Home » » MTANGAZAJI WA KIPINDI CHA MBONI SHOW KULISHA YATIMA IRINGA

MTANGAZAJI WA KIPINDI CHA MBONI SHOW KULISHA YATIMA IRINGA

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Monday, December 23, 2013 | 5:03 AM


Mtangazaji  maarufu  wa kipindi cha Mboni Show kinachorushwa na  kituo  EATV  Bi Mboni A .Masimba anataraji  kula  sikukuu ya Krismas na mwaka  mpya  na  watoto   yatima mkoani Iringa .
 
 Akizungumza na mtandao  huu wa www.francisgodwin.blogspot.com ,Mboni amesema  kuwa akiwa kama mtanzania na mwanahabari ameamua  kuandaa chakula  cha  pamoja  na  watoto  yatima  wa  vituo  vitatu vya mkoa wa  Iringa .
 
Alisema  kuwa  hafla  hiyo  ya  kula  chakula na yatima  itafanyika  siku  ya Desemba 25 mwaka  huu ambayo  itakuwa ni sikukuu ya Krismas .
 
Bi Mboni  alisema  kuwa  mbali ya  kuendesha  vipindi  vyake  katika kipindi  chake cha  Mboni Show bado ameguswa  kula pamoja na  watoto  hao 230  pamoja na wageni  mbali mbali  watakaofikisha idadi  ya watu 300.
 
Alisema  kuwa  hafla  hiyo  itafanyika katika ukumbi wa Hihglands mjini  Iringa  na  kuwa  vituo ambavyo vimealikwa ni pamoja na TOSAMAGANGA , Upendo Centre  Sabasaba na YATIMA MOYO KWA MOYO  kilichopo Mufindi kata ya  Bumilayinga

Hata  hivyo  alisema mbali ya  chakula  hicho   pia  watoto  hao  yatima  watapata  zawadi mbali mbali  kutoka kwake.
 
Mboni  amesema  kuwa  amekuwa  bega kwa bega na watoto  yatima  na  kuwa mbali  ya kula na  watoto  hao pia  amekuwa akifanya  hivyo wakati  wa sherehe  za Ramadhan pia  kutokana na kipindi  chake  kutazamwa na  watanzania  wote .
 
Hivyo  alisema  lengo  kuu ni kuwakumbusha  watanzania  juu ya  kuwakumbuka  watoto  yatima  kama  ambavyo  wamekuwa  wakichangia sherehe mbali mbali .
 
Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA