Home » » GEOFREY MUNGAI ATOA ZAWADI ZA TSH MILIONI 2.5 KWA YATIMA WA KITUO CHA DBL KWA AJILI YA KRISMAS NA MWAKA MPYA

GEOFREY MUNGAI ATOA ZAWADI ZA TSH MILIONI 2.5 KWA YATIMA WA KITUO CHA DBL KWA AJILI YA KRISMAS NA MWAKA MPYA

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Monday, December 23, 2013 | 5:04 AM


Bw Mungai  akizungumza na mlezi  wa  kituo  hicho  cha DBL Mchungaji Neema Mwaisumbi mara  baada ya  hafla  hiyo
Mmiliki wa  Hotel ya M.R Bw  Luvinga  akipongeza jitihada za Bw Mungia  katika  kusaidia yatima  hao ,kulia  kwake ni mchungaji Mpeli Mwaisumbi ,Bw  Mungai , Dr Gabon na mkewe
Mmoja kati ya  wazee  waliosaidia  kusomeshewa  watoto na Geofrey Mungai kulia akipongeza kwa msaada   wake
Maombi  maalum  ya kuombea  kituo cha DBL
Wadua  mbali mbali  wakiwa katika maombi maalum
 
 Mkandarasi  Geofrey  Mungai  kushoto  akila  chakula  na  watoto  yatima  wa  kituo  cha DBL mkimbizi  sanjari na mganga Oscar Gabone  kulia.
 ................................................................................................................
MKANDARASI  Geofrey  Mungai  ametoa zawadi   mbali mbali  za krismas na  mwaka  mpya  kwa kituo cha  watoto yatima cha  Daily Bread Life Tanzania  (DBL) zawadi  zenye  thamani ya zaidi ya Tsh milioni 2.5 huku  akiwataka  makandarasi wenzake na watanzania  kujenga  utamaduni  wa  kuchangia  yatima  badala ya  kuchangia sherehe kama harusi.


Mungai alitoa  msaada huo jana  kwa  uongozi  wa  kituo hicho pamoja na kuwaandalia chakula  cha pamoja   watoto  hao  39  na  wananchi mbali mbali wa mji  wa Iringa kama njia ya  kuwahamasisha  kusaidia yatima .

Akizungumza  mara  baada ya  kukabidhi  msaada  huo Mungai  alisema  kuwa imekuwa ni kawaida  yake  kwa  kila mwaka katika msimu  wa  sikukuu ya Krismas na mwaka  mpya  kufika katika  kituo hicho na  kuwapa msaada  watoto  hao  ili nao  kuungana na  watoto  wenye  wazazi  wao kufurahia sikukuu hizo.

Hata  hivyo  alisema  kuwa jamii ya  mkoa  wa Iringa na  watanzania  kwa ujumla wanapaswa  kubadilika kwa  kuelekeza  michango  yao  kwa  watoto  yatima ambao baada ya  kupoteza  wazazi  wao  faraja ya  pekee  wanaisubiri  kutoka kwa  jamii inayowazunguka.

Aidha  alisema  kuwa  yeye  kama mmoja kati  ya makandarasi mkoa  wa Iringa anaendelea  kufanya mazungumzo  na wenzake  ili  kuweka  mpango wa  kuendelea  kutembelea  vituo  vya yatima kila mwaka  kwa  ajili  ya kuwasaidia misaada  mbali mbali.
 
Alisema  kuwa  upo uwezekano mkubwa wa  watoto  hao yatima  kuendelea   kusaidia  iwapo watanzania na wadau  mbali mbali  wakiwemo makandarasi  wenzake  kuwekeza kwa  watoto hao.

Kwa  upande  wake  mkurugenzi mtendaji  wa  kituo  hicho  mchungaji Mpeli Mwaisumbi mbali ya  kumpongeza  Mungai kwa  kuendelea  kusaidia  watoto  hao  bado  alisema  wengine  ambao  wamepata  kufika  kusaidia  watoto  hao  ni pamoja na mwenyekiti  wa CCM mkoa  wa Iringa Jesca  Msambatavangu, taasisi  ya kuzuia na kupambana na rushwa nchini (TAKUKURU) mkoa  wa Iringa ,mamlaka ya mapato  Tanzania (TRA) mkoa  wa Iringa , mbunge wa  viti maalum mkoa wa Iringa Rita Kabati (CCM) na blogu ya Francis Godwin.

Mchungaji Mpeli  alisema  kuwa Mungai  na Msambatavangu  wamekuwa ni msaada  mkubwa wa  kituo hicho na kuwa karibu miaka  yote  wamekuwa wakifika  kusaidia  watoto  hao misaada mbali mbali ikiwemo  ya  elimu .

 Alisema  kuwa  kituo  hicho kinafanya kazi  chini  ya  shirika  lisilo la kiserikali  ya Daily Bread  Life  Tanzania lililosajiliwa  kwa  usajili  12903 chini ya  wizara ya mambo ya ndani ya  nchi pia   kituo  kimesajiliwa na ustawi  wa jamii kwa  kupewa usajili wa makao  ya  watoto namba 00049995.

Hata  hivyo  alisema  kuwa  kituo  kilianza  kupokea  watoto  14 mwaka  2004 na  sasa  kuna  watoto 37 waliopo  kituoni  hapo  na  kuwa  toka  kituo  kianzishwe  jumla  ya  watoto 51 wamelelewa  hapo

Alisema  kutokana na misaada wa  wadau mbali mbali kituo kimeendelea  kupata  mafanikio makubwa kama  kuwa na  shamba  ,basi  moja ,mradi  wa cherehani pia  kuanza mchakato  wa kukamilisha  shule  ya  sekondari ambayo inajengwa  umbali  wa kilomita 6  kutoka mjini Iringa kwa  lengo kuwawezesha  watoto  hao kupata  elimu ya  sekondari.

Pia  alisema changamoto  kubwa katika  uendeshaji wa  kituo hicho ni michango mingi katika shule za msingi ambako  watoto  hao  wanasoma ,kukosa  ruzuku toka  serikalini na  changamoto  nyingine  nyingi.

Wakati  huo  huo   Mchungaji  Mpeli  amempongeza  Rais   Dr  Jakaya  Kikwete  kwa utendaji  mzuri  ikiwa ni  pamoja na  kutengua uteuzi  wa mawaziri  wanne ambao wizara  zao  zilionyesha  kunyoshewa  vidole na  wabunge.

Alisema   kuwa uamuzi  uliochukuliwa na rais ni uamuzi ambao  unapaswa  kupongezwa na  kila mtanzania mpenda maendeleo na amani  ya nchi na kuwataka  viongozi  wenzake wa dini  kuelekeza sara na dua  zao kumwombea  Rais Kikwete na  serikali  yake  kuendelea  kuwahudumia  vema  watanzania.

Mchungaji Mpeli  aliwaomba  watanzania  na  wadau mbali mbali pale  walipo  iwapo  wanahitaji kusaidia  kituo hicho  kutuma  michango  yao kupitia akaunti namba Benk ya Exim ni 5435526007  Daily Bread  Life Childreans home ,ama  kwa njia ya M-PESA  0754362536
MWISHO
Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA