Home » » SAKATA YA MASHINE ZA EFD WAFANYABIASHARA IRINGA WAANZA KUFUNGA MADUKA YAO

SAKATA YA MASHINE ZA EFD WAFANYABIASHARA IRINGA WAANZA KUFUNGA MADUKA YAO

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Tuesday, November 26, 2013 | 5:38 AM


 Hili  ni  duka  lililopo eneo la Miyomboni  jirani na barabara  ya  kuelekea ofisi za CCM mkoa  ambalo kwa  sasa  limefungwa na mali zote   kujumlishwa kama  hatua ya  kupinga maamuzi ya TRA kutaka  wafanyabiashara  kuwa na mashine za EFD

 Hili  ndilo  duka  lililofungwa kama  linavyoonekana kwa nje
 Haya ni maduka  mawili  yaliyofungwa eneo la Hazina Ndogo mjini IringaUAMUZI  wa mamalaka ya mapato   Tanzania (TRA) kutaka wafanyabiashara  kununua mashine  za mashine za kielektroniki kwa ajili ya kukatia risiti za wateja pindi wanapowauzia bidhaa( EFD) umezidi kupingwa na  wafanyabiashara mkoani Iringa .
 
Uchunguzi  wa mtandao  huu  wa www.francisgodwin.blogspot.com umebaini kuwepo kwa baadhi ya maduku kufungwa  kama njia ya  kupinga uamuzi huo  wa TRA  kuwataka  kuwa na mashine  hizo.
Sehemu  kubwa ya  wafanyabiashara  wamefunga maduka  yao huku  baadhi yao wakijumlisha mali  zao  zote na kuamua  kuachana na biashara ambazo walikuwa  wakizifanya awali.
Alex Oswald, kwa niaba ya wenzake alisema kuwa wao waliamua kufunga maduka kwa hiari yao na kwamba lengo la mkutano lilikuwa kutoa msimamo wa kuiomba serikali itoe mashine hizo bure.
Hata  hivyo wafanyabiashara  hao  walisema kuwa kimsingi wao hawajagoma kutumia mashine hizo bali wanataka wawekewe bure, kwani si kila mfanyabiashara anaweza kuinunua mashine hiyo ambayo kwa sasa inauzwa kwa sh 800,000.
Hivyo  walisema  kuwa  wameamua  kurudisha  nyumba kwa  wenye vyumba   hizo  ili kuachana kabisa na biashara  hiyo  ya maduka  kutokana na kushindwa  kununua mashine  hiyo.

Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA