Home » » TRA MKOA WA IRINGA YAKABILIWA NA CHANGAMOTO MBALIMBALI KATIKA UKUSANYAJI MAPATO

TRA MKOA WA IRINGA YAKABILIWA NA CHANGAMOTO MBALIMBALI KATIKA UKUSANYAJI MAPATO

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Tuesday, November 5, 2013 | 5:46 AM

Meneja wa Mamlaka ya Mapato Mkoa wa Iringa Rosalia Mwenda akitoa taarifa kwa vyombo vya habari ofisini kwake leo.Waandishi wa habari wakimsikiliza meneja wa Mamlaka ya Mapato (TRA) ofisini kwake leo.
 ================================================
Na Gustav Chahe
MAMLAKA ya Mapato (TRA) Mkoa wa Iringa inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ya wafanyabiashara waliosajiliwa kwenye kodi ya ongezeko la thamani kutokutumia ipasavyo mashine za kielekitroniki za kutolea risiti.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake leo, Meneja wa TRA Mkoa wa Iringa Rosalia Mwenda alisema wapo baadhi ya wafanyuabiashara wasiowaadilifu ambao hawatumii mashine za kutolea risiti ipasavyi na kuiingizia serikali hasara.
Ametaja changamoto nyingine kuwa ni pamoja na kutotoa na kudai risiti wakati wa kuuza na kununua bidhaa au huduma mbalimbali.
“Pia kuna changamoto nyingine ambazo zinatokana na kuingia kwa bidhaa zilizopigwa marufuku kama vipodozi, pombe aina ya “power one”, double puch na bidhaa nyingine kama sukari kuingizwa hapa nchini kwa njia za magendo pamoja na mwitikio mdogo wa wafanyabiashara wa kununua na kutumia mashine za kielektroniki” amesema Mwenda.
Ili kukabilia na changamoto hizo, wamepanga mikakati ya kutoa elimu ya kodi itakayochangia katika kukuza uwajibikaji wa hiari wa kulipa kodi, kupanua wigo wa kodi ili kuweza kuongeza vyanzo vipya vya mapato vitakavyosaidia kuvuka lengo walilopangiwa na serikali.
Amesema wanafuatilia kwa ukaribu matumizi ya mashine za kielekitroniki za kutolea risiti kwa wafanyabiashara wote waliosajiliwa na kodi ya ongezeko la thamani na kuhakikisha wanazitumia vilivyo, kuzuia ukwepaji wa kodi katika sekta rasmi na isiyo rasmi kwa kutokutoa risiti wakati wa kuuza na kwa ununua bidhaa au huduma mbalimbali pamoja na kuzuia bidhaa zilizopigwa marufuku zisiingizwe nchini kwa njia za magendo.
“Tumejipanga kukuza na kusimamia maadili mema ya wafanyabiashara katika kufanya kazi kwa mujibu wa sheria na taratibu za ajira na kuendelea kutkeleza mpango mkakati wa miaka mitano wa nne ulioanza 2013/2014 na na ambao utafikia mwisho wake 2017/2018” amesema.
Amesema katika utekelezaji wa mipango hiyo ni kujenga uwajibikaji wa hiari na wa hali ya juu wa kulipa kodi ambapo ambapo mamlaka lazima ijenge uwezo mkubwa wa kusimamia sheria za kodi, uwezo wa kudhibiti ukwepaji kodi na utendaji unaozingatia uadilifu wa hali ya juu wa wafanyabiashara wa Mamlaka ya Mapato Tanzania.
Mamlaka ya Mapato Tanzania imeanza kuadhimisha siku ya mlipa kodi Novemba 2 ambapo kilele chake kinatarajiwa kufikia Novemba 8 Mwaka huu.
Katika maadhimisho ambayo ni ya saba tangu kuanzishwa kwake Oktoba 2006, ni kutambua mchango wa walipakodi na kuwatunuku walipakodi ambao wapo mstari wa mbele katika kuweka kumbukumbu zao za biashara kwa usahihi, wanaolipa kodi zinazolingana na biashara zao, wanaojituma kulipa kodi kwa muda unaostahili kisheria na wale wanaolipa kodi zao kwa hiari ambapo jumla ya wafanyabiashara 24 watatunukiwa vyeti kwa kufanya biashara zao kiutaalam.
Mwenda amesema katika maadhimisho hayo ambayo kaulimbiu yake ni “tulipe kodi kwa matokeo makubwa sasa” yataisaidia jamii umuhimu wa ulipaji kodi kwa matokeo  makubwa, kupata mrejesho kutoka kwa walipakodi na wateja wengine kwa ujumla kama juu ya huduma zitolewazo na mamlaka hiyo zinaridhisha na kwamba zina ubora pamoja na kuwakumbusha walipakodi haki na wajibu wao katika ulipaji wa kodi.
Mamlaka ya Mapato Mkoa wa Iringa kwa mwaka wa fedha 2012/2013 imekusanya jumla ya shilingi 29,271,160,861.55 sawa na asilimia tisini (90%) ya utendaji ikiwa walipangiwa kukusanya jumla ya shilingi 32,650,500,000.00/=.
Lengo la Idara ya Ushuru wa Forodha lilikuwa shilingi 302,500,000/= na lengo la Idara ya Kodi za Ndani lilikuwa shilingi 32,348,000,0000/= ambapo kwa makusanyo hayo ya zaidi ya 29 Bilioni yaliyokusanywa, yanaonesha ukuaji wa mapato ya shilingi 4,540,408,676 ukilinganisha na makusanyo ya shilingi 24,730,752,185.00 ya mwaka 2011/2012.
Kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku ya mlipakodi kitakachofanyika Novemba 8, mwaka huu kitakachofanyika katika ukumbi wa Highlands, Mamlaka ya Mapato Mkoa wa Iringa imetoa msaada wa shilingi 700,000/= katika kituo cha kulelea watoto yatima cha Daily Bread Life.
Kipindi cha miaka 16 iliyopita TRA Mkoa wa Iringa imekuwa ikipanda na kushuka katika ukusanyaji kodi kutokana na changamoto mbalimbali.
Hata hivyo takwimu zinaonesha katika kipindi hicho, jumla ya watu 6,665 walitembelea ofisi za TRA kwa masuala ya yanayohusu kodi.
Licha ya changangamoto zinazoikabili Mamlaka ya Mapato Mkoa wa Iringa kwa kipindi cha miaka 16 iliyopita ukusanywaji wa kodi umebainishwa ambapo mwaka huu (2012/2013 unaonekana kutekelezwa kwa asilimia 90 tofauti na kwaka 2011/2012 uliotekelezwa kwa asilimia 105.
Mwaka 2010/2011 ukusanywaji wa kodi ulitekelezwa kwa asilimia 87 chini ya mwaka 2009/2010 uliotekelezwa kwa asilimia 105, mwaka 2008/2009 ulitekelezwa kwa asilimia 110 wakati mwaka 2007/2008 ulitekelezwa kwa asilimia 106.
Mwaka 2006/2007 ulitekelezwa kwa asilimia 139 wakati mwaka 2005/2006 ulitekelezwa kwa asilimia 103 ambapo mwaka 2004/2005 ulitekelezwa kwa asilimia 107 wakati mwaka 2003/2004 ulitekelezwa kwa asilimia 102.

Mwaka 2002/2003 ulitekelezwa kwa asilimia 102 huku mwaka 2001/2002 ukitekelezwa kwa asilimia 104, mwaka 2000/2001 ukitekelezwa kwa asilimia 83, mwaka 1999/2000 ulitekelezwa kwa asilimia 86 na mwaka 1998/1999 ukitekelezwa kwa asilimia 112, mwaka 1997/1998 ulitekelezwa kwa asilimia 106.
Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA