Home » » WAZAZI WA WANAFUNZI WANAOSOMA SOUTHERN HIGLANDS MAFINGA KUKUTANA KESHO JUMAMOSI

WAZAZI WA WANAFUNZI WANAOSOMA SOUTHERN HIGLANDS MAFINGA KUKUTANA KESHO JUMAMOSI

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Thursday, November 28, 2013 | 11:15 PM

 Baadhi ya  wanafunzi  wanaosoma  shule  ya  kimataifa ya  Southern Highlands Mafinga ,chini na  baadhi  ya  wazazi  wa wanafunzi hao

WAKATI  uongozi  wa  shule  ya  kimatiafa ya  Southern Highlands Mafinga  mkoani  Iringa  ukiwa na uhakika  mkubwa wa  wanafunzi  waliofanya mtihani  wa Taifa  wa darasa la saba mwaka  huu  kufaulu wote ,kesho jumamosi  shule  hiyo  imewaita  wazazi  wa wanafunzi hao  na  wengine wote wanaoendelea  kusoma  shuleni hapo.

Mwenyekiti wa bodi ya shule ya hiyo  ya Southern Highlands Mafinga Kitova Mungai alimweleza mwandishi  wa habari hizi  kuwa lengo  la  kuwaita  wazazi hao  ni kuweza  kujadiliana mambo mbali mbali ya kimaendeleo  katika shule  hiyo.

Alisema  kuwa  shule   hiyo  imekuwa na utaratibu  wa  kukutana na wazazi   wanaosomesha  watoto   wao  katika  shule  hiyo  kila mwaka kwa ajili ya kupokea  changamoto mbali mbali kama  njia ya  kuboresha  elimu  shuleni  hapo.

Kwani  alisema  kuwa kimsingi  kiwango  cha taalum shuleni  hapo kipo  juu na kuwa  hata   mwaka  mmoja shule  hiyo haijapata  kufelisha hata  mwanafunzi mmoja.

Bw  Mungai  alisema kuwa  kikao hicho  cha pamoja kati ya  wazazi na  uongozi  wa  shule  hiyo kitafanyika  kuanzia majira ya saa 2 asubuhi hadi saa 7 mchana  katika ukumbi wa  shule  hiyo.

Kwa  upande wake mkurugenzi mtendaji wa Southern Highlands Mafinga Bi Mary Mungai  aliwataka  wazazi kujitokeza kwa wingi katika kikao  hicho ikiwa ni pamoja na kupongeza benk ya wananchi Mufindi (MUCOBA) kwa jitihada mbali mbali  za kuunga mkono jitihada za elimu shuleni hapo kiasi cha kujitolea kiasi cha Tsh milioni 2.5 kwa ajili ya kuwafuingulia akaunti katika benk hiyo wanafunzi watakaofanya vema katika matokeo ya mtihani huo mwaka huu

Bi Mungai  alisema  kuwa  kuwa msaada huo wa MUCOBA ni heshima kubwa kwa shule yake na kuwa ni chachu ya shule hiyo kuendelea kufanya vema zaidi ili kuwavuta wahisani wa ndani na nje kuendelea kuiunga mkono shule hiyo.

Alisema MUCOBA hawajakosea kuunga mkono jitihada za elimu katika shule hiyo kwani kweli ni shule inayotoa elimu bora na toka ilipoanzishwa zaidi ya miaka 13 iliyopita shule hiyo haijapata kufelisha mwanafunzi hata mmoja.

Hata  hivyo baadhi  ya  wazazi  wanaosomesha  watoto  wao katika  shule  hiyo  wameendelea  kupongeza   jitihada zinazofanywa na shule hiyo kwa  kuendelea  kufanya  vema katika mitihani ya taifa na kuwa imani kubwa ya  wazazi ni kuona  shule hiyo inaendelea  kuwa shule  bora  mkoa wa Iringa na Tanzania kwa ujumla .
Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA