia  wanahabari  hao  wamejipanga  kupanda  Mlima  Kilimanjaro kama  njia ya kuhamasisha utalii wa ndani  katika mlima  huo.


Ziara  hiyo  ya wanahabari  ilianza Desemba 2 kwa wanahabari  hao  kutoka  mkoani Iringa hadi  Dodoma na jana  usiku  wameingia mjini Arusha  tayari kwa asubuhi ya leo  kuanza  kutembelea  hifadhi ya  Serengeti .

Akizungumzia  ziara  hiyo mwenyekiti wa klabu ya  waandishi  wa habari mkoa wa Iringa Frank Leonard  alisema  kuwa  ziara  hiyo imelenga kujifunza vivutio  vya utalii pamoja na kuwawezesha  wanahabari hao kuvifahamu vivutio vyote  vya utalii kwa  kuvitembelea  ili  pale  wanapoandika habari za uatalii kuwa na uelewa mpana zaidi.

Mbali ya  Serengeti na mlima Kilimanjaro   alitaja   hifadhi nyingine ambazo wanahabari  hao  watatembelea  kuwa ni  Ziwa  Manyara ,Tarangire,Hifadhi ya Arusha ,Mikumi  na Udzungwa mkoani Morogoro kabla ya kurejea  mkoani Iringa.

Alisema  kuwa ziara  hiyo  imeratibiwa na  klabu ya waandishi  wa habari mkoa  wa Iringa (IPC) kwa ufadhili hifadhi za Taifa  Tanzania (TANAPA)

Alisema  kuwa  ziara  hiyo iliyoanza Desemba 2 itamalizika  Desemba 13 mwaka huu kwa wanahabari  hao  kurejea  mkoani Iringa .
Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA