Home » » MWANDISHI ALIYEJITOSA KUPIGA PICHA NA TWIGA WA SERENGETI KAMA NJIA YAKUTANGAZA UTALII

MWANDISHI ALIYEJITOSA KUPIGA PICHA NA TWIGA WA SERENGETI KAMA NJIA YAKUTANGAZA UTALII

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Saturday, December 7, 2013 | 9:53 AM


Mwanahabari  wa  kituo cha radio Nuru Fm Iringa Victor Meena  akimvizia  Twiga kwa ajili ya kupiga  picha ya pamoja katika  hifadhi ya serengeti  leo wakati wa ziara ya wanahabari mkoa wa Iringa

Mwanahabari  huyo hapa akichukua  picha ya kumbukumbu katika kamera  yake kabla ya kupiga  picha ya pamoja na Twiga wa  Serengeti  leo
Hapa akipiga  picha  na Twiga  kulia katika   hifadhi ya Serengeti  hifadhi  inayoongoza  kwa  kuwa na idadi kubwa zaidi ya  wanyama pamoja na Nyumbu kuliko hifadhi zote nchi 

 IMEELEZWA kuwa siasa za vurugu vinazoendeshwa na baadhi ya vyama vya siasa katika mikoa ya kaskazin zimeendelea kushusha idadi ya watalii katika hifadhi za kaskazin. 

Kauli hiyo imetolewa leo na mhifadhi mkuu wa hifadhi ya Serengeti mkoani mara Bw Wiliam Mwakilema wakati akizungumza na timu ya wanahabari 16 kutoka mkoa wa Iringa ambao wametembelea hifadhi ya Taifa ya Serengeti kwa ajili ya kujifunza na kutangaza zaidi vivutio vya utalii 

Mwakilema alisema kuwa moja kati ya mambo yanayokwamisha watalii kufika katika hifadhi ni pamoja na wanasiasa kuendesha siasa za vurugu ambazo zinawatisha watalii hao ambao wengi wanapenda maeneo yasiyo ya vurugu kwa ajili ya kutembelea. 

Bila kuvitaja vyama ama wanasiasa wanaofanya siasa za vurugu Mwakilema aliwataka wanahabari na vyombo vya habari nchini kuendelea kutoa elimu zaidi kwa vyama vya siasa na wanasiasa ili kuepuka kuendesha siasa za vurugu. 

Wakati huo huo Mwakilema alikanusha upotoshwaji unaofanywa na nchi ya Kenya juu ya wanyama aina ya Nyumbu kuwa ni wanyama ambao wanapatikana kenya na kuwa wanyama hao si raia wa Kenya ni wanyama wenye uraia wa Tanzania ambao Kenya wamekuwa wakifika kwa msimu kwa ajili ya malisho na baada ya hapo huzaliana katika hifadhi hiyo ya Serengeti .
Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA