Home » » AIRTEL , BARAZA LA USALAMA BARABARANI KUHAMASISHA USALAMA WAKATI HUU WA SIKUKUU

AIRTEL , BARAZA LA USALAMA BARABARANI KUHAMASISHA USALAMA WAKATI HUU WA SIKUKUU

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Monday, December 23, 2013 | 5:03 AM


 Balozi wa kampeni za Usalama barabarani, Bw. Athumani Hamisi akizungumzia athari zinazotokana na ajali za barabarani na kuwaasa wananchi waziepuke hususani katika msimu huu wa sikukuu.
Meneja wa huduma za kijamii wa Airtel Tanzania, Hawa Bayumi (kulia) akisisitiza juu ya umuhimu wa wananchi kujikinga na ajali za barabarani kwenye msimu huu wa sikukuu leo wakati wa kikao na waandishi wa habari kilichofanyika makao makuu ya Airtel jijini Dar es salaam.  Katikati ni Katibu Mtendaji wa Baraza na Kamanda mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani cha Tanzania, DCP Mohammed Mpinga akifuatiwa na Balozi wa kampeni za Usalama barabarani, Bw. Athumani Hamisi.


Katibu Mtendaji wa Baraza na Kamanda mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani cha Tanzania, DCP Mohammed Mpinga akisisitiza juu ya utii wa sheria bila shuruti katika msimu huu wa sikukuu kushoto kwake ni . Kushoto kwake ni Balozi wa kampeni za Usalama barabarani, Bw. Athumani Hamisi


Dar es Salaam, Disemba 23, 2013 Kampuni ya mitandao wa simu za mkononi ya Airtel Tanzania imeendeleza ushirikiano wake na Baraza la Taifa la Usalama barabarani katika juhudi za kuelimisha uma kuzingatia sheria na kanuni za usalama barabarani hususani msimu huu wa sikukuu.
Airtel imekuwa ikishirikiana kwa karibu na kikosi cha Usalama Barabarani katika kutoa elimu ya usalama barabarani kwa kudhamini kampeni mbalimbali. 
Akizungumza kwa niaba ya Kampuni hiyo, Meneja wa huduma za kijamii wa Airtel Tanzania, Hawa Bayumi alisema kipindi hiki cha mwisho wa mwaka wananchi wanapaswa kuwa waangalifu zaidi ili kujikinga na ajali za barabarani.
“Hiki ni kipindi ambacho wananchi wanapaswa kuwa makini sana katika kuhakikisha wanajilinda na wimbi la ajali za barabarani ambazo husababisha asara kubwa kwa taifa, na pia madereva wajitaidi sana kuepuka ulevi wa kupindukia,” alisema Hawa.
Aliongeza kwa kusema pia katika msimu huu wateja wa Airtel wanaweza kutumia huduma ya Airtel money kutuma na kupokea pesa bure mahali popote nchi nzima kuepuka kutembea na viwango vikubwa vya pesa.
Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Baraza na Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani cha Tanzania, DCP Mohammed Mpinga alisema Lengo la kampeni hizi ni kupunguza ongezeko la ajali za barabarani pamoja na madhara yake kwa kipindi cha sikukuu za mwaka huu 2013/2014 na wanajitaidi kuhakikisha elimu inatolewa ipasavyo.  
“Tunashukuru Airtel kwa kuungana nasi katika kujali usalama wa watanzania, kazi ya  kuelimisha watumiaji wa barabara ni kubwa na hivyo tunaendelea kutoa wito kwa wadau wengine kutuunga mkono ili kusaidia kufikisha ujumbe. Lengo hili litatimia kwa kushirikiana na wadau katika kufanya operasheni mbalimbali pamoja na kutoa elimu.” Alisema DCP Mpinga.
Mpinga alitumia nafasi hiyo kuwaasa watanzania wote kote nchini kuepuka kusafiri na kiwango kikubwa cha fedha badala yake watumie huduma ya Airtel Money kutuma, kuweka na kutoa pesa.
Akizungumza kwa upande wake Balozi wa kampeni hizi za Usalama barabarani ambaye pia ni muhanga wa ajali za barabarani, Bw. Athumani Hamisi alisema Kuelekea mwisho wa mwaka, matukio ya ajali za barabarani yamekuwa yakiongezeka kutokana na ukiukwaji wa sheria, kanuni na taratibu za usalama barabarani hivyo wananchi wanatakiwa kujitahidi kutokiuka taratibu hizo.
“Ukiukwaji wa sheria husababisha sana ajali za barabarani, wananchi wanapaswa kuhakikisha wanafuata sheria za barabarani ili kuepusha ongezeko la ajali hizo ambazo hutokea mara kwa mara haswa katika msimu huu wa sikukuu.” Alisema Athmani.
Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA