Home » » MFUKO WA BIMA YA AFYA WATOA MSAADA WA MASHUKA HOSPITALI YA MANISPAA YA IRINGA , MWENYEKITI WA BODI ATOA ONYO KALI KWA WANAOGUSHI MADAI

MFUKO WA BIMA YA AFYA WATOA MSAADA WA MASHUKA HOSPITALI YA MANISPAA YA IRINGA , MWENYEKITI WA BODI ATOA ONYO KALI KWA WANAOGUSHI MADAI

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Tuesday, November 5, 2013 | 8:54 AMMwenyekiti wBodi ya Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF), Balozi Ally Mchumo akimkabidhi mashuka kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya manispaa Immaculata Sanje kwa ajili ya Hospitali ya Halmashauri ya  Manispaa ya  Iringa iliyopo  Frelimo makabidhiano yaliyofanyika katika hospitali hiyo mjini Iringa leo 
Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Manispaa Dk. May Alexander akitoa maelekezo kwa 
Mwenyekiti wBodi ya Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF), Balozi Ally Mchumo kuhusu hospitali ya Frelimo

 Mwenyekiti wBodi ya Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF), Balozi Ally Mchumo akitandika moja ya vitanda vya Hospitali ya Manispaa ya  Iringa  eliyopo   Frelimo.
.........................................................................................................
Na Denis Mlowe  wa Francisgodwin.blogspot.com Iringa
MWENYEKITI wa Bodi ya Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF), Balozi Ally Mchumo amesema wale wote watakaobainika kugushi madai na wale watakaobainika kutaka kupata huduma ya bima ya afya kwa ulaghai watachukuliwa hatua kali za kisheria.

Balozi Mchumo alisema kumekuwepo na ongezeko la wanaogushi madai ili kujipatia fedha jambo ambalo linahatarisha uhai wa mfuko huo hivyo ni vema watu na wadau mbalimbali wakaacha tabia hizo ili kuuwezesha mfuko kufikia lengo lake la kuwafikia watanzania wote kwa kuanzia asilimia 30 ifikapo mwaka 2015.

Aliyasema hayo wakati wa mkutano na wadau wa bima ya afya uliofanyika katika ukumbi wa St.Dominic  jana kuwa kuna baadhi ya watumishi wanaoghushi madai na walaghai wanaotumia huduma hiyo bila kutambulika kisheria na mfuko wa bima kama mwanachama wa mfuko huo.

Kwa upande wake Kaimu Meneja wa Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF) mkoa wa Iringa, Emmanuel Mwikwabe alisema mkoa wa Iringa walifanya ukaguzi na kubaini kuwa fomu za madai za bima ya afya hazijazwi vema na kutolipika na hakuna uwazi wa mapato yatokanayo na huduma ya bima ya afya kwa vituo vinavyotoa huduma hiyo.

Mwikwabe alisema ukaguzi huo ulibaini huduma za kugushi ambazo zilipelekea mfuko wa bima ya afya kushindwa kulipa shilingi milioni 15.3m kutokana na makosa hayo yaliyofanywa na vituo hivyo vya afya na hospitali zinazotoa huduma hiyo.

“Kutokana na huduma za kughushi, mfuko haukulipa kiasi cha Sh15.3m, Hospitali ya mkoa, Kalenga famasi, Kituo cha afya ngome, Zahanati ya Frelimo, Zanahati ya sabasaba na kituo cha Afya cha Mkwawa” Alisema Mwikwabe
Wakati huo huo mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Bima ya Afya ameikabidhi Hospitali ya Halmshauri ya Manispaa ya Frelimo mashuka 60 yenye jumla ya thamani ya shilingi laki 9 kwa uongozi wa hospitali hiyo kwa ajili ya wodi ya wazazi.

Awali Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo Dk.  Hassan Mtani alizitaja changamoto  hospitali kuwa ni  pamoja na kutopatikana kwa huduma zote zinazotolewa na mfuko na upungufu mkubwa wa dawa na watumishi.

Aidha alisema ubovu wa miundo mbinu ya kufika katika hospitali hiyo licha ya juhudi za serikali kuahidi kujenga barabara kwa kiwango cha lami,kupanda kwa gharama za dawa, upungufu mkubwa wa dawa katika baadhi ya vituo vilivyosajiliwa na mfuko na vituo vya huduma kutokutumia fursa ya mikopo ya vifaa tiba na uboreshaji wa majengo ya mfuko ili kuboresha huduma.
Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA