Home » » VYOMBO VYA HABARI VINAMCHANGO MKUBWA WA KUTANGAZA UTALII WA NDANI - SEHEMU YA MWISHO

VYOMBO VYA HABARI VINAMCHANGO MKUBWA WA KUTANGAZA UTALII WA NDANI - SEHEMU YA MWISHO

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Wednesday, December 18, 2013 | 12:13 AM Musa Simoni Onesmo   ambae ni  mmoja kati ya  wanachama  wa  chama cha Iringa Masai Market akipanga bidhaa zake za utalii katika eneo lake la kazi
 Eneo  la soko la vinyago mjini Iringa eneo la IDYDC

 Mwenyekiti  wa chama cha waandishi wa habari mkoa  wa Iringa (IPC) Frank Leonard akiwa na mwandishi wa gazeti la Mwananchi Iringa Hakim Mwafongo kulia
 Wanahabari Hakim Mwafongo kushoto na Raymond Francis wakifurahia utalii katika  hifadhi ya Taifa ya Ruaha Iringa wakati wa  ziara ya kiutalii
 Mwanahabari  wa IMTV Rashid Msigwa akichukua matukio katika hifadhi ya taifa ya Ruaha  Iringa katika ziara ya kuhamasisha utalii wa ndani kwa  wanahabari mkoa  wa Iringa
 Ofisa Utalii wa Tanapa wa ofisi ya Utalii Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Bi Risala Kabongo akiwa katika  hifadhi ya Ruaha Iringa
 kaimu  mkurugenzi  wa TANPA Dr Ecekiel Dembe wa pili  kulia akiwa na viongozi mbali mbali wa  serikali na TANAPA  ,pamoja na wakufunzi wa mafunzi ya waongoza  watalii katika hifadhi za Taifa
Makao  makuu ya hifadhi ya Taifa  ya  Ruaha  Iringa  ....................................................
 MKAKATI  wa  kukuza utalii  wa ndani katika  hifadhi  za  mikoa  ya nyanda za juu ikiwemo hifadhi  ya Taifa  ya  Ruaha ukianza na vyombo  vya  habari  vya  habari nchini  utalii  wa ndani utakuwa kwa kasi na  kuwakomboa  vijana  wengi wasio  na ajira.
 
Victor Chakudika ni meneja  wa  kituo cha Radio Nuru Fm  ambacho ni kituo cha radio ya jamii kwa mikoa ya nyanda za juu  kusini anasema  kuwa wao kama radio ya kijamii wameanza kuhamasisha utalii wa ndani na sekta nzima ya utalii katika mkoa  wa Iringa.
 
Chakudika anasema  kuwa wameanzisha  vipindi  mbali mbali vya kijamii  kikiwemo kipindi cha kuhamasisha utalii pamoja na kutoa  elimu kwa wananchi juu ya faida ya utalii ambapo  wamekuwa  wakiwaalika  wadau mbali mbali wa sekta ya  utalii nchini.
 
Mstahiki  meya  wa Halmashauri  ya Manispaa  ya  Iringa Aman Mwamwindi akizungumzia  suala la  ukuzaji utalii  wa ndani  katika Manispaa ya  Iringa amesema  kuwa ushauri  wa  vijana  hao ameupokea japo kwa  sasa eneo hilo la bustani ya Manispaa ya Iringa imechukuliwa na mwekezaji mwingine kwa ajili ya kupatunza  zaidi kwa  kuuza vinywaji  baridi .
 
Kwani anasema  tenda ya  kuendesha eneo hilo ilitangazwa na vijana  hao hawakuomba ila kutokana na mkakati wa  serikali ya mkoa wa Iringa  kuelekeza nguvu katika sekta ya utalii wa ndani na nje Manispaa ya Iringa itafanya mazungumzo  na mwekezaji  wa  eneo  hilo  ili biashara  za bidhaa za kitalii  kuwepo pia eneo hilo.
 
Ofisa Utalii wa Tanapa wa ofisi ya Utalii Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Bi Risala Kabongo anasema  kuwa ofisi yake imeanza mkakati  wa kuhamasisha  utalii wa ndani katika hifadhi za mikoa ya nyanda zakanda ya nyanda za juu  kusini ikiwa ni pamoja na  kukutana na  watoa  huduma mbali mbali  wakiwemo wa mahotel   na kuwapa  elimu ya kuwahudumia  wageni .
 
Kwani  anasema  kuwa  sekta  ya utalii itakuwa zaidi  iwapo watoa huduma  mbali mbali  watakuwa na elimu juu ya huduma  wanazozitoa  kwa  wateja  wao  wakiwemo  watalii
Huku akiwataka  vijana kutumia vema  sekta ya utalii hata kwa kujipanga  kuwatembeza watalii pindi  wanapokuja katika mji wa Iringa kwa ajili ya kwenda katika vivutio vya utalii.
 
Bi Kabongo anasema  kuwa sehemu kubwa ya  watalii wamekuwa  wakitembea wenyewe katika mitaa ya mji wa Iringa  bila ya mwenyeji  jambo ambalo halifai .
 
Kaimu Mkurugenzi wa Mipango na Utalii wa Tanapa, Dk Ezekiel Dembe anasema kuwa idadi  ya  watalii wa ndani na nje wanaotembelea hifadhi ya Ruaha na hifadhi nyingine nchini ni kubwa  zaidi japo lengo  ni kufikisha watalii milioni 2.5 hadi  mwaka 2015.
 
Anasema  kuwa lengo ni kuona idadi ya  watalii  katika hifadhi  inakua  kwa kuzingatia ubora sio ukubwa ili kulinda ikolojia ya maeneo yaliyohifadhiwa
 
Dr Dembe anasema  kuwa kasi  ya  watalii wa nje katika  hifadhi ya Ruaha mbali ya  kuwa inazidi  kuongezeka mwaka  baada ya mwaka  ila  changamoto kubwa ni kutokuwepo kwa mafuta  ya ndege katika  uwanja  wa Nduli Iringa  jambo ambalo  linawalazimu  watalii kujaza mafuta Dodoma kabla ya kwenda Iringa .
 
Hivyo TANAPA inafanya mchakato  wa  kuwatapa  wawekezaji  watakaouza mafuta ya ndege Msembe   katika  hifadhi ya  Ruaha na Katavi pamoja na  kuwapata  wawekezaji watakaowekeza katika  sekta ya Lodge na Hotel katika hifadhi  hizo.
 
 Hifadhi ya Taifa  ya  Ruaha yenye  ukubwa wa kilomita  za mraba 20,226 ni hifadhi kubwa   kuliko zote nchini nay a pili kwa ukubwa katika Afrika baada ya hifadhi ya Kafue nchini Zambia

Sehemu  kubwa ya  watalii wa nje na  wandani  hupenda kutembelea  hifadhi  hii kutokana na kuwa na umaarufu wa wanyama aina ya kudu  wakubwa na wadogo ambao hupatikana kwa  wingi katika hifadhi  hii  huku  ustawi wa hifadhi hii ukitegemea  mto   Ruaha mkuu.
 
Mandhari ya hifadhi ya Ruaha ni mazuri kwa watalii wa ndani na  watalii wa nje na hifadhi  hii  inafikika  vizuri  kutokana na miundo mbinu yake mizuri .
 
Hifadhi  ya  Ruaha  ipo katikati ya Tanzania umbai  wa kilomita 128 Magharibi mwa mji wa Iringa na inafikika pia kwa usafiri  kwa ndege  za kukodi  huku magari  hufika  wakati wote wa  mwaka  kutoka Dar es Salaam ni kilomita 625,Mikumi , Iringa na Arusha  kwa  kupitia Dodoma.
 
Mbali  ya hifadhi ya Ruaha Iringa Tanzania tunajivunia kwa kuwa na hifadhi kama Serengeti  Udzungwa ,Mlima Kilimanjaro, Tarangire, Manyara, Arusha, Mkomazi, Mikumi,, Katavi, Kitulo,  pamoja na  vivutio vingine  kwa mkoa wa Iringa kama kisima  cha  Mkwawa ,maskani ya  watu wa kale  katika  kijiji  cha Ismila  umbali wa kilomita 120 kutoka Iringa mjini na vivutio vingine vingi 
  Mwa maoni na ushauri piga 0754 026 299
MWISHO

Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA