Home » » SHULE YA KIMATAIFA YA SOUTHERN HIGHLANDS MAFINDA YAZIDI KUJIWEKEA REKODI NZURI

SHULE YA KIMATAIFA YA SOUTHERN HIGHLANDS MAFINDA YAZIDI KUJIWEKEA REKODI NZURI

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Wednesday, November 13, 2013 | 6:12 AM


Mkurugenzi  mtendaji  wa shule ya  kimataifa ya Southern Highlands Bi mary Mungai akimpongeza mmoja kati ya  wahitimu wa darasa la saba mwaka huu 
............................................. 
 
Shule ya Southern Highlands School ya mjini Mafinga, mkoani Iringa, imeendeleza record yake nzuri ya kufaulisha vizuri wanafunzi wote darasa la saba tangu ilipoanzishwa mwaka 1997.

Shule hii yenye kufundisha kwa kiingereze, yaani english medium school, imefaulisha tena wahitimu wote wa darasa la saba na kuiwezesha kuwa katika asilimia mbili (2%) ya juu ya shule zote zenye kufaulisha vizuri kitaifa, na katika 10 bora kati ya shule 449 za mkoani Iringa.

Tunawapa hongera wahitimu hao na kuwatakia maendeleo mazuri kokote waendako. Pia tunawapongeza wazazi/walezi, tunawatakia kila la heri kuwaendeleza watoto wao kufuatia msingi huu ulio bora waliopata kutoka Southern Highlands School.

Bila kusahau walimu, tunawapa pongezi sana walimu kwa kazi kubwa wanayoendelea kuifanya kila siku kuhakikisha wanafunzi wanapata elimu iliyo ya kiwango cha juu.

Kwa watakaopenda watoto wao wajiunge na Southern Highlands School, nafasi zipo kwa wanafunzi wa chekechea, darasa la 1, 2, 3, na 5 kwa wanafunzi wote na darasa la 4 na la 6 kwa wanaotoka shule za english medium.

Mawasiliano ya shule ni kama ifuatavyo:
Anwani yetu ni:  P.O.Box 34, MAFINGA.
Simu No:    (026)  2772661 Office,   Tel/fax (026)  2772544.
– 0754651966        – 0754209251       - 0756721040             - 0752840884           

Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA