Home » » VYOMBO VYA HABARI ZINAMCHANGO MKUBWA WA KUTANGAZA UTALII WA NDANI - 1

VYOMBO VYA HABARI ZINAMCHANGO MKUBWA WA KUTANGAZA UTALII WA NDANI - 1

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Sunday, December 15, 2013 | 6:18 PM

 Aliyekuwa mwenyekiti  wa chama cha  waandishi  wa habari mkoa  wa Iringa marehemu Daudi Mwangosi kulia akiongoza  wanahabari Iringa  kutembelea hifadhi ya Taifa ya Ruaha Iringa  enzi  za uhai  wake

 Wanahabari Iringa  wakika katika  hifadhi ya Taifa ya mlima Kilimanjaro hivi karibuni
 Mwanahabari Daniel Mbega wa Mjengwa Blog kushoto na mzee wa matukio daima na jezi ya Taifa  wakipongezwa na watalii wa nje baada ya kufanikiwa  kupanda mlima  kilimanjaro kwa  kkukimbia hadi  kituo cha Mandara na  kuweka  historia nyingine kwa  kutumia  muda mfupi  zaidi wa saa 1.45 kupanda badala ya masaa 3 na kushuka kwa  dakika 45 badala ya saa 1.30
Na Francis Godwin
MKAKATI  wa  kukuza utalii  wa ndani katika  hifadhi  za  mikoa  ya nyanda za juu ikiwemo hifadhi  ya Taifa  ya  Ruaha ukianza na vyombo  vya  habari  vya  habari nchini  utalii  wa ndani utakuwa kwa kasi na  kuwakomboa  vijana  wengi wasio  na ajira.

Ifahamike  kuwa  utali  ni  sekta mojawapo inayoweza kuwakomboa  wengi  hasa  vijana  wasio na ajira  iwapo  uhamasishaji  utafanyika  katika  vyombo vyetu  vya habari zikiwemo radio  za kijamii ambazo ndizo  zinasikilizwa zaidi  na  vijana  walio wengi ambao  hupenda  kusikiliza radio hizo kutokana na muziki inayopigwa muda  mwingi  zaidi.
 
John Moleli ni  mmoja kati  ya  vijana  ambao  wamepata  kujiajiri wenyewe  katika  sekta  ya utalii kuwatembeza watalii katika maeneo mbali mbali  ya mji  wa Iringa  pindi  wanapofika   kutembelea  hifadhi  ya  Ruaha Iringa na baadhi ya maeneo  ya  vivutio  vya utalii yakiwemo makumbusho  ya chifu Mkwawa  eneo la Kalenga .

Moleli  anasema  kuwa tatizo  la vijana  wengi  kutojiingiza katika shughuli ya utalii  ndani ya  mikoa ya  kusini ni kutokana na  kutokuwa na elimu ya  kutosha  ya utalii   na  wale  wachache ambao  wanafanya shughuli  za kitalii kwa maana ya kuuza vinyago mbali mbali na  kufanya kazi  ya  kuwatembeza  watalii katikati ya  mji  wa Iringa ni  wale  ambao  wametokea  mikoa ya  kaskazini kama Arusha , Kilimanjaro  na  Msoma ambako   sekta  ya  utalii imeonyesha  kuwa  kimbilio  la vijana  wengi.
 
“ Mfano  vyombo  vya habari  vya  mikoa ya kaskazini  vimefanya kazi kubwa  ya kutangaza utalii  na vijana  wengi  kupitia  elimu mbali mbali  inayotolewa na  vyombo hivyo  vya habari  walipata  kuhamasika  na  kupenda shughuli  za kitalii ….japo  jambo  jingine  ambalo limefanya  vijana  wengi wa mikoa ya kaskazini  kuwa na ajira ya uhakika katika  sekta ya utalii ni wao wenyewe  kuupenda utalii  na kujikuta  wengi  wao  badala ya  kushinda vijiweni ama stendi kufanya kazi ya kupiga debe katika  vyombo vya usafiri  kwa kipato kidogo wamekuwa wakielekeza nguvu  zao kupigia debe sekta ya utalii kwa kuuza bidhaa mbali mbali ama kuongoza  watalii“ alisema
 
Kuwa kutokana  na  hesima  kubwa iliyopo  mkoa  wa Iringa  kwa  kuwa na hifadhi  kubwa  kuliko  zote nchini hifadhi ya  Ruaha na kama vyombo  vya  habari na  wanahabari mkoa  wa Iringa  watatumia  vema kalamu zao  kuitangaza hifadhi  hiyo ikiwa ni  pamoja  na kuandaa vipindi vya elimu ya utalii na jinsi ya vijana  mkoani Iringa wanavyoweza kujiajiri  wenyewe katika sekta   hiyo  ni wazi  wageni  wa ndani na nje  watakaofika mkoani Iringa  kutembelea  hifadhi hiyo  watakuwa ni sehemu ya  ajira ya uhakika kwa vijana.
 
“Binafsi nashangazwa na vyombo  vya habari  vya utangazaji mkoani Iringa mbali ya kuwa ni moja kati ya mkoa wenye idadi kubwa  ya radio kwa  kufikia idadi  ya vituo vya radio na Runinga zaidi ya 6 ila  bado  sehemu kubwa  ya vituo  hivyo  vya radio  vimekuwa  si msaada wa  kutangaza utalii  wa kusini kutokana na kutenga muda mwingi wa  burudani badala ya kutenga muda wa  kuelezea utajiri mkubwa ambao mkoa wa Iringa unao ambao pia ungewezesha vituo hivyo  kunufaika  utajiri wa vivutio  vya utalii na utalii wa ndani kwa watanzania  hasa wakazi wa mkoa wa Iringa  wenyewe”
 
..............Itaendelea kesho .......
Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA