Home » » VYOMBO VYA HABARI ZINAMCHANGO MKUBWA WA KUTANGAZA UTALII WA NDANI - 2

VYOMBO VYA HABARI ZINAMCHANGO MKUBWA WA KUTANGAZA UTALII WA NDANI - 2

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Tuesday, December 17, 2013 | 8:44 AM


Mwanahabari  wa TBC1  Adolph Mbata  akichukua picha  za utalii wa katika mahema ndani ya hifadhi ya Taifa ya Ruaha leo kama  njia ya vyombo  vya habari  kuhamasisha  utalii wa ndani
 Mwanahabari Frank Leonard akijinadikisha katika  kitabu cha  wageni mara baada ya  kuingia lango kuu la hifadhi ya Taifa ya Ruaha jana kulia ni Mawazo Marembeka ,Adolph Mbata na Raymond Francis jumla ya  wanahabari saba akiwemo mzee wa matukio daima walitembelea  hifadhi ya Ruaha jana na leo
 Mtangazaji wa radio Ebony Fm Raymond Francis kushoto akiwa na mzee wa matukio  daima katika daraja la mto Ruaha mkuu katika  hifadhi ya Taifa ya Ruaha jana wakati wa ziara ya  kuhamasisha utalii wa ndani kwa  wanahabari
 Tembo  wa hifadhi ya Taifa ya Ruaha  Iringa akila majani
 Tembo  wa hifadhi  ya Taifa  ya Ruaha wakiwa na watoto  wao
 Mwanahabari Frank  Leonard  akitazama mto  ruaha  mkuu jinsi  ulivyokauka kwa  kukosa maji kutokana na uharibifu wa  vyonzo vya maji unaofanywa na  wananchi  wa nje ya  hifadhi  hiyo
 Mhifadhi  Risala kabongo akiwa na mwanahabari Hakim Mwafongo katikati na Raymond Francis katika  hifadhi ya Ruaha
 Mwanahabari Raymond  Francis akiwa katika hema la kitalii ambapo watalii wengi  hupenda  kulala katika hema kama  hizi
mzee  wa matukio  Daima  akitoka katika moja kati ya hema  za  kitalii katika hifadhi ya taifa  ya Ruaha
MKAKATI  wa  kukuza utalii  wa ndani katika  hifadhi  za  mikoa  ya nyanda za juu ikiwemo hifadhi  ya Taifa  ya  Ruaha ukianza na vyombo  vya  habari  vya  habari nchini  utalii  wa ndani utakuwa kwa kasi na  kuwakomboa  vijana  wengi wasio  na ajira.
 
“Binafsi nashangazwa na vyombo  vya habari  vya utangazaji mkoani Iringa mbali ya kuwa ni moja kati ya mkoa wenye idadi kubwa  ya radio kwa  kufikia idadi  ya vituo vya radio na Runinga zaidi ya 6 ila  bado  sehemu kubwa  ya vituo  hivyo  vya radio  vimekuwa  si msaada wa  kutangaza utalii  wa kusini kutokana na kutenga muda mwingi wa  burudani badala ya kutenga muda wa  kuelezea utajiri mkubwa ambao mkoa wa Iringa unao ambao pia ungewezesha vituo hivyo  kunufaika  utajiri wa vivutio  vya utalii na utalii wa ndani kwa watanzania  hasa wakazi wa mkoa wa Iringa  wenyewe”
 
Kwa  upande  wake Musa Simoni Onesmo   ambae ni  mmoja kati ya  wanachama  wa  chama cha Iringa Masai Market anasema  katika mkoa wa Iringa utalii ndio umeanza kuonekana  miaka  ya hivi karibuni hasa  wakati  wanafanyia  shughuli hiyo   eneo la Posta kabla ya uongozi  wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa  kuwatoa eneo hilo ambalo lilikumbwa na mkasa wa kuungua moto miaka miwili  iliyopita  hivyo wao  kuamua kujibanza eneo la IDYDC  kando  ya  barabara  ya Uhuru kati  ya Iringa – Dodoma .
 
Anasema kuwa  eneo  hilo bado  si la  kuutangaza  utalii  kwani biashara ya vinyago ambayo  wanaifanya inahitaji eneo linaloonekana   vizuri kwa watalii kama eneo la Bustani  ya Manispaa ya  Iringa ama eneo jingine linaloonekana  vizuri  tofauti na hapo  walipo ambapo ni mafichoni  zaidi.
 
Hata  hivyo anasema  kuwa kwa upande wake  ameanza shughuli  hizo  za kuuza vinyago kwa watalii zaidi ya  miaka 10  sasa na hamasa ya kuanza shughuli  hiyo aliipata  kutoka kwa kaka zake ambao  walikuwa wakimtuma shughuli za kuuza vinyango kwa watalii katika mkoa wa Arusha na  sasa ameanzisha  biashara yake  mwenyewe .
 
Huku akidai  kwa mkoa wa Iringa kasi  ya wateja wa bidhaa za kitalii ni ndogo sana ukilinganisha na mikoa ya Kaskazini  japo ni  kubwa kwa  sasa ukilinganisha na miaka ya 2000 na 2010 katika  mkoa  huo  wa Iringa na  kuwa hivi  sasa hata watalii wa ndani ambao  awali  walikuwa  wakipuuza vinyango kwa  sasa  wanafika  kununua bidhaa hizo  za kitali japo  bei wanayouziwa  watalii wa ndani ni chini  na ile ya  watalii wa nje.
 
.............Itaendelea  Kesho......

Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA